Nitawezaje kujaza wino kwenye Printer ya EPSON L210?

Nitawezaje kujaza wino kwenye Printer ya EPSON L210?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
12,151
Reaction score
44,121
Natumia Printer ya EPSON L210 yenye kutumia wino wa maji wa kujaza kwenye matanki(Liquid ink refilling tank), kwa kuwa nilinunua ikiwa mpya kabisa ilikuja na package ya chupa za 4 za rangi tofautitofauti za wino original wa EPSON nikajaza na nikatumia vizuri.

Kwa sasa wino wa chupa moja unakaribia kwisha kwenye mtungi mmoja, nimepata wino mwingine but sio original EPSON, sasa nauliza naweza jaza hivyo hivyo au ni lazima nifanye software setting?

Je printer ya EPSON L210 inaweza kukubali wino ambao sio original?
 
Natumia Printer ya EPSON L210 yenye kutumia wino wa maji wa kujaza kwenye matanki(Liquid ink refilling tank), kwa kuwa nilinunua ikiwa mpya kabisa ilikuja na package ya chupa 4 za rangi tofautitofauti za wino original wa EPSON nikajaza na nikatumia vizuri.

Kwa sasa wino wa chupa moja unakaribia kwisha kwenye mtungi mmoja, nimepata wino mwingine but sio original EPSON, sasa nauliza naweza jaza hivyo hivyo au ni lazima nifanye software setting mpya tofauti na EPSON ili viendane(kuna mtu aliniambia although hakuniambia namna ya kufanya)?
Je printer ya EPSON L210 inaweza kukubali wino ambao sio original?
 
Nauliza naweza jaza hivyo hivyo.
  • Ndio jaza hakikisha ni wino ambao ni sahihi kwa epson
Au ni lazima nifanye software setting?
  • Hakuna software setting yeyote ya kufanya, ni kuweka wino na kuendelea kutumia.
Je printer ya EPSON L210 inaweza kukubali wino ambao sio original?
  • Ndio inawezekana tafuta huu ulioandikwa CLARITY
Zanzibar-ASP
 
Last edited by a moderator:
tafuta wino wa epson origino

Mkuu hapo hujanijibu wala hujanisaidia. Kukujibu tu, Original wino wa EPSON huwa unakuja na Printer yenyewe, tofauti na hapo ni kubahatisha tu, na ndipo nilipo kwa sasa. Je, unataka ninue tena Printer mpya ya EPSON?
 
Epson ina tabia ya matokeo usiyoyatarajia kwa kutumia wino fake, kama una haja ya kununua CSI nyingine kwa karibu 200,000/- weka fake. Nenda pale mtaa wa Agrey kariakoo wino wa Epson umejaa kibao kichupa 5,000/- tu!!
 
Back
Top Bottom