Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilombero aondolewa

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
MENEJA WA TARURA WILAYA YA KILOMBERO AONDOLEWA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor H. Seff amemuondoa kwenye majukumu yake aliyekuwa Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilombero kwa kushindwa kusimamia kikamilifu miradi ikiwemo ujenzi wa Boksi Kalavati katika Barabara ya Mawala-Mofu-Ikwambi Km 30 iliyopo Halmashauri ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Hayo yamejiri baada ya Kiongozi huyo kufanya ziara ya ukaguzi wa miradi wilayani Kilombero na kubaini mapungufu katika usimamizi wa miradi ikiwemo ujenzi wa boksi kalavati katika barabara ya Mawala-Mofu-Ikwambi ambalo limejengwa chini ya viwango vya mkataba hali iliyompelekea kumuondoa mara moja Meneja wa TARURA wa Wilaya hiyo.

“Nimekagua na kujiridhisha kwamba mradi huu umejengwa chini ya kiwango, kwakweli sijaridhishwa kabisa na usimamizi wa hapa, hivyo nimemuondoa kwenye nafasi yake kuanzia leo aliyekuwa Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilombero na atapangiwa majukumu mengine”, alisema Mhandisi Seff.

Aidha, Mtendaji Mkuu amemtaka Mkandarasi aliyejenga mradi huo chini ya viwango vya mkataba kubomoa kwa gharama zake na kukamilisha ujenzi wa Boksi Kalavati jipya ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

Pia, Mhandisi Seff amewataka Mameneja wa TARURA nchi nzima kusimamia kikamilifu miradi kwenye maeneno yao na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atayeshindwa kutimiza majukumu yake ili kuhakikisha fedha inayotolewa na Serikali inaendana na ubora wa miradi inayotekelezwa.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) unaendelea na kazi ya kusimamia ujenzi, ukarabati na matengenezo ya mtandao wa barabara za Wilaya wenye jumla ya KM 144,429.77 nchi nzima ili kuhakikisha wananchi wanazifikia huduma za kijamii na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.
IMG-20221016-WA0156(4).jpg
IMG-20221016-WA0155(4).jpg
IMG-20221016-WA0154(4).jpg
 
Clip ya uozo wa TARURA katika usimamizi wa culvert hiyo ya Mofu imesambaa mitandaoni kwa muda sasa.
Eng Sefu kashituka just in time, lakini tatizo la TARURA ni usimamizi wa miradi yote.
Inabidi waige business model ya TANROADS.
 
Akiondolewa kazumi ndio inakuwa imeisha au this is just the beginning of the trauma?
 
Kuna mhandisi wa TARURA wilaya ya Ubungo nae afuatiliwe sana.
Kuna kipande cha batabara ya Makabe kiliwekwa bango la kuweka lami kwa KM 1 lakini wameweka lami tena mbovu hata mita 500 hazikufika na bango liliondolewa hata ujenzi haujakamilika!
Mhandisi Victor tunaomba na hili fuatilia kwa nguvu zote na TAKUKURU saidieni mnalala sana!
 
MENEJA WA TARURA WILAYA YA KILOMBERO AONDOLEWA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor H. Seff amemuondoa kwenye majukumu yake aliyekuwa Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilombero kwa kushindwa kusimamia kikamilifu miradi ikiwemo ujenzi wa Boksi Kalavati katika Barabara ya Mawala-Mofu-Ikwambi Km 30 iliyopo Halmashauri ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Hayo yamejiri baada ya Kiongozi huyo kufanya ziara ya ukaguzi wa miradi wilayani Kilombero na kubaini mapungufu katika usimamizi wa miradi ikiwemo ujenzi wa boksi kalavati katika barabara ya Mawala-Mofu-Ikwambi ambalo limejengwa chini ya viwango vya mkataba hali iliyompelekea kumuondoa mara moja Meneja wa TARURA wa Wilaya hiyo.

“Nimekagua na kujiridhisha kwamba mradi huu umejengwa chini ya kiwango, kwakweli sijaridhishwa kabisa na usimamizi wa hapa, hivyo nimemuondoa kwenye nafasi yake kuanzia leo aliyekuwa Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilombero na atapangiwa majukumu mengine”, alisema Mhandisi Seff.

Aidha, Mtendaji Mkuu amemtaka Mkandarasi aliyejenga mradi huo chini ya viwango vya mkataba kubomoa kwa gharama zake na kukamilisha ujenzi wa Boksi Kalavati jipya ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

Pia, Mhandisi Seff amewataka Mameneja wa TARURA nchi nzima kusimamia kikamilifu miradi kwenye maeneno yao na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atayeshindwa kutimiza majukumu yake ili kuhakikisha fedha inayotolewa na Serikali inaendana na ubora wa miradi inayotekelezwa.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) unaendelea na kazi ya kusimamia ujenzi, ukarabati na matengenezo ya mtandao wa barabara za Wilaya wenye jumla ya KM 144,429.77 nchi nzima ili kuhakikisha wananchi wanazifikia huduma za kijamii na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.
Hakuna mradi wa TARURA unaokuwaga kwenye kiwango labda kwetu huku sijawahi ona wanaujinga mwingi sanaaaaa.

Kila mwaka huku kwetu wanakuja timua vumbi kwenye barabara yetu hawaweki kifusi cha maana wanajaza mawe tu na ikinyesha mvua ni tope tu mwaka wa3 mfululizo kazi ni kuwekewe mawe na msimu wa mvua mawe kusombwa na maji tunabaki kucheza kwenye tope tu

Huu utaratibu mtu kaharibu anapangiwa kazi nyingine ni upi mbona makosa ya kiutumishi na adhabu zake ziko double standard sana kwanini asifilisiwe na akafukuzwa kazi?

Aende apewe kazi nyingine akiharibu tena anahamishiwa anapewa kazi nyingine watu hawajui kuwa responsible na makosa yao nikama manaandaaana chain ya kufichianaaaa makosa.
 
View attachment 2389004
Clip ya uozo wa TARURA katika usimamizi wa culvert hiyo ya Mofu imesambaa mitandaoni kwa muda sasa.
Eng Sefu kashituka just in time, lakini tatizo la TARURA ni usimamizi wa miradi yote.
Inabidi waige business model ya TANROADS.
Hapa Mikumi Tanzam road kuna km kama Saba hivi zina mawimbi kama vile mawimbi ya ndege ikiwa anga za juu(turbulence) kuna water table in some area,na solution ni kusuka zege kwa nondo na smenti,,lakini kila siku wanaigusa na parking yote haidumu hata miexi kila ikitengenezwa,huu ni kutiana shida,Takwimu zinaonyesha Afrika inatumia resources kibao ktk Barabara wakati pesa zenyewe ni za mikopo,tunaomba watawala msuke zege maeneo korofi kama kidodi,kifinga kwa kuwa kuna vijito vingi na water table iko on surface wakati wa mvua
 
Kweli mkuu, lakini barabara a TANZAM Highway ni miradi ya Trunk roads chini ya TANROADS.
Ila toka Iyovi hadi Mikumi na kuja Morogoro barabara hii inahitaji reconstruction.
 
MENEJA WA TARURA WILAYA YA KILOMBERO AONDOLEWA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor H. Seff amemuondoa kwenye majukumu yake aliyekuwa Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilombero kwa kushindwa kusimamia kikamilifu miradi ikiwemo ujenzi wa Boksi Kalavati katika Barabara ya Mawala-Mofu-Ikwambi Km 30 iliyopo Halmashauri ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Hayo yamejiri baada ya Kiongozi huyo kufanya ziara ya ukaguzi wa miradi wilayani Kilombero na kubaini mapungufu katika usimamizi wa miradi ikiwemo ujenzi wa boksi kalavati katika barabara ya Mawala-Mofu-Ikwambi ambalo limejengwa chini ya viwango vya mkataba hali iliyompelekea kumuondoa mara moja Meneja wa TARURA wa Wilaya hiyo.

“Nimekagua na kujiridhisha kwamba mradi huu umejengwa chini ya kiwango, kwakweli sijaridhishwa kabisa na usimamizi wa hapa, hivyo nimemuondoa kwenye nafasi yake kuanzia leo aliyekuwa Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilombero na atapangiwa majukumu mengine”, alisema Mhandisi Seff.

Aidha, Mtendaji Mkuu amemtaka Mkandarasi aliyejenga mradi huo chini ya viwango vya mkataba kubomoa kwa gharama zake na kukamilisha ujenzi wa Boksi Kalavati jipya ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

Pia, Mhandisi Seff amewataka Mameneja wa TARURA nchi nzima kusimamia kikamilifu miradi kwenye maeneno yao na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atayeshindwa kutimiza majukumu yake ili kuhakikisha fedha inayotolewa na Serikali inaendana na ubora wa miradi inayotekelezwa.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) unaendelea na kazi ya kusimamia ujenzi, ukarabati na matengenezo ya mtandao wa barabara za Wilaya wenye jumla ya KM 144,429.77 nchi nzima ili kuhakikisha wananchi wanazifikia huduma za kijamii na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.
View attachment 2388988View attachment 2388989View attachment 2388990
Katika utekelezaji wa kazi hii, TARURA inabidi waeleze umma , msimamizi(consultant) alikuwa wapi wakati madudu yanafanyika?
Utekelezaji wa structures kama hizi ni lazima Consultant awepo na kutoa maelekezo ili kazi iendelee.
Je alikuwepo?
 
