Majigo
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 5,519
- 1,831
- Thread starter
- #101
37--Sasa itakuwaje? niliuliza. Hatuna jinsi, tuingie tu kwenye mvua tukiisubiri mpaka ikatike lazima watatupata, wametumia mvua ili kutuzuia tusifike mbali, alisema Sabina huku akifuta maji usoni, kauli ile ilinivunja nguvu na kuona lazima nitakuwa katika wakati mgumu maishani mwangu kwa kuharibu kila sehemu. Nilikumbuka maneno ya mzee Manoni kwamba Sabina na Helena ni watoto tu hawawezi kitu chochote.
Kila dakika mvua ilizidi kuongezeka ukali wa manyunyu yake ulifikia hatua ambapo matone yake yakimpiga mtu mwilini unahisi maumivu. Tulikubaliana kutembea na ile mvua kuelekea barabara kuu ambapo hakika ilinitia hofu kuhusu usalama wetu.
Ukali wa mvua ulitufanya tusione tunapokwenda kutokana kunyesha kwa nguvu. Baada ya kuona kila hatua ilikuwa ni lazima mtu aanguke kwenye maji, tulikubaliana tusimame sehemu tusubiri mvua ikatike. Lakini Helena aligoma kwa kuamini tukisimama sehemu watu waliokuwa wanatufuata wangetukuta.
Nilijiuliza watu hao wangetukuta wapi? Na kama walikuwa wametugundua niliamini hatukuwa na ujanja wa kufika popote kabla hawajatukamata. Tulikubali kuendelea na safari kwa shida huku mvua ikizidi kutunyeshea na kutufanya tuhisi maumivu makali. Tuliendelea mbele na kiza nacho kilizidi kutuchanganya.
Kilichotokea muda ule sikuwahi kukiona katika maisha yangu. Mvua ilikuwa kali iliyoambatana na upepo mkali, na kiza kizito kilichokuwa hakielezeki kwa maneno. Nilitamani kulia lakini ajabu Sabina na Helena walikuwa mstari wa mbele kuhakikisha tunaushinda mtihani ule. Niliamini maisha yetu yalikuwa kwenye hatari, lakini Sabina na Helena walionesha ujasiri muda wote kumnyanyua kaka kila alipoanguka.
Kuna kipindi tulitumbukia kwenye shimo na kutoka bila kujua tulikuwa tunaelekea wapi, akili yangu ilinionesha kabisa tumeishakosea njia kutokana na kutembea muda mrefu kwenye mvua bila kufika. Jamani hatujapotea? niliuliza. Shija si suala la kuuliza hii ni vita tujitahidi tu tutashinda, Sabina alisema. Hatuna jinsi twendeni tu mpaka tujue mwisho wake, Helena alisema kwa msisitizo. Na kweli tukikosea leo tumeharibu kila kitu, Sabina aliongezea.
Maneno yale yalinivunja nguvu na kuona tumeishauvaa mkenge kwa kuamini ubishi wa kina Sabina ndio uliotufikisha pale. Tuliendelea kutembea kwenye mvua kwa kuanguka na kunyanyuka . Kaka alikuwa amechoka kiasi cha kumshika na kumburuza kwa kutembelea magoti. Jamani niacheni mimi nimechoka, kaka alilalamika. Luhemeja mateso yote haya ni kwa ajili yako jikaze, tunaweza kufika sehemu tukapona, Helena alimueleza kaka ambaye alikuwa hoi kwa safari isiyo na mwisho
. Si yeye hata mimi niliona aibu kusema nimechoka kwa vile kazi ile ilinihusu mimi. Niliuweka mkono wa kaka mabegani kwangu na kuanza kwenda naye huku mvua ikizidi kuwa kali sana, mbele kiza kilikuwa kizito cha kutisha. Baada ya mwendo mfupi tulishtukia wote wanne tukiangukia kwenye mto uliokuwa ukipeleka maji kwa kasi.
Kila mmoja alipiga kelele kutetea nafsi yake. Kasi ya yale maji yalitupeleka kwa kutuburuza bila kujitetea. Kitu kibaya zaidi ni kwamba kulikuwa na kiza kizito ambacho kilitufanya tusione sehemu ya kuweza kujitetea kuyaokoa maisha yetu. Nikiwa napelekwa na maji nilimuomba Mungu aipokee roho yangu kwani sikuwa nafanya jambo isipokuwa kumtetea kaka yangu aliyekuwa mzima lakini akiishi maisha ya wafu.
Ghafla nilihisi kupigwa na kitu kizito kichwani kilichonifanya nipoteze fahamu. Kilichoendelea sikukijua. Niliposhtuka nilijikuta nimefungwa chini ya mti mkubwa, sehemu ambayo wachawi hufanya mkutano wao. Sehemu hiyo haikuwa ngeni kwangu kwani niliishawahi kufika katika sherehe ya wachawi kwa njia ya ndoto iliyokuwa na ukweli .
Pembeni yangu walikuwepo Sabina na Helena ambao nao walifungwa kama mimi. Chini alikuwa amelala kaka yangu akiwa amefungwa kamba huku akiwa amepigiliwa msumari mkubwa katikati ya kichwa na mwingine pembeni ya kichwa. Ilionesha kaka yangu alikuwa amekufa, na alikuwa katika vazi lile lile nililomchukulia nyumbani na kumvisha.
Moyo uliniuma nikijua na mimi muda si mrefu nitamfuata kaka yangu, ila sikuamini kama Sabina na Helena nao wangenifuata nyuma yangu. Bado Sabina na Helena walinitia moyo hawakuonesha kutishika na adhabu ile. Mara lilitokea kundi la wachawi wakiwa wanatoka makaburini ambako walipata miili miwili ya watu ambayo siku hiyo ingeliwa nyama.
Walikuja huku wakiwa wamebeba maiti za watu wawili waliokuwa kwenye sanda ambayo ilionekana mpya. Baada ya kuitua pale, mkuu wa wachawi mzee Manoni alisema: Nafikiri kazi imekwenda vizuri, ila kuna nyama imeongezeka kutokana na kiburi cha kitoto, mzee Manoni alisema huku akinigeukia na kunitazama kwa muda kisha alisema: Shija nilikueleza usiingilie nguvu za watu utapotea sasa ona umesababisha kaka yako kugeuzwa kitoweo usiku huu.
Kwa nini na yeye asiliwe? mchawi mmoja aliuliza. Shija hana kosa, hajui lolote kuhusu uchawi bali watoto wenu. Lakini ameisha ua siri zetu lazima tumgeuze asusa leo, mwingine alichangia. Bado hiyo haitoshi, wa kulaumiwa ni watoto wenu, Shija namjua vizuri.
Kwa hiyo na yeye ageuzwe msukule, kauli ile ilinivunja nguvu na kujua Shija mimi nimekwisha. Hapana huyu haguswi na kitu chochote ila nataka akitoka hapa atoke akijua kaka yake hayupo tena wala asisumbuke kumtafuta. Leo atamshuhudia akiliwa nyama pamoja na maiti nyingine tulizo pata leo. Baada ya kusema vile walimchukua kaka na kuanza kumkata vipande ambavyo waligawiana na kuanza kumla mbele yangu. Maumivu yalikuwa makali kuliko siku aliyokufa kwa kiini macho. Baada ya kumaliza kumla kaka yangu huku wakicheza ngoma, waligawana na maiti zingine mbili ambazo zilikuwa zimelazwa.
Baada ya zoezi lile, nilifunguliwa pamoja na wenzangu Sabina na Helena na kupewa onyo zito. Shija leo itakuwa mwisho wangu wa kukutetea tena, ukifanya chochote kinyume na ninavyokueleza utayamaliza mwenyewe . Haya arudishwe kwao ili wazazi wake asubuhi wamkute chumbani kwake . Baada ya kusema vile nilihisi kizunguzungu na usingizi mzito ulinipitia palepale nilipokuwa nimefungwa kamba, kilichoendelea sikujua
Inaendelea...