Nitakufa Mara Ya Pili

Nitakufa Mara Ya Pili

unaambiwa kingozi ukitunze unaleta uzembe kazi kwako nyanda shija yalya kunhako!!!!!
 
67--“Shija umechelewa nina kazi ya ziada japo sina uhakika kama nitaweza.” “Mungu wangu basi nimekwisha.” “Shija usikate tamaa, hebu nifuate.” Alinishika mkono na kuanza kukatiza kwenye mahindi na mihogo, hali ilikuwa tofauti na siku zote, mvua ile ilikuwa bado inaendelea kunyesha.


“Helena mvua hii ni ya kweli au kichawi?” “Shija mvua ya leo ya kweli wala si ya kichawi.” “Mbona sehemu niliyokuwa iligeuka shimo la tope?” “Shija hukuzama kwenye tope kama ulivyodhani, bali ulikuwa umelala kwenye tope.”

“Ha!” Nilishtuka. “Mambo ya kichawi yana mauzauza, wamepanga kukutesa mpaka ufe kisha wakule nyama yako. Nami nimeapa nitahakikisha hawali nyama yako.” “Mungu wangu nimekwisha,” kauli ya kuliwa nyama ilinikata maini.


Nilikumbuka jinsi kaka yangu Luhemeja alivyoliwa nyama na wachawi, woga ulizidi kuniongezeka, Lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kumuomba Mungu aniepushe na balaa zito kama lile, japo Helena alinieleza ukishageuzwa msukule ni kazi kurudishwa duniani mpaka ifanyike kazi nzito.


Tuliendelea kukatiza kwenye mashamba kwa kukanyaga mazao ya watu. Baada ya mwendo wa nusu saa ambao sikuelewa tunakwenda wapi, kutokana na kutofika safari yetu, ghafla Helena alisema: “Shija hebu subiri,” nilishangaa kumuona Helena akiinama. “Vipi Helena?”
“Shija, nimeumia” “Nini?” “Nimeumia, sijui kama tutafika mbali,” Helena alisema huku akikaa chini na kushikilia mguu wake wa kulia.


Nilishtuka kuona damu, niliinama kuangalia. “Mbona damu zinatoka kwa wingi umekanyaga nini?” “Hata sijui, hebu kivute kilichonichoma.” Nilipiga magoti na kuvuta kwa meno kipande cha mti kilichomchoma, baada ya kukitoa, Helena alinyanyuka na kuendelea na safari yetu kwa shida kutokana na Helena kutembea kwa kuchechemea.


Hata kasi yetu ilipungua, kila hatua Helena alilalamika mguu unazidi kumuuma na damu iliendelea kumtoka. Nilivua kaputula yangu na kubakia na nguo ya ndani. Niliichana kwa meno japo ilinipa shida kutokana na kuloa na tope lakini nilijitahidi mpaka nikafanikiwa kutengeneza kitambaa cha kumfunga Helena.


Wakati namfunga jeraha ambalo lilikuwa bado linavuja damu, Helena alipiga kelele. “Shijaaaa...” Kilichofuata sikujua baada ya kuhisi nimepigwa na kitu kizito kichwani na kupoteza fahamu. Nilipozinduka nilijikuta nimelala sehemu iliyokuwa na baridi kali na harufu mbaya, nilipofumbua macho kulikuwa na kiza kinene, nilijiuliuza pale ni wapi?
Nilipapasa mkono na kuugusa mwili wa mtu aliyekuwa amekaa pembeni yangu.


Mara nilimuona mtu akija na kibatari na kuanza kuwaamsha watu. “Haya amkeni,” mkononi alikuwa na fimbo kama ya kupigia ng’ombe. Nilisikia watu wakiamka kama ng’ombe kwenye zizi. Nami ilinibidi niamke kwa vile tuliamriwa kuamka wote. “Shija rudi ulale.”


“Nilijiuliza yule ni nani mbona sauti yake ni ngeni.” Wengine niliokuwa nimelala nao walipochelewa kuamka walitandikwa fimbo za mgongo na kutoa mlio mkubwa kuashiria zimewaingia barabara. Watu wote walinyanyuka ilionesha walikuwa wengi sana.


Baada ya muda, wote walitoka nje na nikabakia peke yangu. Nikiwa nimejilaza huku nikikung’utwa na baridi, nilibaki najiuliza pale ni wapi, mbona wale watu wametoka wote nje huku wakipigwa kama ng’ombe? Usingizi ulipotea kichwani na kunifanya nibakie nimejikunyata kwa baridi.

Nikiwa bado sijapata jibu, alikuja yule msichana aliyekuwa akiwaamsha misukule wenzangu.


“Shija.” “Naam.” “Vipi nikuletee chakula?” “Wewe nani na hapa nipo wapi?” “Utajua tu, la muhimu kwanza nikupatie chakula.” “Sawa.”

Nilimkubalia kutokana na njaa kali iliyokuwa ikinichonyota. Yule msichana aliondoka na kuniachia maswali mengi, nilijitahidi kumfahamu bila mafanikio, nilishindwa kumjua kutokana na mwanga hafifu wa taa aliyoshikilia.


Baada ya muda alirejea na bakuli lililokuwa na viazi, mkono mwingine alishikilia maziwa yaliyokuwa kwenye kibuyu kidogo.
“Shija kula.” “Asante, lakini wewe nani na hapa nipo wapi?” Niliendelea kumuuliza. “Shija, nimekueleza utanifahamu na hapa utapajua tu, hebu kula kwanza nina kazi nyingi huu si muda wa mazungumzo.”


Nilikula viazi pamoja na maziwa na kushiba barabara kutokana na ubao mzito, yule binti aliniuliza: “Vipi umeshiba?” “Nimeshiba.” “Basi pumzika tutazungumza kesho.” “Mbona sina shuka?” Kauli yangu ilimfanya yule binti kucheka kitu kilichonishangaza, kumuomba shuka yeye anacheka.



INAENDELEA.....
 
mkuu 2pia ki2 aisee yani utamu ndo kwanza unanoga...
 
67--“Hebu subiri.” Aliondoka na kuniachia maswali mengi ya kujiuliza pale ni wapi na Helena yupo wapi? Wakati nikiwa katika maswali yasiyo na majibu, alirudi yule binti ambaye alikuwa akinijua lakini mimi simjui, alipofika alinipa kipande cha gunia.


“Shija, samahani kwa leo utalalia hili.” Nilipokea, kilikuwa kipande cha gunia, nilishtuka kupewa kipande cha gunia kujifunika. Lakini yule msichana hakutaka maelezo zaidi. Baada ya kunikabidhi, aligeuka na kuondoka.


Nilijikuta nikizidi kuwa njia panda kwa maswali yasiyo na majibu. Nilijifunika kile kipande cha gunia ili kupunguza ukali wa baridi iliyokuwa ikiniingia hadi kwenye mifupa. Usingizi ulikuwa mbali kila nililowaza lilipotelea hewani, nilitamani ninyanyuke na kupapasa kutafuta mlango nitoke.


Bado niliona ni kufanya kichekesho kwa vile siwezi kutoka sehemu nisiyoijua. Wazo la haraka lilinijia labda ndiyo nimeshakuwa msukule kamili. Akili yangu ilipingana na kile nilichokuwa nakiona na kushindwa kuamini, msukule anawezaje kula viazi na maziwa?


Bila kujielewa usingizi ulinipitia, nilishtushwa na kitu kilichoniminya kwenye mbavu, nilinyanyuka haraka, kidogo nipige kelele za woga baada ya mguu uliokuwa na magaga kunikanyaga karibu na tumbo. Nilipofumbua macho, nilishtushwa kuona watu wakirudi wakiwa wamechafuka kwa vumbi na matope.


Akili ya haraka haraka nilifahamu wale ni misukule kwa vile nilishawahi kuwaona nilipopelekwa na Sabina nyumbani kwao Helena kwenda kumuona marehemu kaka yangu. Watu wale wenye nywele nyingi na kucha chafu za mikono waliingia ikionekana wanatoka kufanya kazi za usiku.


Kila mmoja alikaa sehemu yake, hali ya mule ndani ambako palikuwa kama kwenye ‘godauni’ la kutunzia vitu ilibadilika. Harufu kali ya jasho lilizidi kuumiza pua zangu. Hakuna hata mmoja aliyeonekana kumfuatilia mwenzake, wote walikuwa kimya wamejiinamia.


Kitu kilichonishangaza watu wengi walionekana na afya kama wanabeba vitu vizito, nilijiuliza wanakula nini na wana furaha gani ya kuishi maisha yale kufikia hatua ya kunenepa. Nilikuwa nimekaa na kujifunika kipande cha gunia kutokana na baridi ya alfajiri.


Aliingia binti mmoja, nilipomwangalia, nilimfahamu kuwa ni mdogo wake Helena. Alinisogelea na kunisalimia. “Mambo Shija?” “Poa.” “Vipi, baridi?” “Mmh! Wee acha tu.” “Pole sana.” “Bado sijapoa, Helena yupo wapi?”
“Mmh! Helena amevimba mguu hawezi hata kutembea baada ya kuumia jana wakati akitaka kukutorosha.”
“Mungu wangu na hapa nipo wapi?” ”Hapa ni nyumbani kwetu.”


