Niwafanyaje watu hawa

Mabrek

Senior Member
Sep 17, 2013
125
21
habari ndugu zangu poleni na majukumu na pia asanteni kwa ushauri na elimu mnayotoa kwa wananchi kupitia jukwaa hli, suala langu ni moja tu mim ni mwalimu na kama ilivo kawaida sehemu za kazi watu husemana sasa kuna mwalmu mwenzangu kanisema vibaya sana kwa mkuu na rai wengne wa mtaani bahati nzuri kuna mzee akaniaeleza mambo hayo na kunitajia muhusika alie mwambia mambo hayo so nahtaj niwashtak ili watoe usibitisho kwan binafs naamin naonewa tu hakuna ukweli wowote ni umbea wa kujipendekeza kwa mkuu ili waendelee kupata vichance vdogovidogo na kuwachafua wengne,niwafanyaje watu hawa kisheria.asanteni
 
Mm nakushauri kaa kimya tu,Ww umiza kichwa namna ya kupamba na ugumu wa maisha ukitegemea huruma ya mkuu hakika hufiki sehemu,Jikite kwenye mambo yako mengine yakiutafutaji ,haya mambo makazini yapo sana na huwezi kuyakwepa kwa kupambana nao kihivyo,Chamsingi ww simamia haki na utende haki mkuu naye ni binadamu kama watu wengine ukweli utajulika wakati ww ukiwa umeshapiga hatua
 
habari ndugu zangu poleni na majukumu na pia asanteni kwa ushauri na elimu mnayotoa kwa wananchi kupitia jukwaa hli, suala langu ni moja tu mim ni mwalimu na kama ilivo kawaida sehemu za kazi watu husemana sasa kuna mwalmu mwenzangu kanisema vibaya sana kwa mkuu na rai wengne wa mtaani bahati nzuri kuna mzee akaniaeleza mambo hayo na kunitajia muhusika alie mwambia mambo hayo so nahtaj niwashtak ili watoe usibitisho kwan binafs naamin naonewa tu hakuna ukweli wowote ni umbea wa kujipendekeza kwa mkuu ili waendelee kupata vichance vdogovidogo na kuwachafua wengne,niwafanyaje watu hawa kisheria.asanteni

Yani unataka uwashtaki at the same time unauliza uwafanyaje? Wapikie chips
 
Nothing to deal with out there! It is too hard to establish a course of action in that scenario!
 
Pole yako. Ukianza kusikiliza na kufuatilia maneno umekwisha. Mwambie huyo mzee aliyekuambia hayo maneno na hata watu wengine wa karibu yako wakisikia tena mahali watu/wafanyakazi wenzio wanakusema/wanakukuteta wasikwambie kabisa. Chapa kazi, tenda mema/haki na sali sana hao wajinga watanyamza bila kunyamazishwa siku yao ikifika
 
Pole sana ndugu hii ndiyo dunia. Watanzania tunapaswa kubadilika. sidhani kama ni sahihi kumshauri mtu ampikie chips, nadhani haya ni majibu ya wataalumu wa kufuga nyuki kule Tabora, wanasheria wana wivu wakisheria, hivyo yapaswa kumshauri kisheria kama alivyoomba mtz mwenzetu. kwako wewe mhanga kuna mambo mengi ya kutizama labda wakati fulani nikipata nafac nitaelezea zaidi. kosa hili kama litathibitika basi linaitwa kosa la madhara(torts or wrong) sasa kosa hili limenyumbulishwa katika vipengele vingi sana inategemea umepata madhara namna gani ni kivipi. si hiyo tu lakini pia ni kwakiasi gani maneno hayo yamesambaa na watu wamekuchukulia vipi ukilinganisha na wakati kabla maneno hayo hayajasambazwa. pia unatakiwa kabla ya lolote lile tafuta mazingira ya usuhuluhishi kama akikana au kuto tii basi chukua hatua za kisheria dhidi yake. sina tafsri nzuri ya kiswahili, lakini kwa kimombo cha kisheria tunaita defamation ambazo zimegawanyika makundi mawili nayo ni libel naslander. libel ni madhara yatokanayo na uzushi kwa njia ya mdomo na slander ni uzushi kwa njia ya maandishi. kwahiyo kwako wewe utafungua jalada kwa libel...............
 
Ukifuata hayo utakuwa kila siku mahakamani, nanivyema ukaeleza wazi hiko alichosema ili tujue km kina madhara na mashiko kisheria. Kwani mtu anaweza alajisemea tu ku Bibi x akivaa Nguo wala hapendezi, wewe litakuudhi lakini kisheria hilo swala halina mashiko, lakini pia jua kuwa inawezekana kweli hupendezi. Chamsingi nikulitafakari kabla ya kwenda mahalamani mwisho wasiku ukishindwa kuthibitisha unaweza kushitakiwa wewe ulipe gharama
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom