Niulize chochote kuhusu vipimo vya Maabara za Afya

Niulize chochote kuhusu vipimo vya Maabara za Afya

Kwanini ni nadra kuumwa malarial
malaria saivi kwa hapa Tanzania iko controlled, ikumbukwe sio kila mbu ana malaria.

nahisi na jitihada za watu kulalia chandarua au dawa za kuzuia mbu zinasaidia ndo maana wanaoumwa malaria saivi ni wachache compared na population iliyopo.

kuna sehemu nimewahi kufanya kazi, kupata malaria positive kwa mwezi nlikua naweza kupata kama 20 katika wagonjwa 200 au 250, japo prevalence inabadilika kulingana na misimu na majira ya joto(huongezeka).
 
Nadhani wanaoripoti kwamba malaria 1,2 nakadhalika wana base kweny mRDT sababu kile huonesha kwa mistar, so nafikiri hicho ndicho wanachomaanishaga kwamb ukiwa na Malaria 1 means mRDT Positive kwa Plas.Fascipalum na Malaria 2 kwa Mixed Infection ya Malaria parasites, ila ni mawazo yangu tuu
mkuu em nami nijaribu kidogo.

Nachofahamu ni kwamba kuna njia tatu za kuripoti malaria parasites katika blood slide..
1. kuripoti Kwa mfumo wa namba yaani (1,2,3,4) njia hii ni old method ambayo WHO walisha iondoa katika kuitumia kuripoti malaria parasites
2 . Kuripoti Kwa mfumo wa number of malaria parasites/ white blood cells either 200 or 500 wbcs depending on situation flan flan..
3 . Kuripoti Kwa mfumo wa number of malaria parasites /microlitre of blood .

Mifumo miwili ya mwisho ndo pendwa na ambayo Inapendekezwa Sana na WHO itumike kuripoti malaria parasites...

njia hii ni complex kidogo ,inachukua muda ,inahitaji staff with enough knowledge katika kuangalia na kureport majibu sahihi ya malaria na ni gharama pia sababu inahitaji uwe na reagent n.k

na ndo hapo watu wakakaa chini wakaja na njia ambayo itarahisisha diagnosis ya malaria na mgonjwa kupata matibabu haraka ....na ndo wakaleta Malaria Rapid Diagnostic Test (mrdt) ambayo yenyew ni Kwa ajili ya kuonesha Tu mgonjwa kama ana malaria ama hana ili aanze kupewa matibabu haraka ...(positive or negative)

Hii haioneshi wingi wa wadudu but just presence of malaria parasites antigen or antibody.

blood slide husaidia pia katika masuala ya utafiti (research) kufaham uwingi na Aina ya mdudu wa malaria ...pia Kwa mtu alotumia dawa ukihitaj kuangalia kama bado ana vimelea vya wadudu wa malaria ama yupo fresh within two weeks za mwanzo baada ya kutumia dawa...
 
Shukrani sana kwa majibu mazuri mkuu

Swali:
Dhana ya idadi ya vijidudu wa malaria kwenye majibu ya blood slide ikoje?... Kwa mfano.. mtu kuwa na malaria 45, 200 au 3... je ukubwa wa namba unaashiria severity ya ugonjwa?? Na nini implication ya kutaja idadi ya vijidudu ilhali dosage itatolewa vile vile??
wakuu watanirekebisha najaribu...

mkuu ukiweza kufahamu namba ya wadudu Kwa mgonjwa inaweza kumsaidia daktar kujua severity ya ugonjwa na kujua njia ya haraka ya kumsaidia mgonjwa.

namaanisha dawa anaweza pewa Kwa kuchomwa sindano ili ifike Kwa haraka sehemu husika na kumletea ahueni mgonjwa ...au mfano mtu anaumwa yupo unconscious (ana malaria Kali) ni ngumu kunywa dawa basi anachomwa sindano kwenye mshipa isafirishwe haraka kumsaidia.

au pia mtu ana homa Kali ya malaria halafu kila anachokunywa anatapika .....na inabidi kumsaidia ko atachomwa sindano ya dawa instead ya kumeza.

Kwa mtu ambae anaweza kunywa na hali yake anaweza kuhimili anaweza tu tumia vidonge vya kunywa ...

Hii ni baada ya daktar kutazama Hali ya mgonjwa ndo atafanya maamuzi pia Kwa kuona majibu yake yalivyo.
 
mkuu em nami nijaribu kidogo.

Nachofahamu ni kwamba kuna njia tatu za kuripoti malaria parasites katika blood slide..
Sawa mkuu!
Screenshot_20201202-141501.jpg
images (1).jpg

Ila mRDT inaweza kukupa majibu kwamba ni one parasite infection au mixed infection, nadhani hapo ndo majibu ya malaria moja na mbili inaanzia.

Kwa mfano picha nilotuma hapo juu inaonesha mtu ana mixed infection ya falciparum na wengine
 
malaria moja na mbili inaanzia.
mkuu nimekuelewa hapo penye either single or mixed infection.

ila ukitumia neno "malaria moja na mbili" Kwa standard reporting za malaria kutoka WHO unaweza maanisha kitu tofauti kama nilivyoelezea hapo juu.

So ni vizuri ukaripoti positive or negative na kama kuna mixed infection report it. ila ukitumia neno malaria moja na mbili unaweza mconfuse mtu sababu MRDT inatumika for qualitification and not quantification of malaria parasites.

japo nachoona watu washazoea hivyo na sio Kwa kufata standard way of reporting ...na ndo wanapowachanganya watu.

na inatokana na wataalamu kutokua updated na pengine kufanya kazi Kwa mazoea.
 
mkuu nimekuelewa hapo penye either single or mixed infection...
Nashukuru umeelewa!

Maana kuna watu wanakataa tu bila kujua mantki ya suala lenyewe.

Vijijin huku watu wakiambiwa wana malaria 2 wanajua huyu mgonjwa anaweza kua na hali mbya tofauti na 1 ingawa ki- professionalism yoyote kat ya mwenye 1 au 2 anaweza pata severe form ya Malaria.

So kiujumla wataalam wa maabara wanatumia maneno mepesi kuwaeleza watu hasa wenye elim ndog kuelewa majibu yao ya vipimo.

Ahsante
 
huwa maabara mkipima ukimwi mnatumia kipimo gani? nimesikia mahali mnatumia kama hivi hivi tunavyouziwa wananchi tuji pime wenyewe? kuna ukweli ktk hilo
Mkuu hivi hivyo vipimo vya Ukimwi Pharmacy huwa wanauzaje?
 
wote wako sahihi mkuu, vyovyote vile ila cha msingi mbegu zipatikane...
Ni katika zoezi la uchomaji sindano hasa makalioni, nilikuwa nikisikia manesi wakisema usikaze makalio itakatikia ndani, ni yapi madhara yanayoweza jitokeza ikitokea hali hiyo. (Inaweza likawa swali la nje ya mada, kama una idea nalo nisaidie kufahamu)
 
mkuu naomba nikukosoe hapo sio "dhana" bali ni technique ya kureport majibu....

Mara nyingi nimekuwa nikiaminishwa na baadhi ya wataalamu wa afya kuwa kadri namba ya vijidudu vya malaria inapokuwa ndogo katika WBC ndivyo mgonjwa anavyotingwa zaidi (Hali mbaya) na kuchukua muda mrefu katika kuiondoa/kuitibu. Je, kuna ukweli wowote?
 
Shikamooni wakuu.

Mimi ni muhanga wa tatizo la ajira, na pia kabla ya hilo ni mtaalamu(mteknolojia) wa maabara(Laboratory technician) mwenye diploma ambayo nimeipata kutoka BUGANDO mwaka 2018...
Pep inafanya kazi kwa mtu aliyekuwa exposed na hiv kwa muda gan
 
Oya we jamaa ondoka dar watu wanaoishi interior wanakuhitaji wasomi mnakosea sana yani kujazana dar ety kutafuta kazi nakati huku interior kuna matatizo chungu nzima
 
Katika kupima U.T.I kuna sampuli ambayo inayoweza kupimwa tofauti na mkojo? Na vipi ukubwa wa ugonjwa huu mfano Ukiwa sugu vipimo vyake vinasomekaje mfano unakuta unaambiwa una U.T.I ipo 55
 
Katika kupima U.T.I kuna sampuli ambayo inayoweza kupimwa tofauti na mkojo? Na vipi ukubwa wa ugonjwa huu mfano Ukiwa sugu vipimo vyake vinasomekaje mfano unakuta unaambiwa una U.T.I ipo 55
mkuu najaribu kidogo ,wenyewe watakuja kujibu Kwa ufasaha.

U.T.I ni kifupi cha urinary tract infections yaani maambukizi katika njia ya mkojo.

maambukizi haya mara nyingi husababishwa na bakteria ambao huvamia eneo la haja ndogo na kuleta maambukizi mahala hapo.

mara nyingi hawa bakteria hutoka katika njia ya haja kubwa ambapo huko hawana madhara ila wakija kwenye njia ya haja ndogo huleta madhara.

sampuli navyofaham ni mkojo tu.

Standard inaelekeza kwamba ili kupata majibu ya uhakika ya mtu mwenye U.T.I ni vizuri kufanya test inaitwa "urine culture"

mkojo unapandwa kwenye special prepared media ambazo zina content maalum zinazowezesha wadudu kuota baada ya kuwekwa kwenye mazingira Sawa na mwilini mwa binadamu ....at 37 degree centigrade kwenye incubator Kwa masaa 24.

Baada ya hapo wadudu huota. Kwa sampuli ambayo ina U.T.I na ambayo haina wadudu hawatoota.

Baada ya hapo hufanyiwa antimicrobial susceptibility testing Kwa maana unatest ni dawa zipi ambazo zitakua zinamtibu ama zimekua sugu Kwa mdudu huyo. Kwa hiyo kupitia kipimo hicho unaweza pata Aina ya mdudu na dawa ipi ni nzuri inaua mdudu na ipi imekua sugu.

Ila kutokana na uhaba wa vifaa na gharama ya vifaa, mahitaji ya watu ambao ni Wana ujuzi wa kutosha ...kipimo hiki unaweza kipata kwenye maabara kubwa na hospitali za mikoa ,rufaa hasa.

sasa huku chini ambako huwez kufanya kipimo hiki , kinachofanyika ni kupima namba ya WBCs tu zinazoonekana kwenye mkojo (pus cells-died WBCs) na kuangalia urine presence of nitrites.

inaaminika kwamba ... Bakteria hawa wakivamia sehemu ya haja ndogo huanza kuzaliana 😊 na kuongezeka in number kufikia namba ambayo wanaanza kusababisha shida na wewe kuanza kusikia homa, na dalili zinginezo ambapo hapo unakua umepata maambukizi katika njia ya mkojo.

kwann tunapima WBCs? sababu hawa ndo walinzi wa mwili hivyo kunapokua na shida huanza kupambana ...na wakishindwa huuliwa na kuanza kutolewa kwenye mkojo na ww huanza kujisikia homa Kwa case hii ya mtu mwenye maambukizi katika njia ya mkojo.

Kwa hiyo kinachopimwa ni died WBCs ambazo kadiri zinapokua nyingi "huenda" ukawa umeathirika pakubwa na hao bakteria.

Njia hii haiwezi kukuonesha ni dawa zipi zimekua sugu na haioneshi idadi ya wadudu. japo ni ya gharama nafuu na haichukui muda na ndo wengi huitumia kulingana pia na uchumi wetu wa kitanzania.

naamini umepata kidogo picha ...wajuzi watakuja kunirekebisha.
 
Pep inafanya kazi kwa mtu aliyekuwa exposed na hiv kwa muda gan

Pep inafanya kazi kwa mtu aliyekuwa exposed na hiv kwa muda gan
unatakiwa kuanza PEP within 72 hours toka ulipokua exposed. sababu muda huu hiv anakua kwenye extracellular fluid bado kuingia ndan ya cell kupitia receptors ambazo zipo on surface ya cell.

watakuja kunirekebisha wajuzi.
 
hapana si illegal,iweje vya mimba viwe legal hv vingine viwe illegal? ukipata muda wewe kajinunulie zako
Acha kumdanganya mwenzako.
Haviuzwi kwa raia na Vyote vimeandikwa ni Mali ya jamhuri haviuzwi.

Sheria inayoruhusu raia kujipima wenyewe ilipitishwa na bunge lililopita lakini nafikir imekwama ktk kuweka kanuni na sera za Utekelezaji.
Usifananishe HIV na Mimba.
 
mkuu em nami nijaribu kidogo.

Nachofahamu ni kwamba kuna njia tatu za kuripoti malaria parasites katika blood slide...
naam uko sahihi mkuu, na asante kwa kunisaidia kumjibu kwa ufasaha na maelezo mazuri.

hiyo njia ya kwanza uliyosema ilikua wanaripoti kwa 1,2,3,4 nadhani ulimaanisha "QBC malaria"
hiyo ya 2 yes ndo inayotumika sana, yaan malaria against white blood cells na hyo ya 3 ni against red bloodcells,

nmefanya kazi sehemu wanatumia hyo ya 2, na pia mwaka huu nmefanta kazi sehemu inatumika hyo ya 3. .

hyo ya kwanza sijawahi kuitumia siwezi kuficha hilo maana hata kwenye mtaala wetu imeondolewa nadhani..
 
Back
Top Bottom