Nitawasilisha hoja tatu kwa chama changu CHADEMA

Nitawasilisha hoja tatu kwa chama changu CHADEMA

Mkuu unaamini Shivji anaweza kuwa mfano halisi na hitimisho la hoja ya tatu????
hizo jamii hasa wahindi wanapewa fursa sawa na watanzania wengine maadam tu ni Mtanzania. hata waziri wa Fedha wa Kwanza wa nchi Mhe. Jamal alikuwa Mtanzania mwenye asili ya kihindi. Ukienda Hospitali zote kubwa za Serikali huwezi kuwakosa madaktari wenye asili ya India yaani wahindi na wamekuwa wakitoa huduma. hadi katika Halmashauri zetu tunao. hapo kwa waarabu ndo pana Mushkeli kwenye utumishi wa umma maana hata wao wenyewe sidhani kama wanahitaji hilo. Ila kwenye Nchi hii haijawahi kuwabagua Wahindi, waarabu na Wengineo. Akina Rostam, Manji, Bakhlesa n.k nadhani unawaona.

Suala la Uraia pacha ina mashiko na ni suala la muhimu kwa kweli ingawa ki usalama inaweza isiwe nzuri sana.
 
Kama Nyerere asingefanya hicho unachojaribu kushauri leo wa Tz wangemjulia wapi Prof. Issa Shivj?
kwa kuongezea..Amir Jamal na Alnoor Kassum walipata kuwa mawaziri nyeti
Bungeni wapo wahindi,ni wao wenyewe tu hawataki kujiingiza huku lakini katiba haizuii
Naibu katibu mkuu mambo ya nje ni mwarabu kabisa
 
Huko India kuna mwafrika mwenye uraia wa India? Huku Tanzania ninazungumzia raia wa asili ya asia ambao ni raia halisi wa Tanzania, sio wageni
Wahindi,waarabu ni kabila kama walivyo wachaga,wanyamwezi nk Tanzania haiajiri mtu Kwa kabila,rangi au dini.Yeriko unapigania ukabila !!!! Ni aibu hata kuwaita watanzania wenye asili ya kihindi au kiarabu ni kuwanyanyapaa.Mbona mmakonde Haitwi mmakonde mwenye asili ya msumbiji au mjaluo haitwi mtanzania mjaluo mwenye asili ya kenya au mgogo haitwi mgogo mwenye asili ya Tanzania? Ajira haziendi Kwa ukabila au rangi au dini mkabila mkubwa wewe.
 
Wahindi na waarabu tumesoma nao kuanzia chekechea mpaka vyuo vikuu, na mchango wao sio mdogo.

Mtu kama Alnoor Kassum, alitoa mchango mkubwa katika awamu ya kwanza. Na wapo wengi tu wa aina yake.

Uraia pacha - kwa bahati mbaya imejengeka dhana kwamba upo uwezekano wa adui wa nje kuihujumu nchi hii kwa kujificha kwenye uraia wa aina hii. Ingawa nahisi kuwa tunapoteza uwezo na vipaji vya watanzania wenzetu ambao mmoja wa wazazi wao ni mtu wa bara jingine.

CHADEMA kabla ya kuifikiria ikulu kwanza ijitazame yenyewe. Huwezi ukataka kuongoza nchi wakati ndani ya chama chako kuna kiongozi ambaye ana miaka 14 madarakani na haijulikani ni lini atawaachia wenzake kijiti cha uongozi.

CHADEMA ijitathmini kwa kina. Huwezi kuongelea udikteta wa serikali iliyopo ikulu wakati kwenye chama chako kuna sura ile ile unayoinyoshea kidole.
Nakushukuru kwa maoni yako yenye kuunga mkono hoja zangu,

Juu ya Chadema na uongozi wake hiyo ndio demokrasia ya chama chetu, demokrasia ni namna watu wenhi wanavyoamua jambo/mambo yao... Katiba inaruhusu mtu kugombea kila muhula unavyoisha, hivyo ndivyo Chadema inavyofanya, kila mhula huwa kuna uchaguzi, na haki ya kikatiba inamruhusu Mbowe kugombea na waliowengi wanamchagua kuwa kiongozi, je unataka tukinzane na demokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa inayosema wengi waamue na wachache wasikilizwe?
 
