Niulize chochote kuhusu vipimo vya Maabara za Afya

Fundisanifu

JF-Expert Member
Nov 3, 2016
515
625
Shikamooni wakuu.

Mimi ni muhanga wa tatizo la ajira, na pia kabla ya hilo ni mtaalamu(mteknolojia) wa maabara(Laboratory technician) mwenye diploma ambayo nimeipata kutoka BUGANDO mwaka 2018..

Pia, katika kukaa sana mtaani nimegundua kua nina muda mwingi sana, japo baadhi hua nautumia katika kutafuta kazi.

Nimetafakari sana na kujiona mimi ni mbinafsi maana kila siku natafuta ajira kwa manufaa yangu na familia yangu.. hivyo nimeamua kwa elimu hii niliyonayo niwanufaishe na wengineo, maana hakuna msaada mwingine nnaoweza kuutoa kwenu zaidi ya elimu yangu.

Sasa naomba kutumia fursa hii, kuwapa ruksa na kuwaomba mniulize chochote kuhusiana na maabara ya afya, ku-interpret vipimo ama kutoa ushauri wa juu ya kipimo gani ufanyiwe.

Kama umeona sehemu ukakasi naweza kukusaidia katika namna ambayo nitaweza, ama kama una mashaka na majibu uliyopewa sehemu pia naweza kukuelezea vizuri kadri niwezavyo kwani kwenye kazi hii nna uzoefu wa utendaji kazi kwa miaka 2..

NB: napokea michongo ya kazi pia kupitia 0786744401,

NIULIZE, NIKUSAIDIE.
 
Swali:
Ugonjwa wa covid 19 ni ugonjwa mpya uliobuka mapema mwaka huu, je viifaa vya kupimia ugonjwa huu navyo ni vipya au ni vilevile vya zamani vinasetiwa kuweza kupima covid 19?
Msinicheke jamani
asante kwa swali lako zuri mkuu!. ugonjwa wa corona ni mpya na vifaa vyake kupimiwa pia ilibidi vitengenezwa baada ya kutokea ugonjwa hvyo naweza kusema navyo ni vipya.

Huu ugonjwa ulipotokea mwanzo walikua wanaangalia
1.dalili, lakini mapema wakajitahidi kutengeneza test kits ambazo zingewezeshwa upimwaji wa corona kwa kutumia PCR(principle inayotumika katika kupimia DNA), na vipimo vilikua very limited.

2.viashiria katika Full blood picture kuonesha kama kuna maambukizi ya virusi(viral infection), hapa nitasema ni kipimo na kifaa cha zamani.

Lakini hivi sasa imerahisishwa kwa kutengenezwa vipimo vya haraka(rapid test) ambavyo vinatoa majibu ndani ya muda mfupi, hivyo jibu la swali lako ni kua vipimo vinatengenezwa ni vipya.
 
Bro nashukuru umenipa mwanga maana mimi natamani sana kusoma medical laboratory kwa kuwa ni rahisi kujiajiri hata kama ukiwa na diploma ushauri wangu tafuta capital kidgo anza kujiajiri anzisha duka la madawa muhimu karibu na hiyo maabara uvute mpunga.
 
Je ni kipi kipimo sahihi cha Typhoid, na malaria? Maana kila nikienda kupima hata nikiwa mzima lazima nikutwe na malaria na Typhoid wakati nipo tu kawaida.
pole sana mkuu.

vipimo vya malaria kwasasa hapa Tanzania kuna

1.Mrdt(vile kama vya ukimwi unavyovionaga) hiki kinaonesha kama malaria ipo au haipo, kina efficiency ya makadirio ya asilimia 98% na serikali saivi inataka hiki ndo kiwe kipimo rasmi cha malaria.

2. Bloodslide( unayochukuliwa damu kwenye ka kioo)..hiki ni kipimo bora maana mtaalam anaona idadi ya vijidudu kwa macho kupitia hadubini(microscope) na anaweza kuvihesabu pia.

Sasa kumekua na changamoto kubwa ya wataalam kutoa majibu yasiyo sahihi hususani katika malaria kwa sababu either utendaji kazi mbovu, vifaa au wengine kwa makusudi ya kukupa ugonjwa ili uuziwe dawa(biashara) hii nmeona kwenye facility baadhi za private!.

Hivyo ukienda tena hospitali/maabara ukitaka kupima malaria anza kupima kwa mrdt kukiwa na malaria ndo utapima kipimo cha malaria bloodslide, na kuhusu typhoid kipimo the best ni kufanya "culture".. nitakuja kuelezea vizuri kuhusu vipimo vya typhoid nkikaa nimetulia.

NB:- siku hizi ni nadra sana kuumwa malaria.. ukiambiwa sehemu una malaria jiridhishe kwa vipimo vyote viwili,.
 
Back
Top Bottom