Nitawasilisha hoja tatu kwa chama changu CHADEMA

Nitawasilisha hoja tatu kwa chama changu CHADEMA

Hoja ya 3 ningefurahi ungetufafanulia wanazuiwa kipi na kwa sheria ipi
 
Ajenda ya ufisadi imekuufa baada ya EL kununua chama kwa bilioni 9!! Slaa aliondoka na ajenda yake iliyokipa chama umaarufu.
 
Dawa ya moto ni moto nakuambia tena acha kujipendekeza wewe kwa rangi rangi ni vyele tambi .. miafrika bhana kweli ndivo tulivo babu zako walionyeshwa vioo wakatoa almas wewe ushaonyeshwa sijui nini unatuletea uchuro hapa.
Aisee kuna watu na viatu
 
Ajenda ya ufisadi imekuufa baada ya EL kununua chama kwa bilioni 9!! Slaa aliondoka na ajenda yake iliyokipa chama umaarufu.
Nani kakudanganya? Agenda sio maneno ni vitendo, ufisadi wa 1.5tr ni vyama mbadala ndio wameligundua na kulivalia njuga nk
 
Miaka yote mshindi anakuwa huyo huyo mmoja tu. Huo ni udhaifu ambao hamuuoni, pengine ni kikwazo cha kukua kwa chama chenu.

Mnahitaji mawazo mapya, watu wapya ili muweze kuwa na mikakati mipya ambayo inaweza kukupatieni ushindi wa kitaifa. Mnatumia silaha zile zile kupambana na adui anayeelewa maana ya mabadiliko ya ndani ya chama, ni vigumu sana kufanikiwa.
Unakinzana na demokrasia?
 
Yericko Yericko !!!!
Dhana ya tatu hujaitendea haki kabisa.

Unaizungumzia kama vile hilo jina lako la mwisho umechovya yaani J.K. Nyerere hukumfuatilia au hukumuelewa kabisa hasa pale alipowapa uongozi sehemu mbalimbali hata zile sehemu au idara nyeti jamii ya hao watu uliowataja.

Hujamuelewa Nyerere mwenzio hata pale alipotoa tafsiri ya makaburu na wabaguzi.

Kama Nyerere asingefanya hicho unachojaribu kushauri leo wa Tz wangemjulia wapi Prof. Issa Shivj?

Daah nimesikitika sana jinsi ulivyo shindwa kutambua nchi yetu ilivyo wapa fursa watu wa jamii ulizozisema hasa kipindi cha Nyerere na Mwinyi muondoe huyu wa sasa ambae sio mwanasiasa au mwana diplomasia au sio mwanafalsafa kama viongozi wa awamu ya kwanza na ya pili.
mie mwenyewe ninamshangaa mbona bungeni tu wamejazana wabunge wenye asili ya kihindi na kiarabu wengi sana
 
Unakinzana na demokrasia?
Demokrasia ya kwenu imekaa kisanii zaidi. Mtu anapokaa kwenye uongozi kwa muda mrefu hutengeneza mazingira ya kuogopwa, ni rahisi kutengeneza makundi ya chini kwa chini yenye kufanya kazi ya kumtumikia yeye badala ya chama.

Hamjachelewa kufanya mabadiliko ndani ya chama, kama kweli mnataka kuitoa CCM pale magogoni.
 
Watakuelewa? Na ushauri tayari umeupeleka UFIPA au umeanzia jf?
 
Nikiwa kama mwanachama hai wa chama kinachojiandaa kushika madaraka nchini, na nikiwa mmoja ya Watanzania wanaolitazama taifa hili kama lulu ya ulimwengu, nikiwa na akili timamu, nitawasilisha hoja zangu tatu kwa chama changu Chadema ziwe agenda muhimu katika uchaguzi 2O2O.
You are no longer the 'insider' or what!? Ama hawakusikilizi siku hizi. Hii si dalili nzuri kwa hicho chama.
----
Nimeshtuka sana.
 
378880.jpg


hhahahahahahahaahha
Kama Felix Wazekwa. Hahah
 
Nikiwa kama mwanachama hai wa chama kinachojiandaa kushika madaraka nchini, na nikiwa mmoja ya Watanzania wanaolitazama taifa hili kama lulu ya ulimwengu, nikiwa na akili timamu, nitawasilisha hoja zangu tatu kwa chama changu Chadema ziwe agenda muhimu katika uchaguzi 2O2O.
Agenda hizo ni:

1. Mabadiliko ya mfumo wa ulinzi na usalama.

2. Uraia Pacha

3. Jamii za Wahindi na Waarabu wa Tanzania zitambuliwe rasmi na zishiriki shughuli zozote za utumishi wa nchi katika maeneo yote nyeti ya nchi.

Hoja ya kwanza nimeitafiti na kujiridhisha kwamba maendeleo ya taifa kwa vina vyote katika mlinganyo wa ulimwengu, mfumo wa vyombo hivi kwa sasa ni kikwazo kikubwa sana kufikia malengo.

Hoja ya 2. Nimejiridhisha kuwa taifa linakosa fursa na nyingi na hasa utaalamu na mitaji ya watanzania wenye uraia wa nchi nyingine kwasababu ambazo zimepitwa na wakati kwaulimwengu wa leo, Izingatiwe kuwa sababu kuu ya kuweka zuio la Watanzania walioghaibuni waliopata uraia wa nchi nyingine huko zilikuwa ni usalama hasa baada ya uhuru na kwenye harakati za ukombozi kusini mwa jangwa la sahara na katika kipindi cha Uhujumu Uchumi chini ya akina Sokoine. Sababu hizo na nyingi leo hazina mashiko....

Hoja ya tatu ni kuwa jamii hizi za wahindi na waarabu ambao ni watanzania halisi na tena kimsingi hazina uraia wa nchi zingi bali Tanzania tu, ndizo zinazochangia pato la taifa kwa ujumla kupitia mitaji yao ya uwekezaji nchini, ni jamii zilizo na wataalamu wa fani mbalimbali kama madaktari, wahandisi, na wachumi ambao leo wangeingia kwenye mifumo ya kiutumishi wa nchi kwa nyanja zote wataleta mafaa kwa taifa kuliko kukumbatia kasumba ambazo nadharia yake ni ubaguzi tu kwa raia nchini.

Ziko sababu nyingi sana za kutetea hoja zangu hizi, nitawasilisha hoja na utetezi wake naamini chama changu kitanielewa na kuzipokea hoja hizi kuwa sehemu ya agenda uchaguzi ujayo, na hazuwi agenda tu za maneno ili kujipatia ufuasi tu kama wale wenzetu 2OO5 walikuja na agenda ya OIC walipewa madaraka wakawatelekeza waliowaahidi.

Kisha 2O1O wakaja na utapeli mwingine wa Mahakama ya Kadhi, hawakutekeleza hadi 2O15, wakaja na utapeli mwingine kwamba watagawa milioni hamsini kila kijiji na watagawa laptop kila mwanafunzi wa Tanzania, matokeo yake kila mwanafunzi nchini anabeba dumu la maji na mfagio wa chelewa...

Chadema kama chama imara nchini usanii kwetu mwiko, tunaahidi unaloweza kutekeleza...!


Ili uelewe zaidi faida na hasara ya hoja hizi, soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.


Na Yericko Nyerere


Mimi na support point zako na ni vizuri kuona vijana wachache kama wewe wanao ona mbali. Watanzania wengi kwenye swala la uraia pacha wajiulize tofauti.

Je kuna Hasara gani kwa Mtanzania kuchukuwa uraia wa nchi nyingine?
Je ni sababu zipi hasa zinasababisha Mtanzania kuchukuwa uraia wa nchi nyingine?

Iko siku nitaeleza kwa kirefu lakini naomba nitumie muda huu kuwapa ukweli na mifano ya kweli kwa uzoefu wangu.

Kwanza nimeishi hapa US mwaka huu utakuwa wa 20!. Nimekuja nikiwa na miaka 21. Sababu kubwa sana na umuhimu wa kuchukuwa uraia ni kuwa na haki na usawa mfano Elimu hapa usikokuwa na uraia hupati mkopo na unalipa penalty inaitwa international student fee hivyo ni sababu mojawapo ya Watanzania wengi kusoma kwa muda mrefu sana au kutosoma ni gharama kubwa. Sababu nyingine ni kazi kupata kazi nzuri za kisomi unahitaji uraia. Kusafiki kwenda nyumbani uraia unasadia.

