Nitawashangaa sana AU wakikubali mapinduzi Zimbabwe!

Nitawashangaa sana AU wakikubali mapinduzi Zimbabwe!

europé tiyari washaingilia hawawezi kumpa support anayekuja kama ajafata wanavyotaka boris Johson uk foreign minister
bbc source
Nomemsikiliza akiongea kinafiki tu...sijamsikia akishutumu mapinduzi
 
Ghadaffi aliondolewa na kuuawa kinyama kwa maslahi ya wazungu na hatima ya nchi ya libya imekuwa ni mbaya sana na kupelekea vita visivyoisha na ukimbizi wa aina yake duniani.

leo hii tunashuhudia jaribio la kumuondoa Mugabe kwa mapinduzi baada ya mbinu za kidemokrasia kushindwa.

Kwa mujibu wa BBC wazungu wanaamini kuwa Zimbabwe imekuwa mismanaged kwa miaka zaidi ya 37...msimamo huu unahusianishwa na yeye kuwafukuza matajiri wachache kwa manufaa ya umma.

Leo hii wazungu wanatuaminisha kuwa nchi ya Zimbabwe imeharibika kutokana na kuondoa mazingira ya unyonyaji wa wawekezaji wa kizungu.

Siku zote wazungu wamesisitiza kuhusu kubadilisha utawala kwa njia ya demokrasia...kwa nini wachekelee mapinduzi? Kwa nini hawatumii maguvu yao kuzuia mapinduzi?Je mfumo wa mapinduzi ni sehemu ya njia bora za kubadilisha tawala?

Ni wakati AU kuonesha makucha yake na kukataa double standards katika Demokrasia.Au wanapaswa kupinga kwa kauli na matendo yote dhidi ya mapinduzi haya ya kijeshi.

AU wasipoponga au UN wasipopinga mapinduzi basi tusuwasikie tena kupinga mapinduzi sehemu yoyote duniani.

Inasemekana jeshi la Zimbabwe liliwasiliana na China ili kufanya hayo wanayotaka kufanya...kama hili ni kweli basi AU haina budi kumuonya China na ikiwezekana kumkataa kama muwekezaji kwani naye atakuwa amekubaliana na wazungu kuimaliza Afrika.

AU watakuwa na kikao kinachohusu usalama kesho...tusubiri tuone tamko lao.

Mugabe hajapinduliwa, atajiuzuru mwenyewe hapo kesho
 
Kilichotokea Zimbabwe ni mtifuano ndani ya chama tawala,wapinzani hata hawahusiki,na hamna hata pressure kutoka nje,wananchi walikuwa wameshamchoka,na inaonekana chama chake pia ilimchoka
 
Mugabe hajapinduliwa, atajiuzuru mwenyewe hapo kesho
lets hope so...but so far vyombo vya Magharibi vinatueleza amepibduliwa na jeshi la nchi hiyo limeshindwa kujieleza vizuri.

Je kwa nini jumuiya ya kimataifa imekaa kimya dhidi ya mapinduzi ya kijeshi???
 
Kilichotokea Zimbabwe ni mtifuano ndani ya chama tawala,wapinzani hata hawahusiki,na hamna hata pressure kutoka nje,wananchi walikuwa wameshamchoka,na inaonekana chama chake pia ilimchoka
Sijasikia kuwa wananchi walimchoka
 
Ziko njia za kidemokrasia za kumpumzisha
Kama zipi hizo? Za kuweka vyombo vyote vya utawala na maamuzi mikononi mwa mhimili uliojichimbia zaidi? You can fool a few people all the time but not all people forever.
 
lets hope so...but so far vyombo vya Magharibi vinatueleza amepibduliwa na jeshi la nchi hiyo limeshindwa kujieleza vizuri.

Je kwa nini jumuiya ya kimataifa imekaa kimya dhidi ya mapinduzi ya kijeshi???
Tayari makamu wake kashapewa urais hata baadhi ya vyombo vya habari hapa Africa vimeshatangaza
 
Kama zipi hizo? Za kuweka vyombo vyote vya utawala na maamuzi mikononi mwa mhimili uliojichimbia zaidi? You can fool a few people all the time but not all people forever.
Kura ndio njia sahihi ya kubadili utawala
 
Tayari makamu wake kashapewa urais hata baadhi ya vyombo vya habari hapa Africa vimeshatangaza
Jumuiya ya kimataifa hasa AU ni lazima ipinge hilo
 
Unashangaa nini? Ulitaka Mugabe aendelee kuvuruga Demokrasia Kwa kutawala kama mfalme
 
Dah! Yaani kuna watu mmebarikiwa kumjua mgonjwa wa tumbo hata kwa kumuangalia makalio tu...!
Kwako wewe ni ajabu lakini kwa madaktari hilo ni jambo la kawaida sana.hivi mtu anayeharisha mfululizo huwezi kuona matako yaliyochubuka?
 
Back
Top Bottom