Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
10,515
Reaction score
17,439
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
View attachment 2149098
Mkuu naomba unisaidie.
Hapo kuna vifaa gani na gani?
Na kama mtu unataman kua na system ya dizain hiyo ni kipi inabidi kiwe cha kwanza kununua?
Natanguliza shukrani

Hapo kuna
1 amplifier
2 equlizer
3 speaker
4 laptop

Kuhusu nin kiwe chakwanza inategemeana
Ila waweza anza amplifiers
Na amplifiers zinatofautiana watts
Sawa na kusema zinatofautiana uwezo wake
Kwahyo kama unataka sounds kama hiyo basi tafuta amplifiers kama hiyo hiyo
Au utengenezewe kama hiyo au yenye sett up kama hiyo
Baadae utakuja tafuta speaker zake
Na sio kwakua basi unanunua tu spika hapana
Nazo zina mahesab yake
Kiasi kua hata mmiliki wa hiyo sound akitoka nje ya hesabu ya hiyo amplifier ataiharibu yrnyewe au hizo speaker
Kwahyo ni sawa na kusema tafuta amplifiers itakayoendana na speaker
Au tafuta speaker itakayoendana na hiyo amplifiers
3 equlizer ni equlizer tu
Zinatofautiana band na freqnc kidogo sana
Ni vyema kupata yenye bands nyingi ili ikupe option ya ku equalize sound vyema
Lakini kumbuka kua lazima iwe ya channel mbili
Yaan L na R
4 naona hapa pc inatumik kam signal output
Ingawa hiyo amp pekee inaweza kua na Bluetooth ikafanya kaz bila pc au vyote kwapamoja


Ni hayo tu
 
Mkuu hii inakuwa ni active subwoofer kwa maana unatengenezea na amplifier yake kabisa ndani?.

Complete ni bei gani ikiwa imekamilika?

IMG_6775.jpg

Sorry sijaifunik sababu mfuniko sijatengenezea


Iyo ndio amplifier yake
Ile speaker ipo kwenye box yake tu
Na kuna zingine jumla zipo speaker 5
Ila mashine ndio hiyo hiyo
 
View attachment 2149098
Mkuu naomba unisaidie.
Hapo kuna vifaa gani na gani?
Na kama mtu unataman kua na system ya dizain hiyo ni kipi inabidi kiwe cha kwanza kununua?
Natanguliza shukrani
anza na speaker, ujue unataka zenye uwezo gani, maan kupata tower speaker za kiwango bongo bado sana, kisha amplifier inayoweza kusukuma speaker zako
 
View attachment 2149271
Hizi za pioneer mim nlinunua 2 kwa 80000 sas inategemeana pia
Wakati mwingine waweza pata kwa bei ya chin au kubwa zaid
Mkuu, embu nielezee ubora wa hivi vi mp3 vinavyofungwa kwenye radio za zamani. Ni vya kichina, kina usb port na Bluetooth, ufanyaje wake wa kazi ukoje haswa kwenye ubora wa sound reproduction?
 
Mkuu, embu nielezee ubora wa hivi vi mp3 vinavyofungwa kwenye radio za zamani. Ni vya kichina, kina usb port na Bluetooth, ufanyaje wake wa kazi ukoje haswa kwenye ubora wa sound reproduction?
Mp3 modulator haitengenezi sauti. Sauti itabaki Ile ile ya redio yako. Labda kama utapata modulator yenye equalizer
 
Mkuu, embu nielezee ubora wa hivi vi mp3 vinavyofungwa kwenye radio za zamani. Ni vya kichina, kina usb port na Bluetooth, ufanyaje wake wa kazi ukoje haswa kwenye ubora wa sound reproduction?

Kwenye ubora vinatofatiana mkuu
Na pengine inahitaji utulivu kufahamu
IMG_6355.jpg

Kuna zile za kwanza zilikua pow sana sana sana
Zikaja za pili hizi hazitoi stereo zinapiga mono
Hivyo huwezi kupata surround nzuri ya mziki
Namna ya kukijua n hadi uwe fundi
Pale kwenye output utakuta waleweka resistor ime link signal zote mbili
Kuhusu sound ni nzuri ikiwa utakipata kinachopiga stereo
 
Hivi nitajuaje kama speaker inapiga vizur bila kuisikiliza?
I mean kuna specifications zozote zinazoonesha kwamba hii speaker itakua inapiga vizur?

Speaker sio rangi yake au vyovyote vile
Kila speaker n nzuri kwenye eneo lake
Hivyo inategemeana sana unaitumia wapi?
Kama ni tweeters zinatofautiana
Kans ni midbass zinatofautiana
Na bass pia

Bass nzuri hua na sumaku kubwa...na mpira mnene pemben na spider ngumu
Hi kwa unumla itakupa bass nzito
Nyingine inawezekana kua ya bass ila ikawa nyepesi
Ukiwa unaitazama spik upande wa mbele(huku kwenye karatasi) ukiwa unaisukuma kwenda ndani au kwenda kwenye sumaku nyuma inapokua ngum sana it means inakua most powerful coz it need more power kui push ili upate kiki,kuliko ile nyepesi
Kwahyo hatuwez kusema kuna moja nzuri au mbaya ila kila moja nzuri kwenye eneo lake
Pia kuna kitu kinaitwa watts na ohms kwenye speaker je unafahamu?
 
Speaker sio rangi yake au vyovyote vile
Kila speaker n nzuri kwenye eneo lake
Hivyo inategemeana sana unaitumia wapi?
Kama ni tweeters zinatofautiana
Kans ni midbass zinatofautiana
Na bass pia

Bass nzuri hua na sumaku kubwa...na mpira mnene pemben na spider ngumu
Hi kwa unumla itakupa bass nzito
Nyingine inawezekana kua ya bass ila ikawa nyepesi
Ukiwa unaitazama spik upande wa mbele(huku kwenye karatasi) ukiwa unaisukuma kwenda ndani au kwenda kwenye sumaku nyuma inapokua ngum sana it means inakua most powerful coz it need more power kui push ili upate kiki,kuliko ile nyepesi
Kwahyo hatuwez kusema kuna moja nzuri au mbaya ila kila moja nzuri kwenye eneo lake
Pia kuna kitu kinaitwa watts na ohms kwenye speaker je unafahamu?
Yaah
Naziskia saana
Kwa navofahamu watts ndo zinapima nguvu ya mziki utaotoka..
Ohms nishasahau..
 
Back
Top Bottom