Waswahili wa Marekani

Waswahili wa Marekani

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
23,240
Reaction score
33,850

View: https://youtu.be/8DNwD9U2mks

1784611859327.png


1784611712234.png

WASWAHILI WA MAREKANI

Huyu mwandishi Nathaniel Mathews tunafahamiana na kwa kiasi fulani alikuwa kama mwenyeji wangu nilipokwenda Northwestern University, Chicago.

Anazungumza Kiswahili vizuri na anakipenda muda wote tulipokuwa pamoja tukisema Kiswahili.
Jambo lililonishangaza ni kuwa kajifunza Kiswahili chuoni Marekani na alikuja Mombasa kukipiga msasa.

Ilikuwa tukiwa kwenye mall au restaurant jamaa zake wanashangaa kumsikia anazungumza na mie lugha ambayo wao hawaifahamu.

Hiki ndicho kitu kilinigusa sana katika vyuo vya Marekani.
Wengi wanasema lugha za kwetu, Lingala, Kizulu nk.

Alinishangaza Mkutubi mmoja alipokuwa akinitembeza kwenye maktaba yake Chuo Kikuu Cha Iowa kanionyesha CD zilizopo za taarab za Bi. Kidude akaniambia kazinunua yeye mwenyewe kwa mkono wake Kariakoo.

Huyo hapo juu Nathaniel Mathews kwenye picha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom