Nitakuwa nakosea?

Hakuna magonjwa ya kurithi wala kubwa lolote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani nimewaza sanaa..mwisho nkasema shida zangu zinanitosha
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani kwamba sitopendwa kwa matatizo yangu..je nahitaji kumpenda mtu kwa matatizo yake?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni wangapi hawakupendi kwa matatizo yako, au unataka tu kuumiza wengine wasio na hatia kwasababu ya mtu mmoja aliyekukacha wakati unamatatizo, na huoni kuwa hata nafsi yako itakuwa inakusuta kuona unaumiza mtu ambaye hana habari kwamba uliwahi kukachwa wakati unapitia magumu?

Cha muhimu tu hapa nakuomba mdogo wangu uwe makini wakati unaanzisha mahusiano mapya, wapo wenye mapenzi ya kweli japo ni ngumu kubaini yupi wa kweli yupi ni mwongo kwasababu wanjajanja pia hukaa macho juu juu kuvizia mipira iliyokufa ili wabutue maana kwenye msafara wa mamba mikenge hukaa humo humo.

Pole kwa matatizo mdogo wangu, siyo kila siku ni ijamaa kwahiyo kubali kuwa hii imeshatokea na maisha yanaendelea, ipo siku isiyo na jina atatokea mfalme wa moyo wako na uta-enjoy sana tu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo lenyewe ni dogo sana..we kuumia mguu tu unaacha?

Sent using Jamii Forums mobile app

Huyo ni dhaifu zaidi ya bunge la JMT, yani kuumia mguu ndo amekukimbia...!! Yani watu hatuna miguu na bado tunapendwa,, mwache aende aisee, nani alimwambia yeye atakufa akiwa na macho au miguu au chochote kile kingali kizima?

Amesahau msemo mmoja unasema HUJAFA...........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana..ntafiata ushauri wako
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani hayajui maisha wala hajapeviuka sawaaawa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…