kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,418
- 7,206
Kwa nini wale Polepole kawaita wahuni hawafai uongozi nitatoa mfano wa TANESCO chini ya waziri wake kijana Januari.
Kuingia tu akaja na mipango kemkem TANESCO mmojawapo wa mipango ni huu wa kubadili mita za umeme kuweka za kisasa eti ukilipa tu sio tena unapewa token ukaingize mwenyewe kwenye mita. Ukisasa ni kwamba ukilipa tu mita yako moja kwa moja inajibu kwa kupokea na kuongeza units kwenye mita kiasi ulicholipia.
Mambo ya kujiuliza ni kwamba je kuna ulazima kuleta mpango huo kwa sasa ukizingatia shirika la TANESCO lilikua kwenye mkakati wa kujikwamua kutoka kupata hasara?
Je hiyo teknolojia ambayo pengine hata Ulaya bado ni mpya kuna haja ya nchi yetu kuikimbilia?
Halafu la msingi kubadili mita nchi nzima kwa bei ya hizo mita si itakua gharama kubwa sana kwa shirika linalopata hasara?
Kwa ufupi wahuni wanakujaga na mipango ya upigaji tu. Hapa tulipo kimaendeleo teknolojia ya mita tuliyonayo inatosheleza kabisa. Hakuna sababu kuingiza shirika gharama kubwa kwa tamaa binafsi ya mtu.
Watakwambia mita zitabadilishwa taratibu lakini sio kweli maana wauzaji hadi ununue ndio upate chako cha juu. Kwa hivyo tutashuhudia ubadhirifu mita nzima zinang'olewa na kubadilishwa.
Huu ni mfano mmoja tu jinsi wahuni hawawezi kuleta maendeleo ya nchi ila kuleta maendeleo yao binafsi na kujikita kudhibiti dola kwa faida yao.