Majigo
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 5,519
- 1,831
- Thread starter
- #201
72--Niliendelea kutii amri na kumfuata kwa nyuma kila kona aliyopita kwa kuvuka milima na mabonde. Muda ulionyesha ni alfajiri kutokana na nuru hafifu kuitawala anga huku baridi kali ikiendelea kunipiga.
Baada ya mwendo usiopungua saa mbili tulifika kwenye kijito, hapo Helena aliniamuru nioge kwa sabuni aliyokuwa nayo. Maji yalikuwa ya baridi sana, nilihisi kama damu inataka kuganda mwilini.
Nilipomaliza kuoga, alinipa dawa ya unga kulamba. Baada ya kulamba nilijiona mwepesi kuliko kawaida na kujiona nipo dunia mpya na mimi mtu kwenye watu.
Shija unajikiaje? Helena aliniuliza. Yaani nauona mwili mwepesi kama nimevuliwa kitu kizito nilichokuwa natembea nacho mwilini. Pia nimeona vitu vingi ambayo toka niingie ndani sikuwa kuviona, inaonesha nipo dunia ile niliyoizoea miaka mingi iliyopita na vile vile napata hewa safi ambayo ni nyepesi puani kwangu tofauti na mwanzo,
ilikuwa ajabu ya mwaka baada ya kulamba dawa nilijiona nimeingia dunia mpya.
Baada ya kuona tofauti ya mwanzo na muda ule nilipolamba dawa, Helena alitoa dawa nyingine na kuanza kunisugua baadhi ya sehemu za mwili wangu. Helena kufanya hivi unamaanisha nini? Hapa nafuta chale za kichawi ambazo huwa kama muhuri wa kutambulika popote kuwa wewe ni mtu wao.
Baada ya hapa inakuwaje? Shija mpaka sasa upo katika dunia uliyoizoea na hapa tupo maeneo ya Kahangara. Kahangara ya Magu? Ndiyo. Usiniambie Helena! Nilishtuka nisiamini.
Kweli? Ina maana tayari umenitoa kwenye dunia ya wafu? Ndiyo Shija. Siamini. Kweli. Hawawezi kutukamata? Hawawezi . Siamini! Nimetoka kwenye umsukule. Amini sasa hivi wewe si msukule tena. Helena kweli?
Bado sikuamini niliona kama ananifurahisha kwa kitu kisichowezekana . Kweli kabisa Shija. Yaani dunia naiona mpya bila kunieleza hapa wapi wala nisingepajua. Kweli, inaonekana kukaa ndani muda mrefu umeanza kusahau vitu vingi. Siamini kama kweli mimi si msukule sasa? Amini, sasa hivi tuna kazi ya kujipanga kufika kwenu na mtu yeyote asikutambue.
Si umesema nisirudi nyumbani? Ndiyo, hii safari kwa mjomba wako. Tutafikaje? Nitakutanda khanga uonekane mwanamke, nilitaka nikuache uende peke yako lakini wasiwasi wangu unaweza kupotea na kuwa kituko kwa watu.
Nitakupeleka mpaka kwa mjomba wako ukiifahamu nyumba mimi nitarudi. Kwa nini usiingie ndani? Kumbuka hii ni siri yetu wawili , hatakiwi mtu yeyote kuijua. Helena mama yako yupo wapi? Mmh! Amesafiri na baadhi ya wachawi wenzake.
Wamekwenda wapi? Wamekwenda kwenye mkutano mkuu wa wachawi Sumbawanga. Mmh! Mkutano huo unachukua siku ngapi? Siku mbili. Tokea lini? Jana usiku na leo. Asiponikuta itakuwaje? Hawezi kunifanya lolote. Si atanitafuta? Atakupata wapi?
Chale nilizokufuta zitamfanya asikuone tena, labda mkutane kawaida lakini kichawi hawezi kukuona.
Tutakwenda Mwanza kwa miguu? Hapana, tutapanda basi.
Nauli unayo? Shija mpango huu nimeupanga muda mrefu kwa hiyo kwa hilo usiwe na wasiwasi . Siamini mpaka nikutane na mjomba. Shija naomba uniamini sitaki tena maswali ya kijunga, Helena alichoshwa na maswali yangu ya kijinga. Samahani Helena kama nimekuudhi.
Maswali gani kila nikikueleza unielewi? Najua nitakuudhi lakini bado naona kama ndoto. Pole Shija, samahani kwa kukukaripia, lakini sasa hivi kama mfungwa upo huru labda ufungwe kwa kosa lingine. Barabara ya kuelekea Mwanza iko wapi?
Ni mwendo kidogo, tufanye tuondoke eneo hili kabla wanakijiji hawajaanza kupita kwenda kwenye kilimo. Helena alifungua mfuko wa plastiki na kutoa kaptura na fulana ambavyo alinipa nivae na kuzitupa za zamani.
Baada ya kubadili nguo, alinipa khanga mbili, moja nilijifunga chini na nyingine nilijitanda juu na kuwa kama mwanamke. Helena alifanya vile vile kisha tuliondoka eneo lile la mto na kufuata njia aliyokuwa akiijua Helena kuelekea barabarani.
Ni kweli Helena amefanikiwa kumtoa Shija kwenye umsukule?
ITAENDELEA BAADAYE kidogo.....