Kazi zote za Consultant ni wao wenyewe Tarura.
Value for money haiwezi kufanywa na client mwenyewe,lazima patakuwepo na hujuma among client staffs.
Na kama Kuna Mkandarasi,fahamu wenye kampuni ni sehemu ya watumishi au pengine Kuna uchepushaji wa funds kwenye mifuko ya waliowapatia Kazi.
Usimamizi makini hauwezi kufanyika iwapo wasimamiaji walipewa % fulani ya fedha za mradi husika.
Ni muhimu kushirikisha private consultants,hata kama mradi ni 100Mln, haiwezekani Mkandarasi awepo alafu Consultant asiwepo.
Consultant asiwe ni sehemu ya client,vivyo hivyo na Mkandarasi asiwe ni sehemu ya wenye Kazi.
Utaratibu wa ugawaji wa zabuni uangalie upya,ikiwezekana consulting firms zipewe mandate ya/kuwa sehemu ya evaluations team katika kandarasi husika.
 
Kazi zote za Consultant ni wao wenyewe Tarura.
Value for money haiwezi kufanya na client mwenyewe,lazima patakiwepo na hujuma.
Na kama Kuna Mkandarasi,fahamu wenye kampuni ni sehemu ya watumishi au pengine Kuna uchepushaji wa funds kwenye mifuko ya waliowapatia Kazi.
Usimamizi makini hauwezi kufanyika iwapo wasimamiaji walipewa % fulani ya fedha za mradi husika.
Ni muhimu kushirikisha private consultants,hata kama mradi ni 100Mln, haiwezekani Mkandarasi awepo alafu Consultant asiwepo.
Consultant asiwe ni sehemu ya client,siku hizi Kuna tabia ya Taasisi za Serikali kutengeneza Consulting firm ili kusimamia miradi inayohusu Taasisi zao kitu ambacho ni kinyume na Construction practice hivyo kusababisha mgongano wa kimaslahi.
Safi mkuu.
Ninavyojua, pengine nisahihishwe, TARRA hawana hata idara ya kusimamia kazi kama ilivyo TANROADS.
TANROADS wanayo TECU(Tanroads Engineering Consulting Unit).
Hawa TARURA bado ati wanajisimamia wenyewe, na ndio maana huyo Meneja ameliwa kichwa.
Its impossible Client akasimamia kazi site on a day-to-day basis.

Hili somo inabidi serikali iliewe maan TARURA wamerithi mainjinia wengi toka Halmashauri za Wilaya na uwezo wao kwa kweli ni mdogo sana kusimamia miradi.
Huu basi ni ushauri kwa TARURA, hawa watu waliza wawepo kusimamia kazi hata kama ni ndogo:
1. Project In charge toka kwa Client
2.Consultant Engineer
3.Contractor

Hao waspokuwepo tutegemee madudu tu toka kazi zote za TARURA.
 
Ni Wakati sasa kwa Sekta ya Ujenzi kufanyiwa REVIEW kuanzia Taasisi za Wizara hadi Private entities ili kulinda Professionals, kukuza ajira kwa wote,kujenga Miundombinu imara yenye kuondoa umaskini na kuongeza uwajibikaji na ufanisi kwa wadau wa Ujenzi/Majenzi bila uwepo wa mgongano wa kimaslahi.
 
Wazo jema sana.
Kwa miaka mingi watu hasa wanasiasa waliojitia kuijua sekta ya ujenzi wameiharibu sana kiutendaji.
 
View attachment 2389004
Clip ya uozo wa TARURA katika usimamizi wa culvert hiyo ya Mofu imesambaa mitandaoni kwa muda sasa.
Eng Sefu kashituka just in time, lakini tatizo la TARURA ni usimamizi wa miradi yote.
Inabidi waige business model ya TANROADS.
  1. Kwanini mnakwenda kukagua dakika ya mwisho mambo yamesha haribika?
  2. Kwanini hiyo timu nzima haijawekwa ndani kwa uhujumu uchumi badala yake ni hadithi za kumsifia Rais kwa kutafuta fedha?
 
We mwanasiasa inaelekea mada wala huielewi.
Unachokielewa vizuri ni jela tu.
 
Mpaka sasa utendaji wa hovyo umekuwa ni sehemu ya Kaulimbiu na sera za chama tawala.
JPM alivyokuwa ana shughulika na kutoa dozi za hiyo minyooo mlimuona ni Dikteta.

sasa na tuendelee kuimba, kazi iendelee
 
Magufuli aliharibu sana sekta ya ujenzu kiutendaji.
Force Account imechafua sana sekta na matokeo yake tutayaona ndani ya hii miaka kumi.
 
Back
Top Bottom