Niulize swali lolote kuhusu Wilaya ya Kilombero

Samahani hivi migomba na Ndizi ni mazao tofauti
Kilombero ni bonde lililo barikiwa na Muumba. Mazao kama mpunga, mahindi, migomba/ndizi , alizeti, mihogo, ufuta, viazi vitamu , nyanya maji na aina nyingi za mboga mboga na matunda yanastawishwa wilayani hapa. Pia maeneo kama Mbingu Cocoa inastawi vizuri.
 
Kuna member amejibu swali lako. Ushauri jitahidi kuuliza maswali ambayo majibu yake yanaweza kuwa na tija kwako na kwa members wengine. Ukijuaa asili ya jina Kilombero inakusaidiaje. Acha uchadema.
Ushaanza kuleta siasa sana mwanalumumba
 
Nitalijibu swali hili japo lipo nje ya eneo nilotaka kuulizwa kwalo. Kidodi ni wilaya ya Kilosa sio Kilombero. Hali ya usalama ni nzuri mno na hakuna matukio ya ujambazi/uporaji yanayoripotia. Kamanda wetu Mutafungwa (RPC) ameufanya mkoa wa Morogoro kuwa mahali salama mno pa kuishi.
Niungane nawe kwa asilimia 109, kwa sisi wazurulaji Kamanda Mutafungwa kaufanya Morogoro kuwa salama SANA, nahisi wale maaskari, vile vikundi vya waliokuwa CORRUPT kawanyoosha..

Mnyonge tumnyonge ila haki yake tumpe, suala la za kubrashia viatu, hizi ka zilishaidhinishwa tokea JUU..

Everyday is Saturday............................ :cool:
 
hekari 3000 za kulima mpunga zinapatikana?
Ukihitaji seriously, unaenda mkoani kama investor, unajadiliwa naamini unapewa Morogoro hasa huko ni ina maeneo makubwa, ukikosa Kilombero utapewa Malinyi, Ulanga, Mvuha e.t.c

Everyday is Saturday........................:cool:
 
Eka moja ya kilimo cha miwa inagharimu kiasi gani mpaka uvunaji? Na je faida ya soko lake Kwa eka ina range kiasi gani?
1.5 Million. Faida kwa mwaka wa kwanza mavuno unaweza kupata 1M. Miaka itakayofuata utapata si pungufu ya 2M.
 
Watu wa kilombelo inasemekana asilimia kubwa watu wanaishi bila kuoana je NI KWELI
(Mfano; MKAMBA VL)
Sio kweli. Kilombero ni kisima na chimbuko la ustaarabu. Wananchi wilayani hapa wanaiishi mila na desturi huku wakizifuata dini walizopokea kwa wageni. Suala la ndoa wanalizingatia sana...
 
Hakuna wilaya ya kilombero siku hizi , wilaya imeshazikwa siku nyingi sasa hivi kuna wilaya ya mlimba na TC ifakara.
Nadhani huelewi ama hujatia bidii kwenye kuelewa/ kueleweshwa. Kilombero ni wilaya na bado ni wilaya hakuna wilaya ya Ifakara wala Mlimba bali kuna Halmashauri tatu nazo ni Halmashauri ya Ifakara mji, Halmashauri Mama ya Kilombero na Halmashauri ya Mlimba. Zote zipo chini ya mkuu wa wilaya ya Kilombero. Inasemwa kuwa huenda Mlimba ikapata wilaya, bado hakuna hakika.
 
Kuna kambwa kanasema ni kajanja ka Kilombelo kalisema kilombelo hakuana kiwanda cha sukari ni kweli?
Kilombero Sugar company, ina viwanda viliwi. Kilombero One na Kilombero 2. Kilombero One kiwanda kipo Wilayani Kilombero. Kilombero 2 kiwanda kipo wilayani Kilosa. Viwanda hivi vinakaribia sana na vinatenganishwa na mto ruaha ambao ndio mpaka wa wilaya ya Kilombero na Kilosa kwa umbali usiozidi Kilometa 5. Jibu Kilombero kama wilaya inacho Kiwanda cha Sukari ambacho ni Kilombero One.
 
Huu uzi umenikumbusha nyumbani..

Hivi mkuu, vipi shughuli za uvuvi kwa kipindi hiki mto Kilombero? Kuna makambi ya wavuvu (Ngemani, Kahema, Luono, Senga n.k).. hv haya makambi bado yapo na shughuli za uvuvi bado zinaendelea?

Vipi wafugaji bado wapo pia maeneo hayo? Mara ya mwisho serikali ilipiga marufuku shughuli za kiufugaji.

Naombeni details wana Kilombero maana maeneo tajwa hapo yalifanya nisiujutie ufugaji.
 
Mtani ni kweli Mimi ninatoka kabila dogo sana lililo sheheni watu werevu la wavidunda linalopatika Kidodi wilayani Kilosa. Nimezaliwa na kukulia wilayani Kilombero. Ni wilaya ninayoifahamu kuliko wilaya yoyote hapa nchini. Maelezo yako yanaukaribia ukweli japo umeelezea changamoto tu pasipo kugusia mafanikio ambayo ndiyo kitovu cha maendeleo ya Kilombero na watu wake.
Kabila la Wavidunda liko Idodi, Kilosa! Nawafahamu Wavidunda ambao asili yao ni Kisaki Morogoro Vijijini kandokando ya reli ya Tazara, wengine walihamia Wilaya ya Kisarawe, Pwani. Nadhani hata ninyi mmetokea Kisaki Morogoro

Vv
 
Ni kweli , Kipande cha barabara Kidatu Ifakara Km 61 ni kipande korofi chenye adha nyingi kwa wasafiri na wasafirishaji. Asante Jemedari wetu kipenzi cha Watanzania, Rais John Magufuli, punde adha ile itakuwa historia. Mkandarasi yupo site na kasi ya Ujenzi inaridhisha. Ni Ujenzi wa kiwango cha lami. Ukija mwakani utastareheka mpaka Lifuakara/tamka Ifakara.
Hongereni sana, barabara za Idodi-I fakara ni noma. Vipi barabara za Ifakara-Mlimba na Lupilo-Malinyi? Na zenyewe zinawekwa lami?

Vv
 
Kabila la Wavidunda liko Idodi, Kilosa! Nawafahamu Wavidunda ambao asili yao ni Kisaki Morogoro Vijijini kandokando ya reli ya Tazara, wengine walihamia Wilaya ya Kisarawe, Pwani. Nadhani hata ninyi mmetokea Kisaki Morogoro

Vv
Vyamavingi, utatakiwa uwaombe radhi wavidunda kwa kuipotosha historia na chimbuko lao. Kifupi ulichoeleza hakishabihiani kabisa na ukweli kuhusu kabila hili adhimu. Nitakuja na uzi kuhusu wavidunda panapo majaaliwa.
 
Back
Top Bottom