Nitawasilisha hoja tatu kwa chama changu CHADEMA

Nikiwa kama mwanachama hai wa chama kinachojiandaa kushika madaraka nchini, na nikiwa mmoja ya Watanzania wanaolitazama taifa hili kama lulu ya ulimwengu, nikiwa na akili timamu, nitawasilisha hoja zangu tatu kwa chama changu Chadema ziwe agenda muhimu katika uchaguzi 2O2O.
Agenda hizo ni:

1. Mabadiliko ya mfumo wa ulinzi na usalama.

2. Uraia Pacha

3. Jamii za Wahindi na Waarabu wa Tanzania zitambuliwe rasmi na zishiriki shughuli zozote za utumishi wa nchi katika maeneo yote nyeti ya nchi.

Hoja ya kwanza nimeitafiti na kujiridhisha kwamba maendeleo ya taifa kwa vina vyote katika mlinganyo wa ulimwengu, mfumo wa vyombo hivi kwa sasa ni kikwazo kikubwa sana kufikia malengo.

Hoja ya 2. Nimejiridhisha kuwa taifa linakosa fursa na nyingi na hasa utaalamu na mitaji ya watanzania wenye uraia wa nchi nyingine kwasababu ambazo zimepitwa na wakati kwaulimwengu wa leo, Izingatiwe kuwa sababu kuu ya kuweka zuio la Watanzania walioghaibuni waliopata uraia wa nchi nyingine huko zilikuwa ni usalama hasa baada ya uhuru na kwenye harakati za ukombozi kusini mwa jangwa la sahara na katika kipindi cha Uhujumu Uchumi chini ya akina Sokoine. Sababu hizo na nyingi leo hazina mashiko....

Hoja ya tatu ni kuwa jamii hizi za wahindi na waarabu ambao ni watanzania halisi na tena kimsingi hazina uraia wa nchi zingi bali Tanzania tu, ndizo zinazochangia pato la taifa kwa ujumla kupitia mitaji yao ya uwekezaji nchini, ni jamii zilizo na wataalamu wa fani mbalimbali kama madaktari, wahandisi, na wachumi ambao leo wangeingia kwenye mifumo ya kiutumishi wa nchi kwa nyanja zote wataleta mafaa kwa taifa kuliko kukumbatia kasumba ambazo nadharia yake ni ubaguzi tu kwa raia nchini.

Ziko sababu nyingi sana za kutetea hoja zangu hizi, nitawasilisha hoja na utetezi wake naamini chama changu kitanielewa na kuzipokea hoja hizi kuwa sehemu ya agenda uchaguzi ujayo, na hazuwi agenda tu za maneno ili kujipatia ufuasi tu kama wale wenzetu 2OO5 walikuja na agenda ya OIC walipewa madaraka wakawatelekeza waliowaahidi.

Kisha 2O1O wakaja na utapeli mwingine wa Mahakama ya Kadhi, hawakutekeleza hadi 2O15, wakaja na utapeli mwingine kwamba watagawa milioni hamsini kila kijiji na watagawa laptop kila mwanafunzi wa Tanzania, matokeo yake kila mwanafunzi nchini anabeba dumu la maji na mfagio wa chelewa...

Chadema kama chama imara nchini usanii kwetu mwiko, tunaahidi unaloweza kutekeleza...!

Ili uelewe zaidi faida na hasara ya hoja hizi, soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.

Na Yericko Nyerere
View attachment 819746
Yeriko hoja ya Kwanza Sina shida nayo maana inaongelea ulinzi!! Ikimaanisha unataka raia walindwe pamoja na ulinzi wa nchi! Ila Sasa hoja ya pili kama ndo utaitumia nadhani Uta fail angalia wana nchi wa Hali ya chini wanauhitaji wa hizo mambo za urahia mbili! Au zitawasaidia n9? Labda useme kuwa unatakiwa uwepo ila uwe strict saana! Usigawiwe kiholela!
Hoja yako ya mwisho nayo siipingi ila naomba unipe takwimu za Hao watu wanaoingiza pato LA taifa na hawana uraia wa Tanzania ila wamezaliwa tanzania
 
Sheria ya ardhi iko vizuri, serikali ni mdhamini mkuu wa ardhi hiyo, raia wa Tanzania hukodishwa tu kwa mkataba wa miaka 33, 66 na 99. Hili sioni kama linatatizo mkuu[/QUOTE
Okay sasa kama ardhi hukodishwa kwa mtu kwa kipindi hicho tumewaandaaje watu maskini kupata huo umiliki? na kama swala la uraia pacha kwa foreighners ambao tuna amini kiuchumi wako vizuri huoni kama wao ndio watahodhi ardhi kwa asilimia kubwa na mzawa akabaki kuwa mpangaji kama jirani zetu Kenya?
 
Kamundu,

..diaspora mngeomba kuwa na status maalum ya ukaazi[kitu kama green card] badala ya uraia pacha.

..uraia pacha unatutisha sana waTz na tayari umeshapewa jina baya. it will be such an uphill batttle kubadilisha mtizamo wetu kuhusu suala hilo.
Hivi mnafikiri mpaka sasa nani hasa ana loose kwenye hili. Wanao loose sio diaspora ni Tanzania kama nchi kwenye hili. Ni sawasawa na mtoto kusema haendi shule mpaka mzazi aombe msamaha.... na kufikiri mzazi ndiye anaye loose kwasababu yeye ndiye anakazania aende shule. Watanzania kwenye hili tumekuwa kama watoto wanaogoma kwenye shule. Ukifikiria vizuri mtu kama mimi nime cost nini au nita cost nini Tanzania nitaiba nini wakati kila siku naombwa nitume pesa za hichi na kile. Nchi yetu inahitaji wazawa hao Wachina mnaofikiri watawasaidia watawafanya watumwa siku moja. Ubinafsi wa Watanzania tunauleta Watanzania wenyewe. Nakumbuka kuna jamaa anaitwa Ali yupo Washington State mji wa Seattle ametuma madawati ya msaada bure kwa shule lakini wanataka alipe kodi wakati kuna watoto wanakaa chini. Kwasababu imefikia wakati hata hatufikirii tunakusanya kodi ya nini hasa kama sio kusaidia watu
 
..mimi nakueleza hali halisi.

..binafsi sizipingi hoja zako, lakini nina uhakika kwa mtizamo wetu zinaweza kuchukuliwa kama DHARAU kwa sisi tuliobaki nyumbani.

..Waswahili wana msemo, " ukitaka kula na kipofu usimshike mkono. "

..kwa hiyo mimi naendelea kusisitiza kwamba achaneni na uraia pacha, badala yake piganieni special status ya ukaazi.

..pia tumieni lugha ya kuomba na kunyenyeke, msitumie lugha ya kudai.

Cc Pascal Mayalla
 
Nikiwa kama mwanachama hai wa chama kinachojiandaa kushika madaraka nchini, na nikiwa mmoja ya Watanzania wanaolitazama taifa hili kama lulu ya ulimwengu, nikiwa na akili timamu, nitawasilisha hoja zangu tatu kwa chama changu Chadema ziwe agenda muhimu katika uchaguzi 2O2O.
Agenda hizo ni:

1. Mabadiliko ya mfumo wa ulinzi na usalama.

2. Uraia Pacha

3. Jamii za Wahindi na Waarabu wa Tanzania zitambuliwe rasmi na zishiriki shughuli zozote za utumishi wa nchi katika maeneo yote nyeti ya nchi.

Hoja ya kwanza nimeitafiti na kujiridhisha kwamba maendeleo ya taifa kwa vina vyote katika mlinganyo wa ulimwengu, mfumo wa vyombo hivi kwa sasa ni kikwazo kikubwa sana kufikia malengo.

Hoja ya 2. Nimejiridhisha kuwa taifa linakosa fursa na nyingi na hasa utaalamu na mitaji ya watanzania wenye uraia wa nchi nyingine kwasababu ambazo zimepitwa na wakati kwaulimwengu wa leo, Izingatiwe kuwa sababu kuu ya kuweka zuio la Watanzania walioghaibuni waliopata uraia wa nchi nyingine huko zilikuwa ni usalama hasa baada ya uhuru na kwenye harakati za ukombozi kusini mwa jangwa la sahara na katika kipindi cha Uhujumu Uchumi chini ya akina Sokoine. Sababu hizo na nyingi leo hazina mashiko....

Hoja ya tatu ni kuwa jamii hizi za wahindi na waarabu ambao ni watanzania halisi na tena kimsingi hazina uraia wa nchi zingi bali Tanzania tu, ndizo zinazochangia pato la taifa kwa ujumla kupitia mitaji yao ya uwekezaji nchini, ni jamii zilizo na wataalamu wa fani mbalimbali kama madaktari, wahandisi, na wachumi ambao leo wangeingia kwenye mifumo ya kiutumishi wa nchi kwa nyanja zote wataleta mafaa kwa taifa kuliko kukumbatia kasumba ambazo nadharia yake ni ubaguzi tu kwa raia nchini.

Ziko sababu nyingi sana za kutetea hoja zangu hizi, nitawasilisha hoja na utetezi wake naamini chama changu kitanielewa na kuzipokea hoja hizi kuwa sehemu ya agenda uchaguzi ujayo, na hazuwi agenda tu za maneno ili kujipatia ufuasi tu kama wale wenzetu 2OO5 walikuja na agenda ya OIC walipewa madaraka wakawatelekeza waliowaahidi.

Kisha 2O1O wakaja na utapeli mwingine wa Mahakama ya Kadhi, hawakutekeleza hadi 2O15, wakaja na utapeli mwingine kwamba watagawa milioni hamsini kila kijiji na watagawa laptop kila mwanafunzi wa Tanzania, matokeo yake kila mwanafunzi nchini anabeba dumu la maji na mfagio wa chelewa...

Chadema kama chama imara nchini usanii kwetu mwiko, tunaahidi unaloweza kutekeleza...!

Ili uelewe zaidi faida na hasara ya hoja hizi, soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.

Na Yericko Nyerere
View attachment 819746
Mkuu hoja zako ni za msingi HONGERA sana. Nadhani wakati ufike sasa uanze kujipambanua kitaifa zaidi kuliko kukumbatia Uchama.

Kiukweli kabisa bila kumung'unya maneno, kwa hali ya kisiasa ilivyo, chama chako kamwe hakiwezi kuja kutekeleza hizi sera hata iweje. Ni bora ungeishauri Serikali iliyopo kwa maslahi mapana ya Taifa. Sasa hivi tunatakiwa kuweka uvyama pembeni ili tutumie mawazo na vipaji vyetu kwa ajili ya Taifa letu bila kujali nani atakaetekeleza.
 
..mimi nakueleza hali halisi.

..binafsi sizipingi hoja zako, lakini nina uhakika kwa mtizamo wetu zinaweza kuchukuliwa kama DHARAU kwa sisi tuliobaki nyumbani.

..Waswahili wana msemo, " ukitaka kula na kipofu usimshike mkono. "

..kwa hiyo mimi naendelea kusisitiza kwamba achaneni na uraia pacha, badala yake piganieni special status ya ukaazi.

..pia tumieni lugha ya kuomba na kunyenyeke, msitumie lugha ya kudai.

Cc Pascal Mayalla

Kenya kumetokea nini kipya baada ya kuruhusu uraia pacha? Na kuhusu Land Kenya tena ni private sio kama kwetu. Ni matisho tu na tumechoka kutishiana. Hebu jaribuni siku mmoja Mtanzania mzawa mfukuzeni na mchukulieni urithi wake kwasababu ya uraia halafu uone hao ndugu zake watafanya nini! mtafanyia wahindi tu hili. Wajaribu waone matokeo yake yatakuwa nini kama patakalika hapo. Sheria za sasa hazitekelezeki tunaogopa wahindi, wachina, wakenya, warwanda na sasa tunaogopa Watanzania walio nje... huu ni upuuzi. Hivi unajua Nigeria kwa land ni ndogo kwa Tanzania na wapo zaidi ya milioni 160 mbona hawana shida ya land.
 
..hoja ya uraia pacha imepewa jina baya hapa Tz.

..so u have to be very careful unapoizungumzia.

..hivyo unavyoi-present wewe nakuhakikishia hautofika mbali, utakwama na kukosa kila kitu.

..usijenga hoja kama vile UNADAI. jenga hoja kama mtu ANAYEOMBA msaada.

..approach unayotumia kujenga hoja zako ilishajaribiwa wakati wa bunge maalum la katiba na ilifeli.

..mwakilishi wa diaspora ktk bunge la katiba alikuja kueleza vizuri sana nini kilitokea, kwanini hoja ya uraia pacha ilishindwa, na nini kifanyike mbele ya safari.

..mimi ushauri wangu ni kwamba mlioko nje muachane na hoja za uraia pacha. Badala yake, ombeni...nasisitiza ombeni mpewe status maalum ya ukaazi inayofanana na green card ya USA, au yellow card ya Ethiopia.

..pia u need to know the right ppl to lobby. Muwaepuke wapinzani wakati mkipeleka maombi yenu serekalini au bungeni.

Cc Pascal Mayalla, Nguruvi3
 
....mimi ushauri wangu ni kwamba mlioko nje muachane na hoja za uraia pacha. Badala yake, ombeni...nasisitiza ombeni mpewe status maalum ya ukaazi inayofanana na green card ya USA, au yellow card ya Ethiopia.[/USER]
Mkuu hili ni muhimu sana. Kuna makundi matatu kuhusu hoja hii

Kundi la Kwanza; ni diaspora wanaotaka uraia pacha. Diaspora wanafahamu Uraia na ukaazi wa kudumu tofauti zao ni ndogo. Tofauti kubwa ni kushiriki katika shughuli za 'siasa' kama kugombea au kupiga kura. Mambo mengine yote fursa zinabaki pale pale, si elimu si afya n.k.

Sioni kwanini Diaspora watake uraia pacha ikiwa inaonekana ni tatizo. Anayetaka kushiriki mambo yanayohitaji uraia kuna option ya kubaki na ukaazi wa kudumu wa nchi aliyopo akibaki na Uraia wa Tanzania. Hili litamwezesha kupata haki zake huko aliko na nyumbani

Kundi la pili; Ni la watu wasiotofautisha vitu hivi. Ukaazi wa kudumu (Permanent resident au green card etc) unatoa fursa na haki nyingi huko aliko.
Hii ni pamoja na kutohitaji vitu kama visa, work permit, study permit , afya, mikopo, elimu n.k.
Uraia pacha (dual citizenship) ni kuchukua uraia wa nchi anayoishi na ile ya nyumbani(Tz)
Kundi hili halitofautishi mambo hayo mawili, linadhani ni 'two in one'

Kundi la tatu; Hili linajua maana ya ukaazi wa kudumu na Uraia pacha.
Kundi hili linatumia uelewa finyu wa kundi la pili kuwachanganya.
Kwamba uraia pacha na ukaazi ni kitu kimoja
Hii ni baada ya kubaini kuwa bila kufanya 'mkanganyiko' huo halina hoja ya kuzuia ima uraia pacha au ukaazi wa kudumu. Kwa maneno mengine, kundi hili linasababisha 'distractions'

Kwa diaspora; Njia rahisi ni kuomba ukaazi wa kudumu. Huu hauna kikwazo kwasababu hata raia wa nchi nyingine wanaoishi Tanzania wanapata hadhi hiyo, sembuse mzawa aliyekwenda kutafuta. Hii hoja haiwezi kuzuiwa kwa hoja yoyote kimantiki

Ukaazi wa kudumu utawapa fursa na kupunguza mambo yasiyo ya lazima kama visa za kurudi nyumbani, umiliki wa vitu kama ardhi, ku renew visa baada ya muda n.k.

Kwa serikali; ukaazi wa kudumu hauna athari kiusalama au kiuzalendo.
Huu utapatikana itakapothibitika tu kuwa mhusika ni raia wa Tanzania aliyeacha uraia huo.

Hivyo mtu kutoka Pakistani hawezi kufanya abuse kwasababu asili yake haitampa fursa isipokuwa tu kufuata taratibu za wageni wanaotaka ukaazi wa kudumu

Kama serikali inatambua mchango wa diaspora kupitia remittance ambazo ni nyingi, kwanini serikali isione 'uzalendo huo'? Hapa ina maana hawa diaspora bado wanakumbuka na wanaguswa na hali za waliko toka. Hivyo kuwafanyia wepesi ni kuwapa incentives.
 
Nikiwa kama mwanachama hai wa chama kinachojiandaa kushika madaraka nchini, na nikiwa mmoja ya Watanzania wanaolitazama taifa hili kama lulu ya ulimwengu, nikiwa na akili timamu, nitawasilisha hoja zangu tatu kwa chama changu Chadema ziwe agenda muhimu katika uchaguzi 2O2O.
Agenda hizo ni:

1. Mabadiliko ya mfumo wa ulinzi na usalama.

2. Uraia Pacha

3. Jamii za Wahindi na Waarabu wa Tanzania zitambuliwe rasmi na zishiriki shughuli zozote za utumishi wa nchi katika maeneo yote nyeti ya nchi.

Hoja ya kwanza nimeitafiti na kujiridhisha kwamba maendeleo ya taifa kwa vina vyote katika mlinganyo wa ulimwengu, mfumo wa vyombo hivi kwa sasa ni kikwazo kikubwa sana kufikia malengo.

Hoja ya 2. Nimejiridhisha kuwa taifa linakosa fursa na nyingi na hasa utaalamu na mitaji ya watanzania wenye uraia wa nchi nyingine kwasababu ambazo zimepitwa na wakati kwaulimwengu wa leo, Izingatiwe kuwa sababu kuu ya kuweka zuio la Watanzania walioghaibuni waliopata uraia wa nchi nyingine huko zilikuwa ni usalama hasa baada ya uhuru na kwenye harakati za ukombozi kusini mwa jangwa la sahara na katika kipindi cha Uhujumu Uchumi chini ya akina Sokoine. Sababu hizo na nyingi leo hazina mashiko....

Hoja ya tatu ni kuwa jamii hizi za wahindi na waarabu ambao ni watanzania halisi na tena kimsingi hazina uraia wa nchi zingi bali Tanzania tu, ndizo zinazochangia pato la taifa kwa ujumla kupitia mitaji yao ya uwekezaji nchini, ni jamii zilizo na wataalamu wa fani mbalimbali kama madaktari, wahandisi, na wachumi ambao leo wangeingia kwenye mifumo ya kiutumishi wa nchi kwa nyanja zote wataleta mafaa kwa taifa kuliko kukumbatia kasumba ambazo nadharia yake ni ubaguzi tu kwa raia nchini.

Ziko sababu nyingi sana za kutetea hoja zangu hizi, nitawasilisha hoja na utetezi wake naamini chama changu kitanielewa na kuzipokea hoja hizi kuwa sehemu ya agenda uchaguzi ujayo, na hazuwi agenda tu za maneno ili kujipatia ufuasi tu kama wale wenzetu 2OO5 walikuja na agenda ya OIC walipewa madaraka wakawatelekeza waliowaahidi.

Kisha 2O1O wakaja na utapeli mwingine wa Mahakama ya Kadhi, hawakutekeleza hadi 2O15, wakaja na utapeli mwingine kwamba watagawa milioni hamsini kila kijiji na watagawa laptop kila mwanafunzi wa Tanzania, matokeo yake kila mwanafunzi nchini anabeba dumu la maji na mfagio wa chelewa...

Chadema kama chama imara nchini usanii kwetu mwiko, tunaahidi unaloweza kutekeleza...!

Ili uelewe zaidi faida na hasara ya hoja hizi, soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.

Na Yericko Nyerere
View attachment 819746
Unaweza kuruhusu uraia pacha kwa nia nzuri kabisa, lakini baadhi/wengi wakatumia hali hiyo kuhujumu nchi. Akiwachoka huku anaelekea kule.
 
Ndiomaana nchi yetu ikaridhia mikataba ya kimataifa ya usalama kama ya polisi ya kimataifa (interpol)
 
Hakuna hoja ulioileta hapo bali umeleta Kioja na hayo ndiyo majibu yako kaa chini jifunze ondoa ujuaji ongea na taja majina ya watu kwa heshima
Ndiyo maana hata huko Chadema wanakupuuza huna adabu.
Kwa hiyo umepoteza muda wako kujibu books? Kweli kuna watu na viatu.
 
Joka Kuu

"usijenga hoja kama vile UNADAI. jenga hoja kama mtu ANAYEOMBA msaada."

Najua una nia nzuri na unataka sisi tufanikiwe lakini sisi kama watoa mawazo tusijuzuie kutoa mawazo yetu halisia kwasababu ya kuogopa kukatiliwa. Kuwa free 100% kusema kilichoko moyoni kwako. Usijaribu kuwa strategist wa kisiasa hapa sio sehemu yake. Nikupe tu statistics chache kukuonyesha kwanini sio vizuri kufikiri kisiasa na ni fikra zisizo ona umbali. Kwanza tujiulize Watanzania mtu wa kawaida ni nani? Kwa takwimu umri wa kati wa Tanzania kwasasa ni miaka 17-18 hivyo umri wa kati wa Watanzania ni teenagers na hii ni fact. Sio hivyo tu 67% ya Watanzania wote wapo chini ya miaka 25. Hizi ni data rahisi tu kwenye google na mashirika ya kimataifa. Sasa hoja ya kwanza. Unasema Watanzania wengi hawa 67% wakati wa katiba mpya miaka michache walikuwa watoto hivyo kama kuna agenda ni za kulishwa na hawawezi kuelewa logic wakati ule. Wengi wao hawajui hata dispora ni nini na na bet asilimia zaidi ya 90 hawajawahi kwenda nje ya Tanzania na asilimia 90% ya hao wakipata nafasi ya kwenya kusoma nje kama US wataenda na watachukua uraia kama utanufaisha maisha ya ndugu, watoto, community na nchi yao kwa namna fulani. Hivyo tusiseme bila data kwamba Watanzania wanapinga, sio Watanzania wengi ni wachache walio na sauti kubwa na sio future population ya Tanzania hili la kwanza. Vile vile hii sio issue ya kudai wala kuomba ni nchi ya usawa tu. Tunamuomba nani hasa Watanzania au viongozi maana hakuna data za kuonyesha Watanzania wengi wanapinga zaidi ya waliopewa madaraka kuna wanaopinga. Lakini vilevile kikubwa hapa kwenye mijadala tujaribu kutoa sababu za msingi kwanini uraia pacha ni tatizo 1,2,3.... na kwanini sio tatizo 1,2,3.... sio kila kitu ni cha kuangalia kisiasa na joto la wakati huo maana hatujui miaka 2-5 Tanzania itakuwa vipi kwasababu jiulize hao watoto wangapi watakuwa wapiga kura, waelewa zaidi na wanajua uchumi. Point zako zinaonekana vizuri sana leo lakini ni kisiasa zaidi na sisi hapa tupo kama waelimishaji. Mimi na miaka yangu 20 US sitakuwa natenda mema kama nitasema sema tu siasa za sasa ni ngumu hivyo tusifanye hivi au vile badala yake ni kuelimisha na kusema ukweli kutokana na uzoefu. Sio Watanzania wengi wamefanikiwa kuja hapa na miaka 21 kama mimi 1997 na kukaa na kupata uzoefu wa kuona mengi kama mimi pande zote TZ na hapa. asilimia 67% ya watanzania wakiwa na miaka 4 tu au hawajazaliwa. Sitaweza kuangalia siasa kwa miaka miwili nina wajibu wa kutoa na kuelimisha. Lakini tujue Waziri wa mambo ya nje na waziri mkuu wanajua hili na ku support .
 
Back
Top Bottom