Lakini pamoja na hayo hapo juu nilienda kuoa Bongo nilivyorudi tu mke wangu akaumwa serious sana kwa mwaka wa kwanza gharama za matibabu yalikuwa $700,000 mwaka wa pili ni $550,000. Mke wangu leo hii yuko hai kwasababu nilikuwa na bima na nimetumia kama $6000 tu. Bima nisingeweza kupata bila kazi na kazi nisingeweza kupata bila uraia. Mke wangu ni Mtanzania. Sasa kwa wale wanaosema uzalendo ningeacha mke wangu afe!, gharama za kuuguza ningeweza vipi bila kazi. Lakini pamoja na majanga yangu yote bado nasadia nyumbani kwa vipesa vya hapa na pale. Najenga, nasomesha mtoto wa kaka, natuma pesa kwa bibi na wazazi. Sasa kwa mnaotaka wote tuwe nyumbani tunaongea tu ... sio wote tutapata nafasi za kazi au biashara Watanzania tuko milioni 56 hawa diaspora hawazidi milioni 2. Pesa dispora wanaleta kuliko wanayochukua zaidi ya trilioni moja kwa mwaka na hiyo ni inayopitia mitandao tu sio ya kutumana. Sasa badala ya kujiuliza wana faida gani tujiulize wana hasara gani / je wata tu cost kwenye lipi kimaendeleo yaani negatively. Madongo hayasadii watu tuna maisha serious na tunapigana sana kusaidia jamii zetu
 
Kamundu,

..diaspora mngeomba kuwa na status maalum ya ukaazi[kitu kama green card] badala ya uraia pacha.

..uraia pacha unatutisha sana waTz na tayari umeshapewa jina baya. it will be such an uphill batttle kubadilisha mtizamo wetu kuhusu suala hilo.
 
3. Jamii za Wahindi na Waarabu wa Tanzania zitambuliwe rasmi na zishiriki shughuli zozote za utumishi wa nchi katika maeneo yote nyeti ya nchi.
Mara paap!..trafiki muhindi anakupiga mkono..swali: umebeba nini ?!!..jibu:Ng'ombe afande!..swali:hujui kama hiyo ni mungu?!!..just joking

Mleta mada kwa kiwango fulani anapoint, ila wrong party,haya mapendekezo si mabaya haswa uraia pacha.
 
Nikiwa kama mwanachama hai wa chama kinachojiandaa kushika madaraka nchini, na nikiwa mmoja ya Watanzania wanaolitazama taifa hili kama lulu ya ulimwengu, nikiwa na akili timamu, nitawasilisha hoja zangu tatu kwa chama changu Chadema ziwe agenda muhimu katika uchaguzi 2O2O.
Agenda hizo ni:

1. Mabadiliko ya mfumo wa ulinzi na usalama.

2. Uraia Pacha

3. Jamii za Wahindi na Waarabu wa Tanzania zitambuliwe rasmi na zishiriki shughuli zozote za utumishi wa nchi katika maeneo yote nyeti ya nchi.

Hoja ya kwanza nimeitafiti na kujiridhisha kwamba maendeleo ya taifa kwa vina vyote katika mlinganyo wa ulimwengu, mfumo wa vyombo hivi kwa sasa ni kikwazo kikubwa sana kufikia malengo.

Hoja ya 2. Nimejiridhisha kuwa taifa linakosa fursa na nyingi na hasa utaalamu na mitaji ya watanzania wenye uraia wa nchi nyingine kwasababu ambazo zimepitwa na wakati kwaulimwengu wa leo, Izingatiwe kuwa sababu kuu ya kuweka zuio la Watanzania walioghaibuni waliopata uraia wa nchi nyingine huko zilikuwa ni usalama hasa baada ya uhuru na kwenye harakati za ukombozi kusini mwa jangwa la sahara na katika kipindi cha Uhujumu Uchumi chini ya akina Sokoine. Sababu hizo na nyingi leo hazina mashiko....

Hoja ya tatu ni kuwa jamii hizi za wahindi na waarabu ambao ni watanzania halisi na tena kimsingi hazina uraia wa nchi zingi bali Tanzania tu, ndizo zinazochangia pato la taifa kwa ujumla kupitia mitaji yao ya uwekezaji nchini, ni jamii zilizo na wataalamu wa fani mbalimbali kama madaktari, wahandisi, na wachumi ambao leo wangeingia kwenye mifumo ya kiutumishi wa nchi kwa nyanja zote wataleta mafaa kwa taifa kuliko kukumbatia kasumba ambazo nadharia yake ni ubaguzi tu kwa raia nchini.

