Denti mmoja msichana mapepe wa chuo aliingia ofisini kwa Profesa akiwa kavalia kiuchokozi chokozi.
Mazungumzo yalikuwa hivi:
Denti: Mambo Profe?
Profesa: (Hakujibu bali aliuliza) Unasemaje?
Denti: Nimekuja na "proporsal" yangu.
Profesa: Iweke juu ya meza nitaiangalia baadae.
Denti: Hapana sio hivyo, ni mipango tu baina ya mimi na wewe; si unajua tena?
Profesa: Sema, unasemaje?
Denti: Niambie unataka nini nifanye nini ili nifaulu mtihani wako wa kesho? We sema tu, ninaweza kufanya chochote.
Profesa: Kweli? Unaweza kufanya chochote nitachokuambia?
Denti: Ndio Profe, chochote, we sema tu mi niko tayari.
Profesa: Kama ni hivyo sawa, rudi nyumbani kasome mada zote 12 tuliyosoma katika semesta mbili.
Ni wachache sana. Hivi ndivyo tunatakwa tuwe, hasa tukitilia maanani kuwa "Profesa, au mwalimu" atakuwa na umri sawa na mzazi au angalau kama kaka wa wanafunzi wao. Badala ya kuzidi kuwapoteza na kuwapa imani kuwa elimu hupatikana "kirahisi rahisi", njia bora ni kuwaelekeza kwenye ukweli wa mambo.very few can do that
Denti mmoja msichana mapepe wa chuo aliingia ofisini kwa Profesa akiwa kavalia kiuchokozi chokozi.
Mazungumzo yalikuwa hivi:
Denti: Mambo Profe?
Profesa: (Hakujibu bali aliuliza) Unasemaje?
Denti: Nimekuja na "proporsal" yangu.
Profesa: Iweke juu ya meza nitaiangalia baadae.
Denti: Hapana sio hivyo, ni mipango tu baina ya mimi na wewe; si unajua tena?
Profesa: Sema, unasemaje?
Denti: Niambie unataka nifanye nini ili nifaulu mtihani wako wa kesho? We sema tu, ninaweza kufanya chochote.
Profesa: Kweli? Unaweza kufanya chochote nitachokuambia?
Denti: Ndio Profe, chochote, we sema tu mi niko tayari.
Profesa: Kama ni hivyo sawa, weka proposal yako mezani, kama inalipa utapasi!