Mkuu sijui km hili swai wameshauliza
nilisumbuliwa sana na Puscells enzi zangu nikichezea timu za mitaani
na nilikuwa nikipima tu nikiona ni greater than < najua hapo nimeumia Gono , kaswende nk nabugia vidonge
sasa nipo kwenye ndoa miaka 10 na zaidi, kuna siku Wife kaenda akaandikiwa hivyohivyo kidogo nipigane
Je nilikuwa sahihi kuwa ni gonjwa la ngono km Gonoriaau ni mchafuko wa mikojo ulimtokea au ni usafi tu hakuzingatia
nisaidie ufafanuzi wa vipimi vya kuandikiwa puscel < 100 au <15 nini maana yake
mkuu najaribu kidogo ....🤓
Hapana pus cells hutolewa nje hasa unapokua na maambukizi katika njia ya mkojo (Urinary tract infections/UTI)..
Pus cells -dead white blood cells
unapopatwa na maambukizi katika njia ya mkojo ambapo bakteria huingia katika njia hii na kuleta shida huwa mwili Una detect na kuanza kupeleka Askari wa mwili (white blood cells ) .....sasa wakizidiwa huanza kuuliwa na kutolewa nje as dead white blood cells (pus cells) ....na wewe hapo huanza kujisikia homa na dalili zinginezo.
sasa mkuu hao unatakiwa ujue pia dalili za gonnorhoea (kisonono) na syphillis (kaswende) pia japo Kwa case yako nafikiri ulikua ni mchezaji peku wa mechi za mchangani (just a guess) na ndo maana pus cells zilikua hazikukosi...
Okay turudi kwenye case yako.....
wanawake ni wahanga wakubwa wa UTI sababu moja ama mbili haswa....
Kumbuka kwamba tumboni mwa binadamu upande wa njia ya haja kubwa ...kuna bakteria kibao ambao wao hapo huwa ni sehemu salama na hawana shida ....na husaidia pia kuuwa some bakteria wasio wenyeji wa eneo la hapo pindi ulapo chochote chenye shida na kazi zingine nimesahau c unajua mtaani muda mrefu mkuu....
Sasa pindi bakteria hawa wanapotoka hapo na kuhamia sehemu nyingine husababishwa shida .....na ndo hapo wanapotoka njia ya haja kubwa kwenda ndogo huleta maambukiz katika njia ya mkojo (UTI)
How?
Kwa wanawake hasa ni wakati wa kujitawadha pindi wamalizapo shughuli ya haja kubwa .....inaweza kupelekea kuwahamisha kutoka sehemu ya haja kubwa kwenda ndogo ....
why wao hasa?
moja......sababu distance Kati ya sehemu ya haja kubwa na ndogo kwao ni kama 1.5 inchi .....ni sehemu ndogo sana......wakati wanaume ni kama inch 7 kama sijakosea ko inakua ni rahisi wao....
Mbili....maumbile yalivyokaa ,, wao pamoja na umbali mfupi but also n kama kashimo while wanaume ni tofauti ko uingiaji wa vijidudu/ mabaki yenye vijidudu ni changamoto kdg....
tatu...hata vyoo vya kukaa .....wao kujisaidia kwao mara nyingi mpk wakae wakati wanaume aweza simama mbaya zaidi ukute mtu ana UTI halafu anakojoa huku amesimama ko anakojolea juu ya eneo la kukaa la Choo ....ko akija mtu ni rahisi kupata UTI hasa Kwa wanawake....
na ndo maana ukiwa upo vizur Kwa mwanaume kupata UTI kama hukuwah umwa ni asilimia ndogo sana tofauti na wanawake......labda Tu ukaiCHOVYE mahali mkuu 🤓
ko usihofu mkuu Kwa wanawake huwa inatokea Sana .....na ni vyema aumwapo ni vizur wote mkapima na kutumia dawa wote sababu mnashare naniliu ko hata wewe waweza pata pia.....na sio mmoja tu atumie itakua ni kutwanga maji Kwa kinu.
Iyo < 100 or <15 ni reporting way mkuu ambayo inaweza kumsaidia daktar kuforecast ukubwa wa tatizo na kukupa dozi inayofaa.
ni muhimu wanawake wanapojiweka Safi baada ya haja , wajisafishe Kwa "kumuvuzisha" mkono wao kutoka mbele kwenda nyuma (yaani kutoka njia ya mkojo kwenda kule kwengine) na si kutoka nyuma kuja mbele sababu atahamisha vijidudu kuja katika njia ya mkojo...
Kuwa makini pia katika matumizi ya vyoo vya kukaa hasa public toilets ....
naamini umepata mwanga kidogo ....watakuja kuweka Sawa wenyewe mkuu....