Nitapataje kidoti kama cha Jokate?

nipher 1

Member
Nov 25, 2016
6
4
Salaam wanajukwaa,

Kwa miaka mingi nimekuwa nikitamani kuwa na kadoti cha shavuni (kama kajiuvimbe). Nikimwangalia Jokate anapendezea sana na kale kakidoti kake.

Naomba wataalam wa maswala ya urembo kama kuna anayefahamu jinsi gani naweza kutengeneza kidoti.
 
Aiseeee! Vuta subira mrembo watakuja wajuzi kukupa 'suluhisho'..

Hebu niulize swali la kizushi: ile alama/uvimbe shavuni kwa Jokate ni 'beauty spot' au ni 'mole'.. Maana nahisi watu wanachanganya sana hivi vitu viwili na nahisi hata wewe unachanganya hiki kitu!! Unataka beauty spot au unataka mole???
 
Wala hata sio kazi katafute mzinga wa nyuki ama kichuguu cha manyigu wewe ingiza kichwa chako humo kwa nguvu halafu ufanye kama unachokonoa chokonoa kuwakera hao viumbe.

Watakung'ata, ukisikia maumivu usilie wala usijute ndio gharama ya urembo, baada ya hapo utajaa vidoti uso mzima, ikiwezekana hata shingoni hapo nadhani utakuwa umepata hicho kidoti unachotaka na nyongeza ya vingine kaa mia hivi.
 
Jamani nimecheka jamani looh siyo kwa ushauri huo.mkuu!!
 
Kweli tunatofautiana, nilikuwa navyo viwili na nilifanyiwa plastic surgery kuvitoa.
 
Mambo yenu ya kupenda kuiga hata visivyoigika ndo yanawapeleka kubaya hayo. Unadhani km ulimuona Jokate amependeza na wewe utakuwa hivyo? Km ingekuwa hivyo basi mbuzi naye angependeza km angevalishwa suti
 
Tafuta mavi ya mbuzi makavu weka kwenye kwenye sufuria na chemsha bila maji, kakichemka bas gandamiza kwenye sehem unayataka kakidot kawe.
Huku mtaani kwangu mademu zangu wameweka hizo dot kwenye mapaji yao mkabala na vitumbua vyao aisee wanapendezea kama nini
 
Kazaliwe upya,omba waumbaji wasisahau kukuwekea hicho kidoti(elekeza kabisa vizuri wasije kosea)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom