Majigo
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 5,519
- 1,831
- Thread starter
- #81
29--Unamjua? Sabina aliniuliza.
Eeh, si Samweli yule.
Si nilikueleza, Shija kila kitu nilichokueleza kina ukweli, nilipoamua kuusema ukweli wa wachawi nilijitoa mhanga wa uhai wangu. Kama wakijua nimekueleza haya ujue lazima nitapoteza maisha yangu
Sabina, nina siri nzito moyoni mwangu hivyo usihofu kitu, nitailinda mpaka mwisho wa uhai wangu.
Ni kweli lakini nina wasiwasi na baba yako kutokana na mabadiliko yako.
Sabina we nione hivi siwezi kutoa chochote ulichonieleza na kunionesha.
Wakati huo tulikuwa bado tumo ndani ya maji ya mabega, kuogelea nilikuwa najua lakini wasiwasi wangu mazingira yalikuwa yakinitisha sana hasa baada ya kiza kutukutia kwenye maji huku yakizidi kuwa baridi. Muda wote sikumuona kaka yangu, nilijiuliza kwa nini nilikuwa simwoni.
Mbona simuoni?
Hata mimi nashangaa lakini yupo.
Sabina usiku unaingia nasikia sehemu hizi zina viboko tunaweza kudhurika.Shija acha woga, hebu nisubiri nikamuangalie.
Sabina alitoka nje ya maji na kuelekea eneo lililokuwa na ngombe wengi, aliingia ndani ya kundi lile la ngombe. Nilibakia kwenye maji peke yangu huku baridi ikizidi kunipiga. Nilijikuta nikiingiwa na wasiwasi baada ya Sabina kuchelewa kurudi. Nilijikuta najiuliza kama asingerudi nigefanya nini. Kurudi njia tuliyoijia nisingeweza kuitambua kutokana na eneo lake kuwa la hatari hasa muda ule wa kiza kuanza kuingia. Kwenda mbele niliogopa kutokana na kuwepo kundi la ngombe bila kujua usalama wake ulikuwa vipi.
Nilibakia nimeganda kwenye maji huku nikimuomba Mungu ashushe miujiza yake. Baada ya muda Sabina alitokea kwenye kundi la ngombe na kusogea karibu na maji, alinionesha ishara ya mkono nitoke ndani ya maji nimfuate. Nilifanya vile kwa kusogea pembeni ya ziwa na kutoka ndani ya maji kumfuata alipokuwa amesimama. Alinishika mkono na kunipitisha katikati ya kundi la ngombe. Nilimfuata nyuma hadi tulipowavuka wale ngombe na kuingia kwenye mashamba ya mpunga kisha kuelekea kwenye makazi ya watu.
Nilichoshukuru ni kwamba giza lilikuwa limeanza kuingia, hivyo kutoka kwetu na nguo zetu na maji hakuna aliyetuona. Nilishangaa kufika mapema barabarani na kuona kumbe kulikuwa na njia ya karibu kuliko kuzunguka njia ya hatari kama ile. Kingine ni kwamba mpaka tunaondoka eneo la ziwani sikumuona kaka yangu.
Sabina mbona tumepita mbali kumbe kulikuwa na njia fupi?
Shija nilikuwa na maana yangu tusingeweza kuja moja kwa moja tungeweza kuonekana na wao kutufuatilia na wangejua umewatambua usiku wa leo usingelala.
Sasa mbona tumerudi na njia hii?
Sasa hivi wameisha ondoka. Na kaka yangu mbona sikumuona?
Hata mimi nashangaa, lakini mara nyingi huwa huku lakini nitamuuliza Helena.
Tulivuka barabara na kuanza kuitafuta njia ya kurudi nyumbani, kama kawaida niliingia nyumbani muda ukiwa umekwenda. Siku hiyo baba hakunivumilia alinichapa sana na kutaka kujua nilikwenda wapi. Nilimdanganya kwamba nilikwenda kucheza mechi kijiji cha mbali kidogo. Alinipa onyo kali la kuwahi kurudi nyumbani na kwamba kila nikitoka shule lazima nirudi nyumbani.
Niliona kwa onyo lile lazima baba angeniona mkaidi na sina adabu kutokana na ukweli kwamba harakati zangu na Sabina zilikuwa zikifanyika jioni.
Siku ile nililala salama mpaka siku ya pili. Asubuhi kama kawaida baba aliniamsha kuwahi shule, kama ilivyokuwa ada yangu nilinawa kisha nilipitia vitu muhimu vya shule na kuwahi namba ambapo njiani kama siku zote nilikutana na Sabina.
Za asubuhi Shija.
Nzuri kiasi.
Kivipi? Nilimuelezea yaliyonikuta jana yake na onyo kali nililopewa na baba.
Sabina alinionea huruma lakini wasiwasi wake mkubwa ulikuwa ni mimi kuitoa siri hiyo nje.
Pole sana mpenzi wangu, lakini hukumweleza ukweli? Sabina niamini mpaka nakufa siri hii itabakia moyoni mwangu.
Asante sana Shija naamini kuwa na wewe ni chaguo langu sahihi.
Hata mimi kuwa na wewe ni chaguo langu sahihi.
Tilicheka na kugongeana mikono huku tukielekea shule, tulipokaribia shule Sabina aliliita jina langu na kunigeukia, kitu kilichonifanya nisimame.
Basi jana nilipofika nyumbani nilikwenda hadi kwa kina Helena kumwulizia kaka yako
Mmh!
Kumbe jana hakwenda kuchunga kutokana na kuamka anaumwa!
Unataka kuniambia hata ndondocha wanaumwa ?
Kwa nini wasiumwe ? Kwani wale ni binaadamu kama binadamu wengine, sema wanaishi katika mazingira ya kichawi tu.
Na wanakufa ?
Kila kinachomtokea mwanadamu nao huwatokea.
Sasa wakifa mnawafanya nini?
Wanaliwa nyama!
Mmh, niliguna.
Shija kuna kitu nilikuwa nakifikiria leo
Kipi?
Nilikuwa na wazo la mimi kujifanya naumwa ili na wewe unisindikize kisha tukishatoka maeneo ya shule twende kwa kina Helena
Kufanya nini?
Nikakuoneshe kaka yako. Utawezaje na wenyewe
wapo?
Inaendelea...