Nivaeje baada ya kuolewa?

vaa nguo ambayo inakufanya uwe confo na ambayo mumeo anairidhia,kama anaridhika utoke na bikini we vaa tu aibu itabaki kwako na kwa mumeo
 
unatakiwa ujiheshimu ili uheshimiwe na ujithamini ili uthaminiwe ... usijitangaze kwa kuwa si biashara
 
Ni wakati wakujistiri vizuri ukishaolewa, uvae nguo ndefu kupita magoti yako, usiache maeneo tamanishi ya mwili wako yakiwa wazi,

NB: jua kuwa wewe ni mke wa mtu,
1. Jitunze
2. Jithamini
3. Jiheshimu nawe utaheshimika...

pia muheshimu umpendae na umtunzie heshima yake hata katika mavazi unayovaa
 
Acha vile vi-top vyako vya kitovuni,vimini, vim'pasuo vya mapajani,vi-blouse vinavyoonyesha maziwa,vim'bato vyako vinavyo-onyesha mpaka uvimbe wa uchi wako nk.Inshort vaa ngua zinazositiri mwili wako.Hatimaye mvae Yesu.

Mh nimecheka sana hapo kwenye Red!
 
Juzi tulikuwa sehemu na mada hii ikaibuka! Vipi mwanamke aliyeolewa avae vipi? Huyu dada aliyepekea hoja ianze ni mnene asiye na upungufu wa nyama mwilini! Bantu haswa! Lakini kavaa 'skini taiti', kishati kidogo kiloacha sehemu ya kifua chake kikubwa nje. Mguuni kipo kikuku! Mkononi ana pete ya ndoa ilobebana na ya engagement kuonesha ni mke wa mtu! Mke wa mtu, utokeje?

Mke wa mtu akipiga tenge anapendeza sana na mimi napenda sana
 
Nakubaliana na wewe, Mwanandoa anapaswa kuvaa vile mumewe anavyotaka. Pia akumbuke kujiheshimu na kuwaheshimu wengine pia ili kuondoa unnecessary misunderstanding.

Sikubaliani na wewe; mwanamke akiolewa siyo kwamba anaacha kuwa binadamu kamili mwenye utashi na mapendezi yake mwenyewe! Mkitaka wa hivyo tengenezeni marobot mnayo yaprogram kufanya yale mnayo yataka. Na sorry to tell you some truth, you will end up a very unhappy man if u expect a woman to do kile tu unachomtaka afanye, coz she will definetely disappoint you!

About the topic; vaa what you feel is appropreate to you, angalia hali ya hewa kwa maana ya material ya nguo unayovaa, angalia purpose (kama mwanzo ulivaa kwa ajili ya kumattract mwanaume, you dont need to coz the purpose has been fulfilled alread), angalia wapi unaenda (kama ni kanisani, msikitini, msibani, club, picnic, hunting, jogging etc) na social expectation.
 
Ikiwa mwanamke anatakiwa kuvaa kama mumuwe atakavyo manake na mume avae kama mke atakavyo?
 
vaa nguo ambayo inakufanya uwe confo na ambayo mumeo anairidhia,kama anaridhika utoke na bikini we vaa tu aibu itabaki kwako na kwa mumeo

Ukipata mume kichaa si utaishia kujidhalilisha?
 
kuna wanaume wengine wanapenda wake zao wavae nguo za kubana.kuna kaka mmoja alimuoa mschana ambae alikuwa mtu wa kuvaa ushungi.akawa anamwambia mke kuanzia leo,ushungi pembeni,na uvae jeans ambazo zipo tight.mke akawa anavaa hivyo,wacha aanze kusemwa njekwa wanaomfahamu huyo mwanamke.baadae alishindwa,akamwambia mume wake,hivi vitu sijazoea,akarudi tena kwenye ushungi wake.kwa hiyo ndoa ni makubaliano yenu wenyewe,ingwa wengine huwa wanayoambiwa hawafati
 
Ndio kusema mwanamke akishaolewa hana uhuru namna ya yeye kuvaa?
 
Sikubaliani na wewe; mwanamke akiolewa siyo kwamba anaacha kuwa binadamu kamili mwenye utashi na mapendezi yake mwenyewe! Mkitaka wa hivyo tengenezeni marobot mnayo yaprogram kufanya yale mnayo yataka. Na sorry to tell you some truth, you will end up a very unhappy man if u expect a woman to do kile tu unachomtaka afanye, coz she will definetely disappoint you!

About the topic; vaa what you feel is appropreate to you, angalia hali ya hewa kwa maana ya material ya nguo unayovaa, angalia purpose (kama mwanzo ulivaa kwa ajili ya kumattract mwanaume, you dont need to coz the purpose has been fulfilled alread), angalia wapi unaenda (kama ni kanisani, msikitini, msibani, club, picnic, hunting, jogging etc) na social expectation.

Nimekusoma Kaunga! Hivyo ndo kusema mwanaume hawezikuamua mkewe avaaje?
 
Vaa vile anavyopenda mume wako.
Usiache nafasi ya yeye kunung'unika kwamba unajionyesha sana au kubaki anatamani ungevaa hivi au vile.
 
Wanaweke wengine yaan wakishaolewa ndo wanataka kuonyesha kuwa bado wana "run the shit"..***** huo na akuna anayependa mkewe atamaniwe kingono ngono.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom