Nitawasilisha hoja tatu kwa chama changu CHADEMA

Nitawasilisha hoja tatu kwa chama changu CHADEMA

Kwanza uraia pacha hatuhitaji kwa sasa utatumika kama kichochoro cha kutuibia rasrimali zetu.
Hoja yako sidhani kama ina mashiko,mtanzania diaspora amepewa uraia wa huko anawezaje kuja kutuibia?!
 
Yericko tokea utangaze operation kataa fisadi Lowasa kwenda ikulu, alafu mkahongwa mapesa na kubadili gia angani na kuanza kumwabudu Lowasa, hamuaminiki tena mbele ya macho ya watanzania.

2020 chadema ikiambulia hata wabunge 10 wakatambikeee.
 
Kwanza uraia pacha hatuhitaji kwa sasa utatumika kama kichochoro cha kutuibia rasrimali zetu.
Pili wahindi na waarabu walio na uraia halisi wanapata huduma kama kawaida hivyo haihitaji kuwapa special treatment ukitilia maanani wengi wao ndiyo waliotufikisha hapa kwakushirikiana na watz wasiokuwa waaminifu. Ila kama mnafikiri chadema hiyo itawatoa karibuni 2020!
Ndugu kwa sasa hatuibiwi raslimali zetu?
 
Yericko tokea utangaze operation kataa fisadi Lowasa kwenda ikulu, alafu mkahongwa mapesa na kubadili gia angani na kuanza kumwabudu Lowasa, hamuaminiki tena mbele ya macho ya watanzania.

2020 chadema ikiambulia hata wabunge 10 wakatambikeee.
Huyu kijana ameporomoka kwa kasi ya ajabu.
 
Ee Mwenyezi Mungu saidia hili genge lisambaratike na lifutike. Limejaa watu wenye ukanda, ubinafsi, tamaa ya madaraka, wahuni. Amen.
 
Mara paap!..trafiki muhindi anakupiga mkono..swali: umebeba nini ?!!..jibu:Ng'ombe afande!..swali:hujui kama hiyo ni mungu?!!..just joking

Mleta mada kwa kiwango fulani anapoint, ila wrong party,haya mapendekezo si mabaya haswa uraia pacha.
Hahaha
 
3. Jamii za Wahindi na Waarabu wa Tanzania zitambuliwe rasmi na zishiriki shughuli zozote za utumishi wa nchi katika maeneo yote nyeti ya nchi.....
Na watoto wao na wetu weusi waoane tuungane kikweli kweli na siyo kwa maneno tu..😉🙂😛😎
 
Nikiwa kama mwanachama hai wa chama kinachojiandaa kushika madaraka nchini, na nikiwa mmoja ya Watanzania wanaolitazama taifa hili kama lulu ya ulimwengu, nikiwa na akili timamu, nitawasilisha hoja zangu tatu kwa chama changu Chadema ziwe agenda muhimu katika uchaguzi 2O2O.
Agenda hizo ni:

1. Mabadiliko ya mfumo wa ulinzi na usalama.

2. Uraia Pacha

3. Jamii za Wahindi na Waarabu wa Tanzania zitambuliwe rasmi na zishiriki shughuli zozote za utumishi wa nchi katika maeneo yote nyeti ya nchi.

Hoja ya kwanza nimeitafiti na kujiridhisha kwamba maendeleo ya taifa kwa vina vyote katika mlinganyo wa ulimwengu, mfumo wa vyombo hivi kwa sasa ni kikwazo kikubwa sana kufikia malengo.

Hoja ya 2. Nimejiridhisha kuwa taifa linakosa fursa na nyingi na hasa utaalamu na mitaji ya watanzania wenye uraia wa nchi nyingine kwasababu ambazo zimepitwa na wakati kwaulimwengu wa leo, Izingatiwe kuwa sababu kuu ya kuweka zuio la Watanzania walioghaibuni waliopata uraia wa nchi nyingine huko zilikuwa ni usalama hasa baada ya uhuru na kwenye harakati za ukombozi kusini mwa jangwa la sahara na katika kipindi cha Uhujumu Uchumi chini ya akina Sokoine. Sababu hizo na nyingi leo hazina mashiko....

Hoja ya tatu ni kuwa jamii hizi za wahindi na waarabu ambao ni watanzania halisi na tena kimsingi hazina uraia wa nchi zingi bali Tanzania tu, ndizo zinazochangia pato la taifa kwa ujumla kupitia mitaji yao ya uwekezaji nchini, ni jamii zilizo na wataalamu wa fani mbalimbali kama madaktari, wahandisi, na wachumi ambao leo wangeingia kwenye mifumo ya kiutumishi wa nchi kwa nyanja zote wataleta mafaa kwa taifa kuliko kukumbatia kasumba ambazo nadharia yake ni ubaguzi tu kwa raia nchini.

