Nitamsaidia Humphrey Polepole kutaja wahuni(Hooligans) ambao sio tu hawakumalizwa bali waliongezeka awamu ya tano mara 100 zaidi

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
21,536
2,000
Mh Polepole naona anazunguka sana kuwataja majina na level zao wahuni ambao anadai Serikali ya Awamu ya Tano ilishindwa kumalizana nao.

Kwanza Polepole anakubali kuwa Wahuni hao ni wanachama wa CCM.

Pili Mh Polepole hakatai kuwa Wahuni hao (Hooligans) ni viongozi ndani ya chama na wengine wameshika nyazifa mbali mbali ndani ya serikali.

Mh Polepole anakubali kuwa hao wahuni ni watu walioaminiwa na wananchi wakapewa dhamana ya kuongoza.

Katika kipindi cha miaka 5-6 tumeshuhudia uhuni mwingi waliofanyiwa watanzania. Hasa chanzo kikiwa ni kutoka ndani na nje ya chama cha mapinduzi ambacho Polepole anakiri wahuni wako huko.

Sasa wahuni hawa Hapa. Polepole acha kuzunguka mbuyu. Hata wewe ni Mhuni. Hujamalizwa ile umekatwa mabega yalitaka kuzidi kichwa. Sasa ule uhuni umekutoka unaona wivu kwa wahuni waliobaki. Uhuni ni sifa ndani ya chama chenu kama ulivyofafanua.

1. Wahuni walidiriki kudanganya watanzania kuwa pesa za miradi ni za ndani kumbe walikuwa wakikopa kimya kimya na hatujui kama hizo pesa wahuni waliweka kwwnye miradi zote au zingine zilidondokea mifukoni mwa wahuni

2. 2019 Tanzania ilishuhudia vurugu (political hooligans) ikifanyika wakti wa uchaguzi wa serikali za mitaa. Ule ni uhuni wa karne.

3. Wahuni hawa walijaa kila kona ya nchi wakitembelea Noah Nyeusi na Nissani Nyeupe. Kiukweli yeyote aliyekutana nao hadi leo hajasahau kama hajfa basi kabaki na ulemavu wa kudumu. Wahuni wanatoka ccm kwa mujibu wa Polepole na wengine ni viongozi ngazi mbali mbali.

4. Wahuni wana tabia za kuharibu na kupora mali za waungwana. Kumbuka korosho za mtwara, Nyumba za kimara Dar es Salam na pesa za rambi rambi za Bukoba.

5. Polepole akiwa kiongozi wa wahuni anatuhumiwa kuendesha kampeni za kihuni za kununua na kuuza wabunge kutoka vyama mbali mbali vya siasa. Kama kawaida ya wahuni hawakununui kwa pesa tu bali kwa vitisho kutaka kukua, kukuharibia mali, kukuachia ulemavu na Kukufunga kwa kesi ngumu ngumu.

7. Wahuni sio watu wazuri. Wamebomoa mali za machinga.

8. Wahuni wanapenda politoical violence and intimidations. Mwaka 2020 oktoba ni mwaka wa shetani na mwaka wahuni. Wahuni hawa wanapenda kutumia nguvu za dola kuanzisha vurugu, unyama na utesaji. Kama tulivyoshuhudia uhuni wakti wa kampeni hadi uchaguzi watu waliunguziwa nyuma, kupigwa na kuuawa. Wahuni hawakumalizwa bali walitengenezwa na kuwa wengi zaidi.

9. Wahuni hawapendi kuleta huduma za jamii hutumia pesa nyingi kujilinda na kukandamiza wengine. Wakati tunakaribia uchaguzi huona wahuni wakiagiza magari mengi ya washa washa kuliko magari ya Kuhudumia wagonjwa Ambulamce. Mwaka 2014 pekee yaliagizwa magari 700.

10. Kwa mara ya kwnza ktk bara la afrika wahuni walizima internet Tanzania nzima na twitter tar 27 October. Wahuni hawapendi ukweli na uwazi. Matendo yao hupenda yafichwe yawe siri yasiongelewe.

11. Polepole wahuni mliwatengeneza sasa wamewageuka. Wewe na Bashiru ni miongoni mwa waathirika kutokana na vitendo vya wahuni.

Mnavuna mlichopanda. Na bado!!
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
21,536
2,000
Kule china Chini ya mwenyekiti wa chama Mr Mao hushirikiana na wahunk kwa karibu kunyamazisha raia wanaolalamika kuhusu kukosa haki za binadamu na huduma muhimu.

Ukionekana unalalamika unadunguliwa hata waandishi wa habari hula msoto wakiandika habari za malalamiko za wanachi.

Hapa kwetu tuliambiwa asisikike mtu anasema vyuma vimekaza atatiwa grisi.
 

Immortan joe

Senior Member
Nov 7, 2021
164
250
Hawa politician watazidi kutufanya wajinga sisi wadanganyika sijui had lini!

IMG_20211204_061051_407.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom