Niulize chochote kuhusu vipimo vya Maabara za Afya

Niulize chochote kuhusu vipimo vya Maabara za Afya

Mleta mada Fundisanifu uko vizuri sana. Ninatamani upate Ajira then ujikusanye upate mtaji ufungue laboratory yako. Yaani you are the smartest Lab Physician. Keep it up
mkuu mimi sio smartest kwasababu wako wengi pia walioko smart kuliko mimi.. na huenda wengine siwafaham!
 
Hii kozi npo mwaka wa 1 diploma,broo umenitisha since 2018 hujapata pakujishikiza
 
Hii kozi npo mwaka wa 1 diploma,broo umenitisha since 2018 hujapata pakujishikiza
Usitishike, the future is beautiful and yet to come!, Hakikisha unajua vitu ukimaliza.
 
Shikamooni wakuu.

Mimi ni muhanga wa tatizo la ajira, na pia kabla ya hilo ni mtaalamu(mteknolojia) wa maabara(Laboratory technician) mwenye diploma ambayo nimeipata kutoka BUGANDO mwaka 2018..

Pia, katika kukaa sana mtaani nimegundua kua nina muda mwingi sana, japo baadhi hua nautumia katika kutafuta kazi.

Nimetafakari sana na kujiona mimi ni mbinafsi maana kila siku natafuta ajira kwa manufaa yangu na familia yangu.. hivyo nimeamua kwa elimu hii niliyonayo niwanufaishe na wengineo, maana hakuna msaada mwingine nnaoweza kuutoa kwenu zaidi ya elimu yangu.

Sasa naomba kutumia fursa hii, kuwapa ruksa na kuwaomba mniulize chochote kuhusiana na maabara ya afya, ku-interpret vipimo ama kutoa ushauri wa juu ya kipimo gani ufanyiwe.

Kama umeona sehemu ukakasi naweza kukusaidia katika namna ambayo nitaweza, ama kama una mashaka na majibu uliyopewa sehemu pia naweza kukuelezea vizuri kadri niwezavyo kwani kwenye kazi hii nna uzoefu wa utendaji kazi kwa miaka 2..

NB: napokea michongo ya kazi pia kupitia 0786744401,

NIULIZE, NIKUSAIDIE.

Kwa kawaida sindano ikichomwa huwa ile dawa inaingia ktk mishipa ya damu ili ifanye kazi yake sasa swali langu jee mbona huwa tunachoma sindano ktk makalio wakat ni sehemu ya nyama tupu inakuwaje hapo msahada tafadhali
 
Boss mm natka kujua comfimatory test za sickle cell ni zipi?
 
Boss mm natka kujua comfimatory test za sickle cell ni zipi?
Najaribu mkuu watakuja wenyewe kuweka Sawa ....

1. High performance liquid chromatography (HPLC)- hii ni best sababu inafanya both identifying and quantification of different Hemoglobin types including Hemoglobin S inayohusiana na sickle cell pamoja na zingine HbA, HbA2, HbF etc

2. Hb electrophoresis- hii inafanya identification ya hemoglobin types Kwa kuzifanyia separation according to their charge (it shows just presence or absence only) haifanyi quantification kujua Aina flani ya hemoglobin ipo Kwa kiasi gani kwenye sample ya mgonjwa.

3. Isoelectric focusing -hii pia ni kama hiyo hapo juu nayo inaonesha uwepo Tu wa type mbali mbali za hemoglobin kwenye sampuli ya mginjwa.

ngoja nikakatie nyasi ng'ombe Kwanza nitarudi...
 
Kaka, Kama Kuna Group au Page huko nisaidie nitembelee pia maana Ni mteknolojia ila umetema madini haswaaa!!
 
Kaka, Kama Kuna Group au Page huko nisaidie nitembelee pia maana Ni mteknolojia ila umetema madini haswaaa!!
binafsi sina mkuu ila ngoja nimtag huyu kama anayo Fundisanifu

naupenda huu uzi sababu unasaidia kurefresh vitu vingi ambapo inasaidia kujikumbusha kumbusha..si unajua ukiwa upo mtaani tu vitu navyo vina-vapour.

Ukipata connection mkuu usinisahau pia maana hii kazi ya mchanga ipo kunikosesha mke aisee....
 
Swali langu Ni hili vidonda vya Tumbo vinaweza kupimwa kwa kipimo cha Kutolewa damu???
 
Swali langu Ni hili vidonda vya Tumbo vinaweza kupimwa kwa kipimo cha Kutolewa damu???
vipimo vifuatavyo hufanyika :-

1. Kupima damu 'Blood test'
Kuangalia bakteria aina ya H.pylori na kama mgonjwa amekuwa akitumia antibayotiki au dawa za vidonda Proton Pump Inhibitors 'PPIs' mfano Omeprazole vipimo vyake vya damu vitaonyesha majibu hasi 'Negative'

2. Kupima pumzi 'Breath test'
Mgonjwa hupewa anywe maji yenye atomi za kaboni zinazoweza kuvunjika, hii hufanya bakteria H.pylori kuvunjika na baada ya lisaa mgonjwa hutoa pumzi kwenye chombo kilichofunikwa kama mgonjwa ameambukizwa sampuli ya pumzi itaonyesha vipande vya kaboni kwenye kabonidioksaidi.

3. Kupima antijeni kwenye kinyesi 'Stool antigen test'
Kipimo hiki huangalia kama kuna bakteria H.pylori kwenye kinyesi. Vilevule kipimo hiki hutumika kuangalia ufanisi wa matibabu yaliyotolewa dhidi ya bakteria.

4. X-ray ya sehemu ya juu ya tumbo 'Upper gastrointestinal x-ray'
Picha huonyesha umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach' na Dudenum. Mgonjwa humeza maji yenye 'Barium' ambayo hufanya vidonda kuonekana kirahisi kwa x-ray.

Kamera ya tumbo 'Endoscopy'. Mrija mrefu wenye kamera huingia tumboni na daktari huona vidonda kwenye skrini ya kompyuta 'Monitor'.

Mwenye uzi atajazia zaidi.
 
Samahani mkuu..

naomba kuuliza hapo pointi ya Kwanza ya "blood test" kwamba ni Kwa vipi mtu akiwa anatumia hiyo proton pump inhibitors drug itasababisha majibu "negative" nafikir ukimaanisha "false negative"? (Kifamasia)

Mtazamo wangu (kimaabara)

Mimi nafikiri hiyo test ya blood ni kuangalia protein inayozalishwa na mwili ambayo ni Kwa ajili ya ulinzi na kupambana na bwana h.pylori bakteria. ambazo ndo hizo twaziita "antibody"

kama ulivyosema mtu mwenye vidonda vya tumbo akitumia dawa anatakiwa akae wiki sita baada ya kumaliza dawa ndo aje tena kupima Kwa sababu bado hizo proteins (antibodies) zinakua zinazunguka kwenye mzunguko japo sababu ametumia dawa wadudu wanaweza kuwa washakufa. Hiyo huweza pelekea majibu tunasema "false positive" (positive ya uongo au ambayo haikupaswa kuwa positive)

lakini pia kipimo hiki cha damu hakipendelewi Sana sababu sometimes kunatokea muingiliano wa antibodies zà hpylori na zingine hivyo inaweza kukawa na antibodies zingine zenye mfanano na antibody ya h.pylori kipimo kikasoma positive kumbe ni "false positive"

kutotumia sampuli inayohitajika, kutumia kipimo kilicho expire, kufanya bila kufata maelekezo ya ufanyaji (standard operating procedures) nk zinaweza sababisha majibu ambayo ni "false negative" ama "false positive"

kipimo cha kinyesi (stool antigen test) kwangu mm naona ni nzuri zaidi.

Kufanya CULTURE ni gharama, complex na inachukua muda mrefu wadudu kuota japo ni best.
 
hua tunatumia

1. rapid test ambazo kuna SD bioline na Unigold.. Unigold ndio standard na best( confirmatory test).. kwenye pharmacy hua zinakuepo ila ni magendo.
2. Elisa,
3. PCR.. hiki ndo kinachopima na viral load pia.
Ni kipi ni cha uhakika kuliko vyote? Au vyote vina uhakika wa majibu?
 
Back
Top Bottom