Ziko sababu nyingi sana za kutetea hoja zangu hizi, nitawasilisha hoja na utetezi wake naamini chama changu kitanielewa na kuzipokea hoja hizi kuwa sehemu ya agenda uchaguzi ujayo, na hazuwi agenda tu za maneno ili kujipatia ufuasi tu kama wale wenzetu 2OO5 walikuja na agenda ya OIC walipewa madaraka wakawatelekeza waliowaahidi.

Kisha 2O1O wakaja na utapeli mwingine wa Mahakama ya Kadhi, hawakutekeleza hadi 2O15, wakaja na utapeli mwingine kwamba watagawa milioni hamsini kila kijiji na watagawa laptop kila mwanafunzi wa Tanzania, matokeo yake kila mwanafunzi nchini anabeba dumu la maji na mfagio wa chelewa...

Chadema kama chama imara nchini usanii kwetu mwiko, tunaahidi unaloweza kutekeleza...!


Ili uelewe zaidi faida na hasara ya hoja hizi, soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.


Na Yericko Nyerere

Kwani huko Chadema huwa Hamna vikao vya chama mpaka ulete huku JF?
 
Hoja ya 3 ningefurahi ungetufafanulia wanazuiwa kipi na kwa sheria ipi
Hakuna sheria inayowazuia, katiba ya nchi inawatambua kuwa kila raia ana haki sawa katika Jamhuri.

Kinachowazuia ni sheria ya asili inayoishi kwenye akili za wanaoitwa/wanaojiita wazawa nawahindi/waarabu wenyewe. Ikiwa kutakuwa na kifungu cha kisheria kitakacho kazia haki ya kikatiba kwakutamka bayani kwamba jamii za wahindi na waarabu zitakuwa na haki sawa kokote katika nchi na zitatumikia nchi eneo lolote bila kikwazo, hilo litaifuta natural law.
 
Mara paap!..trafiki muhindi anakupiga mkono..swali: umebeba nini ?!!..jibu:Ng'ombe afande!..swali:hujui kama hiyo ni mungu?!!..just joking

Mleta mada kwa kiwango fulani anapoint, ila wrong party,haya mapendekezo si mabaya haswa uraia pacha.
Hahahaaahaa
 
Kamundu,

..diaspora mngeomba kuwa na status maalum ya ukaazi[kitu kama green card] badala ya uraia pacha.

..uraia pacha unatutisha sana waTz na tayari umeshapewa jina baya. it will be such an uphill batttle kubadilisha mtizamo wetu kuhusu suala hilo.
Mkuu JokaKuu

Kwanza shikamok mzee wangu, naamini wewe ni mzee wangu nikiangalia mijadala yetu ya siki nyingi tuliyoghani humu,

Habari za siku nyingi mzee wangu, tumeachana humu siku nyingi, nadhani tangu mijadala ya Historia ya Uhuru wa Tanganyika tukiwa na mzee Mohamed Said Nguruvi3 na Mag3

Kwenye huu mjadala hasa hoja hii ya uraia wa nchi mbili, ninakumbuka vema na ninaamini hoja hii inajibiwa na Rasimu ya katiba ya Warioba iliyosemaà raia wa Tanzania WALIO nje na uraia wa huko, "watapewa vibali maalumu (mfano Green Card) vya kuwatambua wao na watoto wao vinavyowapa haki sawa na Watanzania wengine isipokuwa vitu viwili tu..

1.Kugombea nafasi Za uongozi Wa kisiasa .

2.Kupiga kura katika chaguzi Za Tanzania.

Inawezekana kungekuwa na dhamira ya kimamlaka (rais) ya kuhakikisha katiba ile inafanikiwa, hakika hili lisingekuwa hoja leo... Lakini tuliruhusu siasa ziingie kuandika katiba matokeo wote tunayajua....
 
Unaionaje hoja husika mkuu
Kwanza uraia pacha hatuhitaji kwa sasa utatumika kama kichochoro cha kutuibia rasrimali zetu.
Pili wahindi na waarabu walio na uraia halisi wanapata huduma kama kawaida hivyo haihitaji kuwapa special treatment ukitilia maanani wengi wao ndiyo waliotufikisha hapa kwakushirikiana na watz wasiokuwa waaminifu. Ila kama mnafikiri chadema hiyo itawatoa karibuni 2020!
 
Back
Top Bottom