~~ nitarudi chi-town ~~ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

~~ nitarudi chi-town ~~

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, May 3, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Na. M. M. Mwanakijiji
  2151055118_317a87feb3.jpg

  Toka mbali niliweza kuona Jiji la Chicago likianza kuibuka mbele ya uso wangu utadhani ule mji wa Kibiblia ulioshushwa toka mbinguni. Kwa mbali niliweza kuona Jengo refu kabisa la Sears Tower likinikaribisha katika mji huo wa “Upepo”. Kama kuna kitu ambacho ilinibidi nifunze mara moja ni jinsi ya kuendesha gari hasa unapojaribu kuingia jijini hapo. Kuna matengenezo makubwa yanaendelea katika barabara ya I-94/90 inayopita katikati ya jiji hilo. Nikiwa bado na ushamba ushamba wangu wa kijijini nilijikuta nakoswa koswa na madereva wa Chicago ambao bila shaka waligundua kuwa mimi ni mgeni kwani gari langu lilikuwa na namba za Jimbo jingine. Hata hivyo moyo wangu ulifurahi kwani hii ilikuwa ni mara ya kwanza kuingia katika jiji hili na kukaa kwa muda kidogo.

  Niliachana na barabara kuu ya I-94 na kuchukua mtaa wa Randolph na kuingia jijini kwenyewe. Nilipigwa na butwaa kwani jiji la Chicago lilijaa watu waliokuwa katika pirika pirika zao za siku ya Jumamosi. Hali ya hewa ilikuwa ni murua kabisa na jua ndo lilikuwa likiangaza utadhani limetumwa. Hii ilinikumbusha kwa sekunde chache nyumbani Bongo mitaa ya Posta. Pole pole niliamua kutafuta mahali ambapo ningeliweza kuegesha gari langu. Nilikata kona katika mtaa wa Wabash ambao sehemu yake imefunikwa na reli ya jijini hapo. Kila baada ya dakika chache ngurumo ya treni inayozunguka jijini hapo ilisikika. Nikashangaa sijui watu wanafanya kazi vipi hapo na mtikisiko na ngurumo hivo. Na hilo nalo likanikumbusha watu wanoishi pale Kipawa karibu na uwanja wa ndege. Kumbe kwa mazoea watu wanalala usingizi licha ya ngurumo za ndege mchana kutwa na usiku kucha. Nilifanikiwa kupata nafasi ya kuegesha gari kwenye jengo la kuegeshea magari kwa bei ya kutwa nzima kwenye mtaa huo huo karibu na Taasisi ya Sanaa ya Illinois (Illinois Institute of Arts).

  Niliondoka hapo pole pole nikiwa nimebeba mkoba wangu uliokuwa na nyaraka mbalimbali na hotuba ambayo nilitakiwa niitoe mchana huo kwenye Maktaba ya Chicago. Nilitembea kwa kama dakika kumi hivi, pole pole huku nikivinjari watu na majengo na hatimaye nilifika Maktaba. Jengo la Maktaba ya Chicago lilikuwa kando kabisa ya mtaa maarufu kabisa wa Michigan ambao ndio mtaa mkuu jijini hapo. Jengo la Maktaba hiyo ni kubwa na kumbukumbu zinaonyesha kuwa mwaka 1991 jengo hilo liliingia katika rekodi za Guinness kama Jengo Kubwa zaidi la Maktaba ya Hadhara Duniani. Jengo hilo lina ghorofa tisa pamoja na ile ya ardhini. Niliingia ndani kwa taratibu huku nikiangalia picha na kazi nyingi za sanaa zilizotungikwa ukutani. Nilienda kwenye eneo la kuhudumia wateja na kujitambulisha kuwa nilikuwa hapo kwa ajili ya mkutano wa Wakutubi (librarians) wa kanda ya Kati Magharibi. Nilielekezwa kwenye ofisi ya Mkutubi Mkuu Msaidizi wa Maktaba hiyo ambaye ndiye mwenyeji wetu.

  Nilibisha hodi kwenye ofisi ya Mkutubi huyo na nilikaribishwa na dada mmoja mrefu na mwembaba wa wastani.

  Nilinyosha mkono wangu kumsalimia nikijitambulisha. Na yeye aliinuka kwenye kiti chake na kuja mbele ya meza yake na kunyosha mkono wake kujibu salamu yangu.

  “Naitwa Lisa DeJohn, Mkutubi hapa” Alisema huku akinikazia macho yake. Nilijua dada huyu si wa kuchezea kwani yuko kazini.

  “Naitwa M. M. Mwanakijiji, Mkutubi toka Maktaba ya Michigan, nafurahi kukutana nawe” Nilimjibu nikiutingisha mkono wake na kumwangushia tabasamu lililoonyesha meno yangu meupe yaliyopangiliwa vizuri.
   

  Attached Files:

 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  May 3, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Aaaah hii mbona ya zamani...nakumbuka kati ya 05 au 06 hii...toka enzi za Tanzatl....vipi huna mpya?
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  May 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  yeah.. this was in 2006.. mpya itakuja moja this week.. halafu the shabang inakuja kwa mchango!!!
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  May 3, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Mchango? you mean we have to pay for it?
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  May 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  si ndiyo!!! ama a bad idea?
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  May 3, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Oh no...it's a great idea....I just wasn't exactly sure what you meant by "mchango"..so I wanted to make sure. So you go 'head man....I'm not gonna knock your grind...go 'head and make that paper....
   
 7. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Cuzn hapo ni State street na Congress.....alafu nakusubiria next week cuzn.....nimeshaweka schedule tayari....
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  May 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  muhimu cuz.. !!
   
 9. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2016
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Tanzatl bado ipo Au ilifia wapi?
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Feb 23, 2016
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Ilishakufa zamani tu mbona....
   
 11. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2016
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mzee mwanakijiji kanogewa na Chi-town
   
 12. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2016
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  I see watu kumbe huwa mnaona mbali, hiki kizee magumashi ulishakibaini ni kipigaji tu six years back!!
   
 13. Bufa

  Bufa JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2016
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 4,167
  Likes Received: 3,371
  Trophy Points: 280
  O'Hare international airport ndiyo kiwanja nilichofikia mara ya kwanza naingia States miaka kadhaa nyuma, nilikua nacheka Cheka ka chizi huku nikishikwa na butwaa. Mwaka Jana majira ya joto pia nilifika tena kwenda kutazama game la Man untd vs PSG pale soldiers field.
   
 14. wambagusta

  wambagusta JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2016
  Joined: Nov 28, 2014
  Messages: 1,468
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Duh unajuwa!
   
 15. luckyline

  luckyline JF-Expert Member

  #15
  Feb 24, 2016
  Joined: Aug 29, 2014
  Messages: 8,512
  Likes Received: 4,035
  Trophy Points: 280
  Luckyline mara yangu ya kwanza kuingia jiji la lumumba dah nilitarajia kuona mengi ambayo sijawai ona chini ya dunia hii. Nilitarajia kukutana na watu wa high status kwenye jumba hilo cha kushangaza nakutana na wabeba box, wauza kofia ofcoz wengi wao walikuwa wamevalia sale zao. Nilienda huko ili nione vitu vipya na mm niwe wa kisasa maana nasikia uko mambo safi, bahati mbaya sikuona jipya bandugu safari yangu ilikuwa mbaya sikununua hata kitu cha kusimulia nikirudi huku tz bidhaa nilizokutana nazo ndo kama izo kofia, vitambaa, kanga na tishet. Sina hamu ya kurudi lumumba states.
   
 16. SPSS

  SPSS JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2016
  Joined: Feb 20, 2016
  Messages: 664
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 80
  nimeipenda
   
 17. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #17
  Mar 1, 2016
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Chi-town?
   
 18. falcon mombasa

  falcon mombasa JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2016
  Joined: Mar 5, 2015
  Messages: 7,744
  Likes Received: 4,770
  Trophy Points: 280
  Mi pia naupenda mji wa chicago with no reason
   
 19. falcon mombasa

  falcon mombasa JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2016
  Joined: Mar 5, 2015
  Messages: 7,744
  Likes Received: 4,770
  Trophy Points: 280
  Mi pia naupenda mji wa chicago with no reason
   
 20. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #20
  Apr 10, 2016
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Rudi rudi Mzee mwanakijiji
   
Loading...