“Nafanya nini?” “Shija umegeuzwa msukule lakini bado hujawa msukule kamili.”

“Una maana gani?” “Kuna kitu alinieleza Helena, sijui nini..,” ilionesha amesahau. “Kuhusu nini?” “Shija nimesahau nitakwenda kumuuliza Helena.”

“Kwani yeye yupo wapi?”
“Yupo nje amejilaza kwenye mkeka.”
“Mbona hajaja, bado hawezi kutembea?” ”Ameniambia amekatazwa asikusogelee, la sivyo akifanya kiburi basi watakugeuza kitoweo.” “Mmh!” Niliguna. “Pole Shija.”


“Hata sijui niseme asante au?” “Kwa nini?”
“Matatizo yangu bado, unataka kuniambia nitaishi maisha haya siku zangu zote zilizobaki za kuwa duniani?” “Mmh! Siwezi kujua.” “Sundi, ina maana wewe hujui taratibu za kichawi?” “Ndiyo.”


“Wewe si mchawi?” “Ndiyo.” “Mbona jana ulikuja kuwaamsha na huku ukiwatandika bakora?” “Hutumwa mara moja moja hasa au Helena anapokuwa na udhuru, pia yupo mama mdogo ambaye amesafiri.” “Kwa hiyo wewe si mchawi?” “Ndiyo.”



INAENDELEA...
 
68---“Kama si mchawi mambo ya kichawi umeyajuaje?” “Shija sikuja kujibu maswali, chakula watakacholetewa wenzako usikiguse, wewe subiri chako.” “Mpe pole Helena.” “Amesema mtaonana usiku atakuja kuzungumza na wewe.” “Sawa.”


Baada ya kusema vile aligeuka na kuondoka lakini baada ya muda alirudi na blauzi ya Helena na kunipa niivae. Niliifahamu nguo ile kutokana na kuwahi kumuona Helena ameivaa. “Shija utavaa hii.” “Asante.” Sundi aliondoka na kuniacha nikivaa blauzi ya Helena, kisha nilijiegemeza kwenye ukuta nikiyawaza maisha ya kimsukule.


Nilijiuliza baada ya muda nami nitakuwa kama mwenzangu kuishi bila kuoga, nywele zisizo nyolewa wala kusukwa na kucha ndefu zenye kutunza uchafu. Nikiwa bado nipo kwenye maswali magumu ambayo niliamini mpaka kuingizwa mle ndani kuanza kutumikia kifungo cha maisha cha kimsukule, hakukuwa na mtu wa kuweza kuyajibu maswali yangu japo nilijipa matumaini huenda Helena ana kitu kipya cha kuniambia.


Lakini nilikumbuka jinsi tulivyotaka kumtorosha kaka yangu na tuliposhindwa, nilishuhudia akiliwa nyama mbele ya macho yangu. Wasiwasi ulikuwa mkubwa kama Helena atanishawishi kunitorosha na kuishia mikononi mwa wachawi.


Nikiwa nimezama kwenye dimbwi la mawazo waliingia watu wanne wanawake wawili na wanaume wawili wakiwa na masinia makubwa mikononi mwao yaliyokuwa na kitu kama uji huku yakifuka moshi kuonesha muda mfupi yametolewa jikoni.


Baada ya kuyaweka chini yale masinia, wenzangu waliyavamia na kuanza kunywa kwa mikono bila mikono yao kuungua. Walioleta yale masinia walinishangaa na kuniuliza: “Wewe mbona huli? utakufa na njaa,” sikuwajibu niliwatazama tu.


“Mwache ajitie kiburi atanyooka tu,” mwingine aliongezea. Sikuwajibu niliwatazama tu, niliziona sura zao ambazo zilikuwa ngeni kwangu, baada ya wenzangu kumaliza kula kwa kugombania kama mbwa, wale watu walibeba masinia na kuondoka nayo huku wakiwaacha wakilamba mikono yao michafu iliyokuwa na uji.


Nilishindwa kuelewa kwa ulaji ule walishiba kweli au laa, walioleta chakula kile waliondoka huku nikiwasindikiza kwa macho. Kuna maneno waliyazungumza kwa kunong’onezana kisha walicheka na kutoka nje, baada ya muda mdogo wake Helena aliingia na viazi na maziwa ya mtindi, nami nilishambulia kisha nilijilaza kwenye kipande cha mkeka na kujifunika kipande cha gunia.


Muda ule kulikuwa kimya hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa akizungumza. Wote tulijilaza huku nikiwa bado najiuliza yale ndiyo maisha yangu mpaka kufa? Niliamini kulia kusingenisaidia kitu chochote zaidi ya kukubali matokeo, baada ya kufanya uzembe mwenyewe.


Lawama zangu kwa Helena hazikuwa za msingi kwa vile ilionesha nimejitaki mwenyewe. Siku ile nilikula chakula muda tofauti na wenzangu, nilikula mara tatu, wao walikula mara mbili. Walikunywa uji alfajiri na chakula kingine walikula saa kumi na mbili jioni.


Na usiku ulipoingia tulilala wote kila mtu sehemu yake, ilipofika katikati ya usiku aliingia mtu tofauti na mdogo wake Helena na kuwaamsha misukule kwa mtindo ule ule wa kuwatandika bakora.

Kwa vile alikuwa mtu mwingine aliyeonekana hana mzaha hata kidogo, nilijikuta na mimi nikinyanyuka na kurudi nyuma ili nisipigwe na bakora walizokuwa wakipigwa misukule wenzangu.


Nilishangaa kusikia aliyekuwa akiwapiga akiniita jina langu: “Shija toka huko.” Nilitoka kwenye kundi la msukule na kusogea sehemu iliyokuwa tupu, aliendelea kuwatandika waliokuwa wanachelewa kuamka. Baada ya kutoka wote kama kawaida nilibakia ndani peke yangu.


Dada aliyekuwa akiwafurumusha misukule alirudi na kunieleza: “Shija unaweza kuendelea kulala.” “Asante,” nilimjibu huku nikijilaza kwenye kipande changu cha mkeka na kujifunika gunia. Alitaka kuondoka lakini alinigeukia na kuliita jina langu tena: “Shija,” “Naam.”


“Umempa nini Helena kiasi cha kutaka kujitoa kafara kwa ajili yako?” “Sijampa kitu.” “Ni mpenzi wako?’ ”Ni rafiki yangu wa kawaida tu.” “Mmh, Shija niambie ukweli.” “Kweli kabisa.” “Mmh haya!” Baada ya kusema vile aligeuka ili aondoke, alinigeukia tena na kunisemesha:

“Nilisahau,
Helena amesema anakuja, alikuwa anasubiri mama yake aondoke.” “Sawa.” Yule dada aliondoka na kuniacha nimejilaza kwenye kipande changu cha mkeka, baada ya kuondoka nilijiuliza maswali ya yule dada juu yangu kuhusiana na Helena kujitoa muhanga kwangu, alikuwa na maana gani?

Wakati najigeuza ubavu wa pili nilishtushwa na mwanga wa kibatari. Nilijigeuza kuangalia kuna nini tena, nilimuona Helena akija huku akichechemea. ”Shija,” aliniita. “Helena,” nilisimama. “Pole Shija.” “Asante.” “Shija upo sawa?” “Nipo sawa.” “Hawajakupiga?”



Helena atamueleza nini Shija? Je, ataweza kumuokoa?
INAENDELEA...
 
69--“Hawajanipiga si umewakataza.” “Shija wangu jamani,” Helena alinikumbatia huku akibubujikwa na machozi. “Usilie Helena,” nilijikuta nikimuonea huruma. “Siwezi kuacha kulia, Shija upo sehemu mbaya.”


“Ni kweli, lakini sina jinsi.” “Shija nimepata kazi sana kukutetea, mama yangu ana roho mbaya aliitamani damu na nyama yako,” Helena alisema huku akiketi kwenye mkeka wangu. “Kwani nimemkosea nini?” “Toka siku tulipogombana shuleni bado nipo na Sabina, ulipotuambia sisi wachawi alikasirika sana.


Kingine kukingiwa kifua na marehemu mzee Manoni, kitendo kile kilimuuma sana hasa siku ile tulipokuwa tunakutorosha na kushtukiwa na mzee Manoni na kupewa adhabu ya kutoa nyama ya mtu katika familia. Aliapa kuwa mzee Manoni aishi milele lakini akitangulia basi cha moto ungekiona.”


“Lakini mbona aliona mimi na wewe tumepatana?” “Hata sijui kwa nini alikuchukia kiasi hicho.” “Kwa hiyo ndiyo kasemaje?” “Shija, wana bahati siku ile nilijikwaa na kuumia, lakini nisingekubali wakukamate kirahisi vile. Baada ya kukufikisha hapa walipanga kukula siku ile ile usiku.


Lakini nilimuapia mama kuwa wakikula nyama atafuata yeye au mimi. “Mama alinibembeleza sana nikubali wakutie adabu, ujinga wa mara ya kwanza nilivyo kusaliti, lakini niliapa sitarudia tena kutenda kosa la kinyama kama lile.

Niliapa sitakusaliti mpaka nakufa. Pamoja na kunitisha nilikuwa tayari kwa lolote kuhakikisha wanatula nyama wote. “Ilibidi kifanyike kikao usiku ule ule wakubaliane wakufanye nini, wapo waliopendekeza uwe mchawi kwa vile siri nyingi unazijua.


Lakini ulikosa sifa moja, ulishafanyiwa zindiko la kifo. Wengine walipendekeza uwe msukule, wengi waliunga mkono. Wakati wanajiandaa kukufanya ndondocha, niliendelea kumbembeleza mama wasikutie undondocha, wakuache msukule freshi.


Mama alisema analifanyia kazi, ndiyo maana mpaka leo hii upo katika hali hii.” “Asante sana Helena.” “Shija muda wa kunishukuru bado, mpaka nikutoe humu ndani.” “Helena! Bado tu hujakata tamaa?” “Siwezi kukata tamaa, kwanza kukuleta hapa ni nafasi yangu nyingine ya kufanya vitu vyangu kwa uhakika.”


“Helena, unaweza kukosea na kusababisha nikageuzwa asusa.” “Shija wee acha tu, nitakachokifanya hutanisahau mpaka unaingia kaburini.” “Helena unataka kufanya nini?” “Shija ni siri yangu naijua mimi na Mungu wangu.” “Hivi wale walioletea chakula misukule wenzangu, kina nani?”

“Wale ni wafanyakazi walioajiriwa kwa ajili ya kupikia misukule.” “Nao ni wachawi?” “Si wachawi, ila hujipaka dawa ili kuwaona misukule wakati wa kuwapa chakula.”
“Hawawezi kutoa siri nje?” “Wapo waliojaribu lakini walikufa na wengine kuwa vichaa siku siri ilipovuja.”


“Eti mama Suzana alikufa au ndiyo wamemfanya kama mimi?” “Mama Suzana kweli amekufa baada ya kutupiwa uchawi, lakini kaburi lake ndugu zake walizindika. Mwili wake haukuchukulika.” “Kwa hiyo walitaka kumfanya nini?” “Shija kuna kitu kingine zaidi ya kumla nyama.”


“Mh! Kweli wamepania.” Siku ile tulizungumza mpaka kulipokaribia kupambazuka ndipo Helena aliponiaga na kuniachia kipande cha shuka. “Shija utajifunika hiki.” “Asante Helena.”


Helena aliondoka na kuniacha nizidi kumfikiria na msaada wake mkubwa kuokoa maisha yangu.
Haukupita muda Misukule wenzangu walirudi toka kwenye mashamba ya mama Helena. Siku zilikatika nikiwa naishi maisha ya kimsukule, tofauti yangu na misukule wengine ilikuwa, wao hawaongei lakini mimi nilikuwa naongea pia nilikula chakula kizuri, nililala kwenye kipande cha mkeka na kujifunika shuka.


Lakini wenzangu walilala chini vifua wazi. Hata ulaji wao ulikuwa tofauti nmimi, wakati wa kula
waligombea chakula kama nguruwe, hata chakula chao kilikuwa bora chakula, siku nyingine walikula mapumba au ugali ambao haufai mwanadamu kula. Helena naye alipona na kuweza kuingia ndani mle wakati wa kuwatoa misukule kwenda shamba. Siku nyingine alinichukua kwenda kuangalia kazi ya misukule mashambani.


Asikuambie mtu wanadamu tunateseka, walilima kama trekta na anayetegea hutandikwa kama ng’ombe. Kuna kipindi Helena aliwatandika mpaka nikawa nafumba macho, kingine kilichonishangaza ni ukubwa wa shamba la mama Helena. Nilijiuliza shamba lile lipo wapi.


Nini hatma ya maisha ya Shija?


ITAENDELEA BAADAYE.... NIKIWA MAPUMZIKONI KTK BIASHARA YANGU YA KARANGA!
 
  • Thanks
Reactions: Cpp
2pia mzee majigo mambo matamu sana....
 
69--"Hawajanipiga si umewakataza." "Shija wangu jamani," Helena alinikumbatia huku akibubujikwa na machozi. "Usilie Helena," nilijikuta nikimuonea huruma. "Siwezi kuacha kulia, Shija upo sehemu mbaya."


"Ni kweli, lakini sina jinsi." "Shija nimepata kazi sana kukutetea, mama yangu ana roho mbaya aliitamani damu na nyama yako," Helena alisema huku akiketi kwenye mkeka wangu. "Kwani nimemkosea nini?" "Toka siku tulipogombana shuleni bado nipo na Sabina, ulipotuambia sisi wachawi alikasirika sana.


Kingine kukingiwa kifua na marehemu mzee Manoni, kitendo kile kilimuuma sana hasa siku ile tulipokuwa tunakutorosha na kushtukiwa na mzee Manoni na kupewa adhabu ya kutoa nyama ya mtu katika familia. Aliapa kuwa mzee Manoni aishi milele lakini akitangulia basi cha moto ungekiona."


"Lakini mbona aliona mimi na wewe tumepatana?" "Hata sijui kwa nini alikuchukia kiasi hicho." "Kwa hiyo ndiyo kasemaje?" "Shija, wana bahati siku ile nilijikwaa na kuumia, lakini nisingekubali wakukamate kirahisi vile. Baada ya kukufikisha hapa walipanga kukula siku ile ile usiku.


Lakini nilimuapia mama kuwa wakikula nyama atafuata yeye au mimi. "Mama alinibembeleza sana nikubali wakutie adabu, ujinga wa mara ya kwanza nilivyo kusaliti, lakini niliapa sitarudia tena kutenda kosa la kinyama kama lile.

Niliapa sitakusaliti mpaka nakufa. Pamoja na kunitisha nilikuwa tayari kwa lolote kuhakikisha wanatula nyama wote. "Ilibidi kifanyike kikao usiku ule ule wakubaliane wakufanye nini, wapo waliopendekeza uwe mchawi kwa vile siri nyingi unazijua.


Lakini ulikosa sifa moja, ulishafanyiwa zindiko la kifo. Wengine walipendekeza uwe msukule, wengi waliunga mkono. Wakati wanajiandaa kukufanya ndondocha, niliendelea kumbembeleza mama wasikutie undondocha, wakuache msukule freshi.


Mama alisema analifanyia kazi, ndiyo maana mpaka leo hii upo katika hali hii." "Asante sana Helena." "Shija muda wa kunishukuru bado, mpaka nikutoe humu ndani." "Helena! Bado tu hujakata tamaa?" "Siwezi kukata tamaa, kwanza kukuleta hapa ni nafasi yangu nyingine ya kufanya vitu vyangu kwa uhakika."


"Helena, unaweza kukosea na kusababisha nikageuzwa asusa." "Shija wee acha tu, nitakachokifanya hutanisahau mpaka unaingia kaburini." "Helena unataka kufanya nini?" "Shija ni siri yangu naijua mimi na Mungu wangu." "Hivi wale walioletea chakula misukule wenzangu, kina nani?"

"Wale ni wafanyakazi walioajiriwa kwa ajili ya kupikia misukule." "Nao ni wachawi?" "Si wachawi, ila hujipaka dawa ili kuwaona misukule wakati wa kuwapa chakula."
"Hawawezi kutoa siri nje?" "Wapo waliojaribu lakini walikufa na wengine kuwa vichaa siku siri ilipovuja."


"Eti mama Suzana alikufa au ndiyo wamemfanya kama mimi?" "Mama Suzana kweli amekufa baada ya kutupiwa uchawi, lakini kaburi lake ndugu zake walizindika. Mwili wake haukuchukulika." "Kwa hiyo walitaka kumfanya nini?" "Shija kuna kitu kingine zaidi ya kumla nyama."


"Mh! Kweli wamepania." Siku ile tulizungumza mpaka kulipokaribia kupambazuka ndipo Helena aliponiaga na kuniachia kipande cha shuka. "Shija utajifunika hiki." "Asante Helena."


Helena aliondoka na kuniacha nizidi kumfikiria na msaada wake mkubwa kuokoa maisha yangu.
Haukupita muda Misukule wenzangu walirudi toka kwenye mashamba ya mama Helena. Siku zilikatika nikiwa naishi maisha ya kimsukule, tofauti yangu na misukule wengine ilikuwa, wao hawaongei lakini mimi nilikuwa naongea pia nilikula chakula kizuri, nililala kwenye kipande cha mkeka na kujifunika shuka.


Lakini wenzangu walilala chini vifua wazi. Hata ulaji wao ulikuwa tofauti nmimi, wakati wa kula
waligombea chakula kama nguruwe, hata chakula chao kilikuwa bora chakula, siku nyingine walikula mapumba au ugali ambao haufai mwanadamu kula. Helena naye alipona na kuweza kuingia ndani mle wakati wa kuwatoa misukule kwenda shamba. Siku nyingine alinichukua kwenda kuangalia kazi ya misukule mashambani.


Asikuambie mtu wanadamu tunateseka, walilima kama trekta na anayetegea hutandikwa kama ng'ombe. Kuna kipindi Helena aliwatandika mpaka nikawa nafumba macho, kingine kilichonishangaza ni ukubwa wa shamba la mama Helena. Nilijiuliza shamba lile lipo wapi.


Nini hatma ya maisha ya Shija?


ITAENDELEA BAADAYE.... NIKIWA MAPUMZIKONI KTK BIASHARA YANGU YA KARANGA!


ebana majigo inabidi 2kulipe uwe una2ma story uache kuuza karanga mpaka story iishe
 
70--Lakini sikutaka kuuliza kwa kuonekana najifanya najua, kitu ambacho nilikiogopa ni kumuudhi Helena, mtu aliyekuwa muhimu sana kwa kipindi kile. Baada ya kuwahimiza kulima kwa viboko, alirudi chini ya mti niliokuwa nimekaa.


Alionekana akitweta na kukaa pembeni yangu huku akivuja jasho. “Pole Helena, kumbe kutusimamia ni kazi!” “Shija wee acha, kuyasimamia majitu yasiyo na akili kazi kubwa.” “Mbona huwa mnawapiga bila huruma?” “Shija japo hawana akili lakini wana kiburi sana.


Ukiwachekea kazi haifanyiki , nikuambie kitu?” Helena aliniuliza “Niambie.” “Kazi hii nilikwishaikataa na kumuomba mama atafute mtu mwingine wa kisimamia misukule yake. Na mtu alikwishapatikana , mama mdogo aliyekuletea chakula.”

“Sasa mbona unaendelea nayo?” “Sababu yako, imebidi niendelee nayo kuhakikisha unakuwa salama, nahofia nikimwachia mtu mwingine, utateseka.” “Asante, kwa hiyo maisha yangu yote ya huku utaendelea nayo?”
“Ndiyo Shija, kwa vile siipendi kazi hii, hata mimi huwa sipendi kuwapiga misukule kwa kuamini ni viumbe wenzangu.


Nitatumia kila uwezo wangu kuhakikisha nakutoa kisha naachana na kazi hii.” “Utaiachaje?” “Nimeshapata mchumba, wewe ndiye unanichelewesha, nikishakutoa naolewa na kuachana na kazi hii ya kishenzi.” “Mmh! Haya.”


Baada ya kilimo tulirudi nyumbani kuendelea na kifungo changu cha kimsukule.

**************


Siku zilikatika huku nikiendelea na maisha yangu ya kifungo cha msukule, nilikuwa na tofauti kubwa na wenzangu. Helena alihakikisha naishi maisha mazuri japo sehemu yenyewe haikuwa salama.


Tofauti yangu kubwa na misukule wengine ilikuwa ni nywele . Wenzangu walikuwa na nywele ndefu zilizojisokota kwa uchafu, hawakuyajua maji ya kuoga wala kufua nguo, miili yao ilikuwa na harufu kali ambayo mwanzo ilikuwa kero kwangu. Kwa upande wangu Helena alininyoa nywele japo hakuwa mjuzi sana wa kunyoa lakini kichwa kilikuwa kisafi.


Alitumia muda wa kwenda kusimamia misukule shambani kunifanyia usafi wa kuoga na kunifulia nguo zangu.
Siku moja nilishangaa kumuona Helena akiniletea nguo zangu nilizoziacha nyumbani kipindi kirefu toka nijulikane nimekufa.


Kabla ya kupokea ilibidi nihoji: “Helena nguo zangu umezitoa wapi?” “Nyumbani kwenu.” “Kwetu?” Nilishtuka. “Ndiyo, kwenu.” “Helena umezipataje?” “Nimezipata tu.” “Sawa umezipata, kumbuka ni muda mrefu toka nitambulike nimekufa, ina maana nguo zangu bado hawajazichoma?” “Shija, la muhimu kupata nguo, si maswali nimepataje.”

“Mmh, sawa,” nilijibu kwa unyonge... “Shija umekasirika?” Sauti yangu ya unyonge ilimtisha Helena. “Walaa.” “Ngoja nikwambie japo sikupenda kukueleza kitu hiki.” “Kama si cha muhimu kiache tu.”
“Hapana Shija, lazima nikueleze kwa vile umetaka kujua.”

“Hapana Helena, kama unaona halina umuhimu wa mimi kulijua, achana nalo,” nilimtoa hofu Helena. “Si kihivyo .” “Basi niambie.”

“Shija, jana wakati napita kwenu nilimwona baba yako akizitoa ndani baadhi ya nguo zako ambazo alizifukia kwenye shimo alilokuwa amechimba.


Nilipoona vile, niliamini kama nitafukua nitapata nguo za kuvaa, usiku nilirudi na kufukua sehemu zilipofukiwa nguo zako na kuzichukua baadhi ya ambazo ndizo nimekuletea.”

