Nitamng'oa Mnyika Ubungo - Juliana Shonza

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
Juliana Shonza aliyetimuliwa CHADEMA na kujiunga na CCM jana amelalamikia CHADEMA kuwa kuna mfumo dume na kwamba hakuna mwingine anayetoa kauli zaidi ya viongozi wa juu wa chama hicho.

Shonza alitumia fursa hiyo kumtumia salamu Mbunge wa Ubungo John Mnyika (CHADEMA) na kumtaka ajiandae kwa mapambano katika uchaguzi wa mwaka 2015.Shonza amesema mjini Dodoma kwamba mwaka huo ndiyo utaamua kati yake na Mnyika ni nani zaidi Ubungo

Akihojiwa na gazeti la Mwananchi Mbunge wa Ubungo John Mnyika amemtaka Shonza amuombe Mungu kwanza ili apitishwe na CCM kugombea na mengine yatafuatia.

Source:Tanzania Daima/Mwananchi.
 
Hakuna kilichofanyika kwenye jimbo la Ubungo zaidi ya kumuona mbunge wetu Mnyika akiruka sarakasi zake bungeni ambazo hazitusaidii chochote sisi wananchi.

Juliana Shonza atapata ubunge bila ya wasiwasi.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hahahah hata hajamaliza siku moja tayari kaanza kuropoka!!
Nani kamwambia atateuliwa kugombea ubunge jimbo la ubungo?!
Kama alikua hajui hili asubiri aone!
 
Juliana Shonza aliyetimuliwa Chadema na kujiunga na CCM jana amelalamikia CHADEMA kuwa kuna mfumo dume na kwamba hakuna mwingine anayetoa kauli zaidi ya viongozi wa juu wa chama hicho.

Shonza alitumia fursa hiyo kumtumia salamu Mbunge wa Ubungo John Mnyika (CHADEMA) na kumtaka ajiandae kwa mapambano katika uchaguzi wa mwaka 2015.Shonza amesema mjini Dodoma kwamba mwaka huo ndiyo utaamua kati yake na Mnyika ni nani zaidi Ubungo

Source:Tanzania Daima

By the way, kauli za chama zinatolewa na msemaji wa chama, weye alitaka kila mtu ajisemee? Kama ni kauli yako waweza jisemea, au kutoa maoni. Sasa basi fursa unayo, waweza endelea kujisemea utakavyo huko uliko.
 
Naamini hutakufa kabla ya kujiona ukiwa miongoni wa wapinzani wa serikali itakayoundwa na CDM itakavyokuwa inahudumia watanzania kwa Uadilifu, weledi na haki.
 
Kuna malengo mengine kwa kweli hata kama unayaweka inabidi uangalie uhalisia wa kuyafikia, ni sawa na mtu kutokuwa na uwezo wa kununua hata baiskeli halafu ukajiwekea lengo la kununua chopa. Lengo kama hili kwa huyo binti ni la juu sana na atafanikiwa tu endapo mshindi wa jimbo hilo atapatikana kwa kuchakachua na si kwa kura halisi.
 
CCM wameisha fanya kura za maoni tiyali na kumpitisha yeye kgombea kwa tiketi ya CCM? Huyu Dada ndo mwisho wake umefika, Hata Viti maalumu hawezi pata,
 
By the way, kauli za chama zinatolewa na msemaji wa chama, weye alitaka kila mtu ajisemee? Kama ni kauli yako waweza jisemea, au kutoa maoni. Sasa basi fursa unayo, waweza endelea kujisemea utakavyo huko uliko.
mwache aropoke na huko kisha akutane na Nape !!
 
Kwanza ni vizuri angejiuliza, CCM watampitisha awe mgombea wao wa Ubungo.
Jibu lipo wazi kabisa NEVER.
 
Juliana Shonza aliyetimuliwa Chadema na kujiunga na CCM jana amelalamikia CHADEMA kuwa kuna mfumo dume na kwamba hakuna mwingine anayetoa kauli zaidi ya viongozi wa juu wa chama hicho.

Shonza alitumia fursa hiyo kumtumia salamu Mbunge wa Ubungo John Mnyika (CHADEMA) na kumtaka ajiandae kwa mapambano katika uchaguzi wa mwaka 2015.Shonza amesema mjini Dodoma kwamba mwaka huo ndiyo utaamua kati yake na Mnyika ni nani zaidi Ubungo

Source:Tanzania Daima
safi sana mdada.
 
Labda anaijua Ubungo ya kwenye gazeti la Uhuru. Kwetu wakazi wa Ubungo hata umsimamishe Obama na Mnyika, lazima Obama arammbe mchanga! Awape salamu hizo na ma-dhaifu wenzie wanaompokea kwa mbwembwe mtu aliyefukuzwa kwa kuonekana hafai toka chama kingine.
 
Back
Top Bottom