Nitamng'oa Mnyika Ubungo - Juliana Shonza

Nitamng'oa Mnyika Ubungo - Juliana Shonza

Juliana Shonza aliyetimuliwa Chadema na kujiunga na CCM jana amelalamikia CHADEMA kuwa kuna mfumo dume na kwamba hakuna mwingine anayetoa kauli zaidi ya viongozi wa juu wa chama hicho.

Shonza alitumia fursa hiyo kumtumia salamu Mbunge wa Ubungo John Mnyika (CHADEMA) na kumtaka ajiandae kwa mapambano katika uchaguzi wa mwaka 2015.Shonza amesema mjini Dodoma kwamba mwaka huo ndiyo utaamua kati yake na Mnyika ni nani zaidi Ubungo

Source:Tanzania Daima

kama mtatiro alishindwa, huyo mjukuu ndo ashinde?
 
Hajawajua CCM vizuri, kuna watu ndani ya CCM wanapiga jaramba miaka nenda rudi hata kupewa nafasi ya kugombe uenyekiti wa mtaa hawajapewa sasa yeye kaingia jana tu anajangaza kugombea jimbo la Ubungo? Mbona Nape alishatangaza analitamani hilo jimbo? Na yeye analitaka? Amuulize Hawa Ng'umbi kilichompata hadi sasa hazungumzii tena Ubunge. Sijui au Jay Kaya jana kaonja joto la ka binti? Ndo akakaahidi hiyo chance!
 
Huyu mbona anakuja vibaya hivyo??? Anafikiri CCM unajiamulia tu ugombee wapi na unapita kama ilivyo CDM? CCM kuna demokrasia ya kweli, kuna mchakato wa kumpata mgombea, hamna udicteta wa CDM wa Mbowe au Slaa wa kuamua nani agombee wapi!!!!
 
To the extent she doesn't know completely appointment procedures in ccm, neither the way forward to compete with a

giant and intellectual man like Mnyika.

poor Shonza i real fee sorry for the ignorance you have shown so far.
 
Dah! magamba wameshamdanganya huyu binti mwenye ubongo mdogo.Vipi uenyekiti wa Bavicha hautaki tena,huyu kweli ni mfa maji.
 
Juliana Shonza aliyetimuliwa Chadema na kujiunga na CCM jana amelalamikia CHADEMA kuwa kuna mfumo dume na kwamba hakuna mwingine anayetoa kauli zaidi ya viongozi wa juu wa chama hicho.

Shonza alitumia fursa hiyo kumtumia salamu Mbunge wa Ubungo John Mnyika (CHADEMA) na kumtaka ajiandae kwa mapambano katika uchaguzi wa mwaka 2015.Shonza amesema mjini Dodoma kwamba mwaka huo ndiyo utaamua kati yake na Mnyika ni nani zaidi Ubungo

Source:Tanzania Daima

Mapovu tupu haya! Kwanza hata hiyo nafasi ya kugombea ataipata wapi? Namuonea huruma sana huyu msichana anatapa tapa mno. Ccm haiwezi kumsimamisha yeye ubungo wakati kuna vijana lukuki ambao wamekuwa kwenye chama siku zote bila kuhama hama na wanaitaka hiyo nafasi ya kugombea japo wana uhakika wa kushindwa. Namshauri juliana atafute kazi ya kuajiriwa siasa hawezi atakufa maskini. Poleeeee
 
Hakuna kilichofanyika kwenye jimbo la Ubungo zaidi ya kumuona mbunge wetu Mnyika akiruka sarakasi zake bungeni ambazo hazitusaidii chochote sisi wananchi.

Juliana Shonza atapata ubunge bila ya wasiwasi.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Aaah! Hakuna kilichofanyika sio. Unam'mis keenja nn? Alifanya makubwa ikiwemo kutohudhuria hadi vikao vya bunge na kutoonekana jimboni. Kweli kazi ya kichwa ni kufugia nywele.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Juliana Shonza acha kujitekenya mwenyewe na kisha kucheka mwenyewe!!! Kwanza CCM wanakuchekea wewe kwa sababu tu wananakuona ni mtu wa muhimu saizi lakini ikikaribia 2015 umaana wenu utapungua na hivyo kukosa nafasi zote ambazo mnatarajia kugombea.

Hebu nemba web ya CCM kaangalie utajuta msemo CCM ina wenyewe, je wewe ni mionhoni mwao???

Hata hivyo, huna ubavu wa kumtumia Mnyika salamu na ukamtisha. Mnyika hata kama akigombea na mwanaCCM yoyote Ubungo bila fitna ni lazima ile kwenu!!
 
Last edited by a moderator:
Kweli njaa imehamia kichwani,dada pumzika kwa amani.
 
Back
Top Bottom