Ndio maanua hamuwrzi shika dola. Yaani muhindi au mwarabu awe waziri mkuu? Awe rais? Kule kwao hata muhindi mwenye ngozi nyeusi bado hawamtaki.
Mpeni muhibdi uenyekiti wa chama chenu kwanza.
Una roho ya kibaguzi sana ndugu, soma katiba, inasema kila raia wa Tanzania ana haki zote katika nchi, je Wahindi hawa na Waarabu sio raia wa Tanzania?
 
Yericko Yericko !!!!
Dhana ya tatu hujaitendea haki kabisa.

Unaizungumzia kama vile hilo jina lako la mwisho umechovya yaani J.K. Nyerere hukumfuatilia au hukumuelewa kabisa hasa pale alipowapa uongozi sehemu mbalimbali hata zile sehemu au idara nyeti jamii ya hao watu uliowataja.

Hujamuelewa Nyerere mwenzio hata pale alipotoa tafsiri ya makaburu na wabaguzi.

Kama Nyerere asingefanya hicho unachojaribu kushauri leo wa Tz wangemjulia wapi Prof. Issa Shivj?

Daah nimesikitika sana jinsi ulivyo shindwa kutambua nchi yetu ilivyo wapa fursa watu wa jamii ulizozisema hasa kipindi cha Nyerere na Mwinyi muondoe huyu wa sasa ambae sio mwanasiasa au mwana diplomasia au sio mwanafalsafa kama viongozi wa awamu ya kwanza na ya pili.
Siyo rahisi kumuelewa Yericko kwenye dhana hii y'a tatu mpaka uwe unajua mambo yahusuyo uchumi.
 
hizo jamii hasa wahindi wanapewa fursa sawa na watanzania wengine maadam tu ni Mtanzania. hata waziri wa Fedha wa Kwanza wa nchi Mhe. Jamal alikuwa Mtanzania mwenye asili ya kihindi. Ukienda Hospitali zote kubwa za Serikali huwezi kuwakosa madaktari wenye asili ya India yaani wahindi na wamekuwa wakitoa huduma. hadi katika Halmashauri zetu tunao. hapo kwa waarabu ndo pana Mushkeli kwenye utumishi wa umma maana hata wao wenyewe sidhani kama wanahitaji hilo. Ila kwenye Nchi hii haijawahi kuwabagua Wahindi, waarabu na Wengineo. Akina Rostam, Manji, Bakhlesa n.k nadhani unawaona.

Suala la Uraia pacha ina mashiko na ni suala la muhimu kwa kweli ingawa ki usalama inaweza isiwe nzuri sana.
Hakuna sababu yoyote ya kiusalama inaweza kuwa justification ya jambo hili la Uraia wa nchi mbili, Watanzania waelewe, msingi wa jambo hili ulitumika kwakuwa baada ya Uhuru nchi yetu ilikuwa sio mwanachama wa ulinzi na usalama wa kimataifa yaani Interpol, ambayo ni polisi ya kimataifa, leo ni wanachama, hivyo hoja ya usalama kwamba wahujumu uchumi watakimbilia nchi nyingine wakishaiba ni DHAIFU na inadhihirisha ujinga na ubaguzi tulio nao kama taifa. Unaweza kujiuliza sababu za kujiunga Inter
pol ni nini ikiwa tunashindwa mambo madogo kama haya ya kudhibiti watu wetu tunaodhani watakimbilia nchi nyingine wakifanya makosa huku.

Ukweli unasimama kuwa makosa mengi yanayowakimbiza watanzania wanaoitwa wahalifu nchini ni makosa yanayotokana na sheria za kisiasa zinapingwa na jumuiya ya kimataifa kama vile sheria ya uhuru wa Habari, Sheria ya Mitandao, sheria ya vyombo vya habari na sheria ya uchochezi ambazo nyingi yazo ni sheria za kikoloni ambazo ulimwengu unazipinga...hivyo mtu aliyetenda kosa la uchochezi kwa sheria ya Tanzania, kosa hilo kwa sheria ya Marekani sio kosa na hatakamatwa na Interpol ikiwa Serikali ya Tanzania itamhitaji ili kufunguliwa kesi...
 
