Nitakufa Mara Ya Pili

Nitakufa Mara Ya Pili

Hizi stori, sitafuatilia tena maana nimekuwa teja toka kwa mjeda na my wit wake.

Hapa waweza limwa memo

Tuwe pamoja kiongozi
Nakutegemea hata kwa stori tam na kusisimua
Ijayo baada ya hii Mungu Akijaalia!
 
Kaka asante sana.Daa my three days have gone well.Thanx once again.
 
Mkuu Majigo umeniacha na maswali mengi, an anyway, nachukulia kama stori tu, ngumu kumesa kwa kweli!

Kwa hiyo hujawahi kwenda kwenu tena? Mama Helena na Helena na Sabina wanaendeleaje?
 
Last edited by a moderator:
74---Nilitembea taratibu kuelekea nyumbani kwa mjomba, muda ulionesha bado asubuhi kwani hata mlango ulikuwa haujafunguliwa.
Kabla ya kugonga nilijifikiria nizivue zile khanga au niingie nazo vilevile . Niliamua kuingia na khanga zangu ili wasishtuke mapema.

Siku hiyo nilichukuliwa na kupelekwa kwenye kanisani kufanyiwa maombezi kwa utukufu wa Mungu kuonesha jinsi nguvu zake zinavyoweza kuushinda uchawi.

Mjomba alitaka kunipeleka nyumbani, nilimweleza masharti niliopewa na mtu aliyenitoa kule kuwa nisirudi tena kijijini.

Mjomba alikubaliana na mimi nibakie kwake , wazazi wangu walifuatwa , hawakuamini lakini niliwaeleza ilivyokuwa na kukubaliana na mimi, ilikuwa furaha isiyo kifani.

Baada ya muda niligundua kumbe niliishi maisha ya umsukule kwa mwaka mmoja na miezi sita.
Mjomba alinitafutia shule ambayo nilisoma kwa miaka miwili na kufanya mtihani wa kidato cha nne.

Majibu yalikuwa mazuri kwa kupata ‘division two’ iliyoniwezesha kuingia kidato cha tano mpaka chuo kikuu

NAMSHUKURU MUNGU, NA NYOTE GUEST NA MAMBER WENZANGU WA JAMII FORUMS
MLIOKUWA PAMOJA NAMI TOKA MWANZO WA SIMULIZI HII YA KWELI KABISA
NAWAPENDA SANA NA MUNGU AWABARIKI!

[><MAZIMA><]

MAJIGO,

Je, hii ni hadithi ya Kweli au??? nijibu tafadhali nina maswali mengi juu ya stori yako hii!!
 
74---Nilitembea taratibu kuelekea nyumbani kwa mjomba, muda ulionesha bado asubuhi kwani hata mlango ulikuwa haujafunguliwa.
Kabla ya kugonga nilijifikiria nizivue zile khanga au niingie nazo vilevile . Niliamua kuingia na khanga zangu ili wasishtuke mapema.

Niligonga mlango na kusubiri, mke wa mjomba ndiye aliyekuja kunifungulia, nilijua hakunifahamu baada ya kuniona. “Karibu, una shida gani?”
Aliniuliza akiwa bado amesimama mlangoni. “Nataka nimuone mjomba.” “Mjomba wako nani?” “Mayunga.” “Mayunga! Wewe nani?” “Shi..,” nilisita kulitaja jina langu. “Umesema nani?” “Shija.” “Shija si jina la kiume hilo?” “Ndiyo.”

Nilisema huku nikitoa khanga niliyojitanda kichwani, nilimuona macho yakimtoka pima kama kaona ngamia akipita kwenye tundu la sindano.
Akitaka kujirudisha nyuma ili anikimbie, niliamini kabisa aliniona si mtu wa kawaida bali mzimu wangu kwa vile aliamini nimekwisha kufa na kuzikwa . Shangazi alipiga kelele: “Jamani nakufa..,” alianguka chini na kupoteza fahamu, mjomba ambaye alionekana amemaliza kujiandaa ili aende kazini.

Alikuja mbio na kumuwahi mkewe bila kuniangalia mimi ni nani. Bila kunitazama usoni aliniuliza: “Amefanya nini huyu,” aliendelea kumtazama mkewe aliyekuwa amepoteza fahamu.

“Ameshtuka baada ya kuniona.” “Kukuona?” Aliuliza huku akinitazama aliponiona ni mimi alishtuka kiasi cha kumbwaga mkewe chini. “Ha! Wee nani?” “Shija mjomba.”

“Hapana, hiwezekani haya ni maajabu.”
“Siyo maajabu, sikufa mjomba.” “Kama hukufa aliyekufa ni nani?” “Mjomba kile ni kiini macho cha wachawi .” “Muda wote huo ulikuwa wapi?” “Mjomba mshughulikie kwanza shangazi nina mengi ya kuzungumza juu ya kifo changu cha bandia.”

Mjomba alimpatia huduma ya kwanza shangazi ambaye alirudiwa na fahamu lakini ilionesha bado ananishangaa. “Huyu si Shija?” Shangazi aliuliza kwa sauti ya juu. “Ndiye.” “Mungu wangu! Haya si maajabu Shija katoka kuzimu si alikufa huyu?”

“Sijafa Shangazi kilikuwa kiini macho cha wachawi .” “Kama hukufa nani alikufa tukamzika?” “Shangazi mimi sikufa ila kilichotendeka siku ile ni kiini macho tu, hamkuzika mtu bali kipande cha mgomba.”

“Na wewe ulikuwa wapi siku zote?” “Ni stori ndefu shangazi.” “Jamani haya ni maajabu ni kweli Shija hujafa?” Shangazi aliendelea kunishangaa. “Kama ningekuwa nimekufa nisingeonekana leo.” “Muda wote ulikuwa wapi?” Mjomba aliniuliza.

“Nilikuwa naishi maisha ya kimsukule.”
“Mungu wangu! Umewezaje kutoka katika maisha hayo? Hizi khanga umezitoa wapi?” “Ni mtoto wa mchawi aliyenichukua msukule.”
“Ndiye aliyekutoa?”
“Ndiyo.”
“Na siku ya msiba wako ulikuwa wapi?” “Nilikuwa nyuma ya mlango, yote mliyokuwa mkifanya niliyaona, wakati mnakuja nilisikia hata mlipoingia ndani kumpa pole mama na kuangua kilio, yote nilikuwa nayaona.

Hata makaburini nilihudhuria mazishi yangu.” “Hii kali kweli wachawi viumbe wa ajabu,” alisema mke wa mjomba huku akishika mikono kiunoni.

“Sasa wamekuachia au imekuwaje?” “Nimetoroshwa.” “Mungu wangu ilikuwaje mpaka ukatoroshwa?” “Ni habari ndefu, naomba nioge niondoe nuksi ya maisha ya nusu kuzimu na nipate chakula maana hapa njaa inaniuma kama kidonda.”

Nilipatiwa vitu vyote kwa haraka hata safari ya mjomba na mkewe kwenda kazini iliahirishwa ili kutaka kujua maajabu chini ya jua. Baada ya kuoga na kupata kifungua kinywa nilikaa kitako kuwaeleza yaliyonisibu huku nikiificha siri ya kumtaja Helena na mama yake kwa usalama wa kijijini.

Siku hiyo nilichukuliwa na kupelekwa kwenye kanisani kufanyiwa maombezi kwa utukufu wa Mungu kuonesha jinsi nguvu zake zinavyoweza kuushinda uchawi.

Mjomba alitaka kunipeleka nyumbani, nilimweleza masharti niliopewa na mtu aliyenitoa kule kuwa nisirudi tena kijijini.

Mjomba alikubaliana na mimi nibakie kwake , wazazi wangu walifuatwa , hawakuamini lakini niliwaeleza ilivyokuwa na kukubaliana na mimi, ilikuwa furaha isiyo kifani.

Baada ya muda niligundua kumbe niliishi maisha ya umsukule kwa mwaka mmoja na miezi sita.
Mjomba alinitafutia shule ambayo nilisoma kwa miaka miwili na kufanya mtihani wa kidato cha nne.

Majibu yalikuwa mazuri kwa kupata ‘division two’ iliyoniwezesha kuingia kidato cha tano mpaka chuo kikuu

NAMSHUKURU MUNGU, NA NYOTE GUEST NA MAMBER WENZANGU WA JAMII FORUMS
MLIOKUWA PAMOJA NAMI TOKA MWANZO WA SIMULIZI HII YA KWELI KABISA
NAWAPENDA SANA NA MUNGU AWABARIKI!

[><MAZIMA><]

NOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
I cant believe ni simulizi ya kweli; bwana sio vizuri hivyo!
 
NOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
I cant believe ni simulizi ya kweli; bwana sio vizuri hivyo!

Dah, umeona? Bado siamini kama ni kweli.

Aje ahakikishe kuwa ni kweli hapa!
 
Mkuu Majigo umeniacha na maswali mengi, an anyway, nachukulia kama stori tu, ngumu kumesa kwa kweli!

Kwa hiyo hujawahi kwenda kwenu tena? Mama Helena na Helena na Sabina wanaendeleaje?

We MESTOD, jiulize maswali tu huku unalimwa memo kwa ufanisi wako wa kazi Kuwa duni kwa ajili ya kusoma story! Ahahahahahahaaaaa, kama kawa MWANA burudani baada ya kazi ni lazima !

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Kisa kizuri chenye kusisimua,mkuu Majigo wewe ndo Shija nini uliyekutwa na huo mkasa?Mazima Mkuu!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Uwanja Ni Wako Mkuu
Mazima

Nashkuru kwa kisa chako very interesting tatizo imeishia pabaya na maswali kibao helen aliporudi kijijin ilikuwaje, mama je sii ataendelea kuiandama familia ya kina shija, kwa sasa shija anaendeleaje. Nawasilisha mkuu
 
Umenitisha ulipomalizia ya kweli kabisa, hii dunia kuna watu wana historia
 
Aixee nimeshinda siku nzima,nasoma ur story,,, if ts true ur such a lucky person
 
Majigo hongera sasa tumtafute muuza ubuyu tumchukue msukule ananguvu sana huyu akatulimie kule kibada
 
mia umetisha mzazi hongera sana nakubali kazi @ Majogo
 
Back
Top Bottom