Ziko sababu nyingi sana za kutetea hoja zangu hizi, nitawasilisha hoja na utetezi wake naamini chama changu kitanielewa na kuzipokea hoja hizi kuwa sehemu ya agenda uchaguzi ujayo, na hazuwi agenda tu za maneno ili kujipatia ufuasi tu kama wale wenzetu 2OO5 walikuja na agenda ya OIC walipewa madaraka wakawatelekeza waliowaahidi.

Kisha 2O1O wakaja na utapeli mwingine wa Mahakama ya Kadhi, hawakutekeleza hadi 2O15, wakaja na utapeli mwingine kwamba watagawa milioni hamsini kila kijiji na watagawa laptop kila mwanafunzi wa Tanzania, matokeo yake kila mwanafunzi nchini anabeba dumu la maji na mfagio wa chelewa...

Chadema kama chama imara nchini usanii kwetu mwiko, tunaahidi unaloweza kutekeleza...!

Ili uelewe zaidi faida na hasara ya hoja hizi, soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.

Na Yericko Nyerere
View attachment 819746
Habari za alfajiri Chief,huwa nasoma makala zako nyingi na unakua na hoja nzito na zenye mashiko,samahani naomba tuwekane sawa kwenye hoja ya uraia pacha kitu ambacho napingana nacho kitambo
Labda ningependa kufamu hili kwa uchache,umefikiri vipi kuhusu mtanzania masikini anaeishi kwa mlo mmoja n mwenye kipato cha wastani kwenye swala la umiliki wa Ardhi?
 
Eti kina Sokoine kwanza huna Adabu kabisa, Jasusi Uchwara mpotoshaji wa Historia hivi unaleta mzaha kwenye mambo ya OIC au Mahakama ya Kadhi? Hovyo kabisa kama hizi ndiyo hoja zenu na chama chako msahau kuchukua uongozi nchi hii.
 
Sheria ya ardhi iko vizuri, serikali ni mdhamini mkuu wa ardhi hiyo, raia wa Tanzania hukodishwa tu kwa mkataba wa miaka 33, 66 na 99. Hili sioni kama linatatizo mkuu
 
Eti kina Sokoine kwanza huna Adabu kabisa, Jasusi Uchwara mpotoshaji wa Historia hivi unaleta mzaha kwenye mambo ya OIC au Mahakama ya Kadhi? Hovyo kabisa kama hizi ndiyo hoja zenu na chama chako msahau kuchukua uongozi nchi hii.
Ndugu unataka kusemaje ndugu mbona hueleweki, unaunga mkono hoja au unakinzana nayo? Lete hoja sio viroja
 
Kwanza tunakubaliana kwamba wako Wahindi wa Tanzania na Waarabu ambao ni raia halali wa Tanzania? Ikiwa tunafahamu hivyo, je tunafahamu haki za raia wa Tanzania zinazolindwa kwa Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977?

Sura ya 3, Ibara ya 13.
________________________
Kifungu cha (4), "Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu aumamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote yaMamlaka ya Nchi.

(5) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii neno "kubagua" maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao,kabila, pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini, jinsia au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni nakuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima, isipokuwa kwamba neno "kubagua" halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia Serikali kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebishamatatizo katika jamii".
 
Ndugu unataka kusemaje ndugu mbona hueleweki, unaunga mkono hoja au unakinzana nayo? Lete hoja sio viroja
Hakuna hoja ulioileta hapo bali umeleta Kioja na hayo ndiyo majibu yako kaa chini jifunze ondoa ujuaji ongea na taja majina ya watu kwa heshima
Ndiyo maana hata huko Chadema wanakupuuza huna adabu.
 
Hoja ya 3 ili ifanikiwe labda maslahi kwenye utumishi wa umma uboreshwe...

Cc: mahondaw
 
Hakuna hoja ulioileta hapo bali umeleta Kioja na hayo ndiyo majibu yako kaa chini jifunze ondoa ujuaji ongea na taja majina ya watu kwa heshima
Ndiyo maana hata huko Chadema wanakupuuza huna adabu.
Nisamehe mkuu nilidhani naongea na mtu mzima kumbe darasa la saba... Haya endelea kuhoroja ndugu
 
"Chadema kama chama imara nchini usanii kwetu mwiko, tunaahidi unaloweza kutekeleza...!"

Hili hitimisho lako limenichekesha sana!

Mwenyekiti wako wa taifa aliwahi kusema kama CCM itachomoka kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 basi yeye ataachia ngazi ya Uenyekiti wa Taifa.

Leo ni July 2018 bado yupo! Kama huu sio usanii basi nadhani neno usanii lina maana nyingine.
haha hahaa
 
Back
Top Bottom