Majigo
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 5,519
- 1,831
- Thread starter
- #21
9--Nilihamishia mawazo yangu shule kuwaza masomo hasa somo la jiografia ambalo jana yake nilikosa maswali mengi tofauti na nilivyojiamini kwa kuyaona maswali mepesi. Sikutaka kuumiza akili yangu kuwaza nilioyaona na kukutana nayo, kwani niliamini hata kama nisingekatazwa bado hakuna mtu angeniamini na kuniona mtu niliyekuwa nikiona ndoto na vitu visivyo na ukweli. Kingine nilichokiogopa ni kuonekana mchawi wa ukweli kuyasema mambo ya usiku watu wamelala.
Nilitembea kwa mwendo wa kawaida kwa kuamini bado sijachelewa kutokana na wanafunzi wengi kuonekana kutembea bila wasiwasi wowote . Nilipokaribia uwanja wa shule nilianza kusikia mlio wa ngoma niliyoisikia usiku iliyokuwa ikipigwa palepale uwanjani. Lakini nilipokaribia sauti ile ilipotea akilini taratibu na mwisho wake ilipotea kabisa.
Nilifanikiwa kuwahi namba, baada ya kuhesabu namba nilikwenda kwenye eneo langu kufanya usafi na kumwagilia maua. Baada ya usafi ilipigwa kengele na wanafunzi wote tulikusanyika kwa ajili ya usafi, baada ya usafi muda wa kuingia darasani ulipofika tuliingia madarasani. Nilipoingia darasani nilikwenda kukaa kwenye dawati langu. Dawati nililokuwa nakaa lilikuwa la wanafunzi wawili . Kutokana na uwezo wangu darasani, katika dawati nilikuwa nakaa na mtoto wa mwalimu mkuu wa kike. Japo hakuwa na akili sana lakini tulisaidiana japo sehemu kubwa ya masomo alinitegemea mimi.
Ajabu ilikuwa baada ya mwalimu kuingia darasani, tulimsalimia vizuri kama kawaida alituruhusu tukae chini . Baada ya kukaa chini mwalimu wakati anaanza kufundisha somo lake, nilipitiwa na usingizi mzito uliopelekea niote yote niliyoyaota jana yake baada ya kurudi kutoka shuleni baada ya kuamka muda usio wa kawaida. Ilikuwa ndoto nyingine iliyonipeleka tena kwenye ngoma ya wachawi , ilikuwa ajabu ile ngoma haikuwa tena kwenye uwanja wa shule. Ilikuwa chini ya mti mkubwa, ngoma ilikuwa imepamba moto kila mtu kucheza anavyojua . Watu walikimbia na fisi na wengine kupaa na kutua na ungo.
Mara moja sikujua sherehe ile inahusu nini kwa wachawi kufurahi namna ile, kitu kingine kilichonishtua kwenye njozi yangu ilikuwa kumuona mmoja wa walimu wetu naye akiwa anacheza ngoma ile huku vumbi likiwa kubwa sana. Kutokana na vumbi kubwa kutimka nilijikuta nikiingiwa na vumbi mdomoni na puani na kusababisha nikohoe mfululizo. Kumbe kukohoa kwangu ndiko kulikowashtua wanafunzi na mwalimu darasani kuwa nimelala, hata mwalimu alipokuja bado nilikuwa nimelala sijitambui. Kila walivyoniita sikuweza kuwasikia , nililala juu ya dawati huku nikiendelea kukohoa sana. Walinichukua na kunitoa nje na kuniweka chini ya mti wenye hewa. Mwalimu aliwaeleza wanafunzi waliokuwa wamepagawa na hali yangu, waniache nipigwe na upepo huku akiwekwa msichana mmoja pembeni yangu aniangalie.
Itaendelea...