26--Ni kweli.
Tatizo nini?
Mawazo.
Ya nini tena?
Kwa yote uliyonieleza jana. Shija utaharibu kila kitu, kukueleza umekuwa hivyo je, ukiona itakuwaje?
Sidhani kuna mtu atahoji kwa nini sikulala.
Basi pole sana.
Asante, vipi umeleta? nilimwuliza.
Nimeleta, lakini utaweza? Unanitia wasiwasi . Nitaweza, nilimhakikishia.
Shija usifanye vituko darasani mwalimu akikugundua vita yenu itakuwa kubwa na pengine kuniponza mimi.
Nitajitahidi nina imani nitaweza.
Mmh, haya.
Tulikuwa ndiyo tunaingia eneo la shule na kengele ya namba iligongwa, tulikimbilia kuhesabu namba kisha kila mmoja alielekea kwenye eneo lake kufanya usafi.
Baada ya usafi kengele ya msitarini ili iligongwa, tulijumuika pamoja. Wakati tunaelekea mstarini Sabina alinifuata na kunipa kikaratasi kidogo na kunieleza kwa sauti ya chini.
Ndani kuna unga mweupe, paka kidogo chini ya macho yote utaona ya kuyaona.
Sikumjibu nilipokea na kukimbilia msitarini, baada ya ukaguzi tuliingia darasani.
Kama kawaida walimu waliingia kwenye vipindi, kipindi cha mwalimu Vene kilikuwa cha tatu cha saa tatu na dakika ishirini mpaka saa nne wakati wa mapumziko.
Kama kawaida aliingia darasani kwa macho yangu nilimuona amevaa nguo, nilimuona Sabina akinitazama. Nilijifanya simuoni, nilitulia kama hakuna kitu chochote. Kutokana na hofu yangu sikutaka kuiweka haraka kwa kuhofia kugundulika. Baada ya kuandika na kutuachia kazi, wakati anajiandaa kutoka kwa kutuambia tukusanye daftari, niliutoa ule unga uliokuwa kwenye karatasi na kujipaka kidogo chini ya macho.
Mmh, kweli ukishangaa ya Musa utayaona ya Firauni, sikuamini niliyoyaona mbele yangu. Kama isingekuwa kujipaka dawa na kuelezwa nitakayoyaona ningepiga kelele.
Mwalimu Vene alikuwa kama alivyozaliwa mkono wa kushoto alikuwa amejifunga hirizi kubwa nyeusi, mkononi alikuwa ameshikilia kitu kama kidole cha mtu. Shingoni alikuwa na kamba iliyokuwa imebeba kichwa cha mtoto mdogo.
Moyo ulitetemeka na hofu ilinijaa, nilimuomba Mungu kimoyomoyo mwalimu aondoke mapema. Wasiwasi wangu Sabina aliuona na yeye nilimuona akiingiwa wasiwasi , pengine alidhani naweza kupiga kelele za mshtuko au mwalimu Vene kugundua nimemjua yupo uchi. Ili kukwepana na kile kilichokuwa mbele yangu, sikuangalia mbele tena mpaka mwalimu alipotoka. Kengele ya mapumziko ndiyo iliyoniokoa, baada ya kutoka nilihisi kichwa kizito, nilichoshukuru Sabina muda wote alikuwa karibu yangu kufuatilia kila kilichokifanya .Wakati wanafunzi wote wanatoka alikuja na kuniuliza. Vipi Shija?
Kichwa, nilimjibu huku nikishika mkono kichwani.
Vipi umeona?
Ndi..yo..o..o.
Pole sana, kanawe na maji utarudi katika hali ya kawaida.
Kaniletee, naweza kukutana naye nje.
Si nilikuambia sasa unamuogopa.
Hapana hii kufuru.
Shija vipo vitu vingi utaviona yataka uwe na moyo mgumu.
Mmh, kweli yataka moyo wa ujasiri.
Sabina alinifuatia maji na kunawa uso, baada ya kunawa nilirudi kwenye hali ya kawaida. Pamoja na kurudiwa na hali ya kawaida, bado mazingira ya shule sikuyaelewa .
Nilikwenda kuomba ruhusa kurudi nyumbani kusingizia naumwa, kwa vile haikuwa tabia yangu waliniruhusu. Sabina alijitolea kunisindikiza japo wanafunzi walimwita wifi na wengine shemeji.
Nilijua nini alichokifanya Sabina alinisindikiza hadi nyumbani.
Njiani aliniuliza ninavyojisikia .
Vipi Shija unajisikiaje?
Hata sijielewi.
Si nilikuambia?
Ni kweli, lakini ni mshtuko tu kwa leo nisingeweza kusoma tena labda kesho.
Basi kuna dawa nitakuletea ukiinywa itakutia ujasiri kila kitu atakachokiona utakiona cha kawaida.
Sitakupeleka kwa kaka yako mpaka nikupatie hiyo dawa. Nitashukuru.
Wacha nikufuatie sasa hivi kwa vile wazazi wapo shamba.
Sabina aliondoka na kuniacha nikiwa nimejipumzisha na yeye kukimbia kwao, baada ya robo saa alirudi.
Alikuwa na dawa nyeusi ya unga ambayo niliikoroga kwenye maji na kuinywa kisha alinipa kipande kidogo cha ngozi sikujua ya mnyama gani ambayo alinieleza hata yeye hakujua ni ya mnyama gani.
Shija ameanza kufumbuliwa mambo kwa kuona na macho nini kitakacho mtokea? Kuyajua yote
Husiondoke Tafadhari.....