Kipindi cha kujiandikisha vitambulisho vya uraia nilipita kariakoo niliwakuta Wahindi wengi tuu wanajiandikisha.
Tatizo hawa watu hata ukiwakumbatia vipi wengi wao wana mentality yao hapa si kwao India na Canada. Unakuta mtoto anazaliwa upanga Kiswahili hajui. Halafu uanze kumkingia kifua cha uraia pacha. Mbona wengine wanabrend in tunaish nao....To hell with Indians....
 
Nakushukuru kwa maoni yako yenye kuunga mkono hoja zangu,

Juu ya Chadema na uongozi wake hiyo ndio demokrasia ya chama chetu, demokrasia ni namna watu wenhi wanavyoamua jambo/mambo yao... Katiba inaruhusu mtu kugombea kila muhula unavyoisha, hivyo ndivyo Chadema inavyofanya, kila mhula huwa kuna uchaguzi, na haki ya kikatiba inamruhusu Mbowe kugombea na waliowengi wanamchagua kuwa kiongozi, je unataka tukinzane na demokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa inayosema wengi waamue na wachache wasikilizwe?
Miaka yote mshindi anakuwa huyo huyo mmoja tu. Huo ni udhaifu ambao hamuuoni, pengine ni kikwazo cha kukua kwa chama chenu.

Mnahitaji mawazo mapya, watu wapya ili muweze kuwa na mikakati mipya ambayo inaweza kukupatieni ushindi wa kitaifa. Mnatumia silaha zile zile kupambana na adui anayeelewa maana ya mabadiliko ya ndani ya chama, ni vigumu sana kufanikiwa.
 
Yericko Yericko !!!!
Dhana ya tatu hujaitendea haki kabisa.

Unaizungumzia kama vile hilo jina lako la mwisho umechovya yaani J.K. Nyerere hukumfuatilia au hukumuelewa kabisa hasa pale alipowapa uongozi sehemu mbalimbali hata zile sehemu au idara nyeti jamii ya hao watu uliowataja.

Hujamuelewa Nyerere mwenzio hata pale alipotoa tafsiri ya makaburu na wabaguzi.

Kama Nyerere asingefanya hicho unachojaribu kushauri leo wa Tz wangemjulia wapi Prof. Issa Shivj?

Daah nimesikitika sana jinsi ulivyo shindwa kutambua nchi yetu ilivyo wapa fursa watu wa jamii ulizozisema hasa kipindi cha Nyerere na Mwinyi muondoe huyu wa sasa ambae sio mwanasiasa au mwana diplomasia au sio mwanafalsafa kama viongozi wa awamu ya kwanza na ya pili.

Nadhani hujamwelewa. Yericko anataka kupanua wigo. Ukiangalia Idadi ya Jamii anayorejelea Yericko na kutembetembea kidogo ofisi za Umma/utumishi huoni na pengine hupati kabisa mrejesho wa maana. Kwa mantiki hiyo inapokuwa sera jambo hupata msukumo wa aina yake.
 
Huko India kuna mwafrika mwenye uraia wa India? Huku Tanzania ninazungumzia raia wa asili ya asia ambao ni raia halisi wa Tanzania, sio wageni
Acha kujipendekeza wewe ... umepata demu wa kihindi nini ? hayo mahaba yako bakia nayo mwenyewe usitake kutuletea ukoloni hapa.
 
Wanabaguliwa kwasababu ya uraia wao au rangi yao? Ikiwa kuna ubaguzi huo nasi tuwaige wao?
Dawa ya moto ni moto nakuambia tena acha kujipendekeza wewe kwa rangi rangi ni vyele tambi .. miafrika bhana kweli ndivo tulivo babu zako walionyeshwa vioo wakatoa almas wewe ushaonyeshwa sijui nini unatuletea uchuro hapa.
 
Back
Top Bottom