Niulize swali lolote kuhusu Wilaya ya Kilombero

Kabila la Wavidunda liko Idodi, Kilosa! Nawafahamu Wavidunda ambao asili yao ni Kisaki Morogoro Vijijini kandokando ya reli ya Tazara, wengine walihamia Wilaya ya Kisarawe, Pwani. Nadhani hata ninyi mmetokea Kisaki Morogoro

Vv
Vyamavingi, utatakiwa uwaombe radhi wavidunda kwa kuipotosha historia na chimbuko lao. Kifupi ulichoeleza hakishabihiani kabisa na ukweli kuhusu kabila hili adhimu. Nitakuja na uzi kuhusu wavidunda panapo majaaliwa.
 
Hongereni sana, barabara za Idodi-I fakara ni noma. Vipi barabara za Ifakara-Mlimba na Lupilo-Malinyi? Na zenyewe zinawekwa lami?

Vv
Chini ya uongozi wa Jemedari Dkt John Pombe Magufuli, mipango ya kuzitengeneza barabara hizo kwa kiwango cha lami ipo. Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umekamilika.
 
Kilombero Sugar company, ina viwanda viliwi. Kilombero One na Kilombero 2. Kilombero One kiwanda kipo Wilayani Kilombero. Kilombero 2 kiwanda kipo wilayani Kilosa. Viwanda hivi vinakaribia sana na vinatenganishwa na mto ruaha ambao ndio mpaka wa wilaya ya Kilombero na Kilosa kwa umbali usiozidi Kilometa 5. Jibu Kilombero kama wilaya inacho Kiwanda cha Sukari ambacho ni Kilombero One.
Thanks mkuu.....Kale kajamaa lijualikali kashamba ka ifaraka kalisema hakuna kiwanda cha sukari hapo
 
Wakuu, mwenye kutaka kujua lolote/ chochote kuhusu Wilaya ya Kilombero iliyopo mkoani Morogoro, aulize nitamjibu. Iwe ni fursa za kibiashara, kilimo, siasa nakadharika.... !
Karibuni kwa maswali,
Karibuni Kilombero.
Wenu Mvidunda.
Mambo vp mkuu, gharama ya kilimo cha miwa ikoje kwa heka moja. na inachukua mda gani hadi uvunaji?
 
Huyu mleta mada anajiita mvidunda kiasili ni mtani wangu huyu, hili kabila moja dogo sana liliopo mkoa WA morogoro wilaya ya kilosa, sehemu inayoitwa kidodi, hawa wanaa mlimani hukoo na shughuli yao kubwa NI kilimo cha maharage niliwai kwenda kwa hawa jamaa huko kwa wavidunda aiseee yaani unakwenda kwa miguu unapandisha milima mpaka unaomba po, hajui vizuli wilaya ya kilombore huyu maana yeye asili yake kilosa, jamani. Kumbukeni huyu mtani wangu sasa ww ukiarib simoooooo,
Asili ya jina la kilombero limetokana na mto kilombero ambao mto huo umetenganisha wilaya ya kilombero mahenge ,watu WA kilombelo wanategemea kilimo hasa cha mpunga kwa ajili ya chakula na biashara japo kwa sasa kuna kilimo cha miwa lkn wanaolima miwa NI watu wachache sanaaa , ukiawa mgeni kuhusu kununua mpunga kwa ajili ya biashara NI changamoto kubwa sana kwa maana mpunga unaweza kuwa mmbovu kwa kuchelewa kuvunwa au ulianguka ktk maji wakati ushakomaaa hii hupelekea mchela kuwa mbaya sasa kama mgeni na mpunga huwezi kuyajua haya utauziwa mpunga mmbovu na mwisho WA cku utazika mtaji wako, kuhusu miwa nayo ina changamoto sana hakuna biashara ambayo haina hasara, unaweza ukalima miwa na mwisho wa cku usivunjwe kutokana na mazingira Fulani Sasa miwa isipovunjwa unatakiwa ww mwenye Shamba uifyeke ili mvua ikinyesha ipate kuchipua tena maaana miwa iliolalia shamba kiwandani haitakiwi,
Shamba linaweza kuungua kabla ya muda hiyo kwko pia NI changamoto nk ,,
Kuhusu kulima mpunga nenda mapema kuanzia mwezi WA 8 ukodi Shamba urubili msimu WA kilimo ujumuike na wana Zengo, ,mwenye swali akuje tafadhali
Hapana mkuu miwa inavunwa hata kama itapitiliza msimu bila kuvunwa msimu ujao utavujiwa bila shida tena hata tani zitaongezeka sababu miwa itachipua mingine mule mule... pia kama shamba lako litaungua kwa ajari pia utavuniwa (ila lazima utatoa rushwa) na utalipa shling laiki moja kama faini ya uzembe wa kutoweka fire break kubwa..
 
Back
Top Bottom