“Helena, hivi maisha yangu ya huku yataendelea hadi lini? Na ni nini hatima yangu juu ya uamuzi wa mama yako?” “Kwa kweli kipindi chote alichonieleza anatafakari hajanieleza kitu chochote, ni wazi amekusamehe.”
“Na vipi mpango wako wa kunitoa huku, nimechoka na maisha ya huku, kuishi na viumbe ambao kila siku wananitisha.”



“Shija shukuru mimi nipo, bila hivyo nawe ungeishi maisha ya wenzako wala usingefikiria kurudi kwenu.

Hawa wenzako wapo kama wanyama wasiojua raha ni nini?” “Kwa hiyo nini hatima ya maisha yao?” “Kuendelea kumtumikia mama mpaka watakapofariki .” “Na wakifa miili yao huliwa nyama?” “Hapana, huzikwa tu, miili yao huwa hailiwi nyama, huwa haifai.” “Mmh! Na mimi je?” “Shija bado najipanga.”
“Mpaka lini?” “Kumbuka bado una kesi na mama hivyo ninatakiwa nisifanye kosa wakati wa kukutoa. Kosa lolote litauumiza moyo wangu.” “Kosa gani?” “Kumbuka nilipojaribu kukutorosha nilikamatwa, ulikuwa uliwe nyama lakini nilikuwa radhi kufa kuliko kukuona unaliwa nyama.
Pamoja na vitisho vizito sikuwa tayari. Lakini nakuhakikishia lazima nitakutoa nakuomba uvumilie tu.” “Mmh, haya nitavumilia japo sina raha na maisha ya huku.”
“Pamoja na hayo lakini ulitakiwa kushukuru kutokana kuwa tofauti na wenzako, unakula chakula sawa na wenzako?” “Hapana.” “Unalala sawa na wenzako?” “Hapana.”

“Hebu jiangalie tofauti na wenzako kwa kila kitu, wao hawazungumzi, wewe unazungumza, wao hawaogi wewe unaoga, wao hawafui wewe unafua, wao wanafanya kazi nzito lakini wewe hufanyi kazi yoyote . Shija naweza sema wewe si msukule ila upo huku.”

“Helena usinifikirie vibaya lakini lazima niseme ukweli toka moyoni mwangu umenifanyia mambo makubwa sana maishani mwangu.” “Shija bado sijafikia nilichokidhamiria kukifanya kwako , nitahakikisha nakutoa humu ndani ukiwa salama.” “Nitashukuru sana Helena.”



INAENDELEA...
 
CPP,ukicoment usi quote,thread inakua ndefu kwa kujirudia rudia
 
71--“Shija nikwambie kitu?” “Niambie” “Wiki moja kuanzia leo nitakutoa humu ndani.” “Mwongo,” nilijua ananitania. “Kweli, niamini.” “Utafanyaje?” “Nitakueleza siku ikifika.” Nilijikuta nikiwa na hamu kujua Helena atanitoa vipi kwenye kaburi linalotembea.


Lakini hakuwa tayari zaidi ya kunieleza atakavyoweza kunitoa kwenye hali ile na kurudi dunia ya kawaida. “Lakini Shija nikikutoa, chonde usirudi tena nyumbani kwenu ikiwezekana hata wazazi wako wahame.” “Sasa tutakwenda wapi?” “Si mnaweza kuuza eneo lenu na kwenda kuishi sehemu nyingine.”


“Helena, unataka kuniambia wachawi hawatafika sehemu tutakayokimbilia ?” “Ooh, lakini kweli, basi nakuomba ukitoka salama ukaishi kwa mjomba wako, kinyume na hivyo wakikupata tena sitakuwa na uwezo wa kukuokoa, pengine nitakuwa kwangu baada ya kuolewa na mambo ya uchawi nitakuwa nimeachana nayo.”

“Mmh! Sijui wazazi wangu na jamii itanichukuliaje nikitokeza mbele yao?” “Ikuchukulie kivipi? Maisha yako wao yanawahusu nini?” “Nitawezaje kujibu maswali yao.” “Shija hayo si maswali ya kujiuliza bali kujifikiria jinsi ya kutoka, mengine najua hayawezi kukusumbua kichwa.”


“Hawawezi kunitafuta na kunipata?” “Hawawezi , kuna dawa nitakupa hawatakusogelea milele, dawa hiyo hupewa tunapoolewa ili tusishiriki mambo ya kichawi waka kudhuriwa nao.” “Unataka kuniambia hata Sabina naye alifanyiwa hiyo dawa?” “Ndiyo.”
“Mmh! Si nitakuwa kituko mbele ya jamii?” “Shija hayo si yakuwaza , kwa hiyo niache kukutoa?” “Hapana Helena.”


“Sasa unataka nikufanyie nini?” ”Nitoe tu, huku haya si maisha.” “Unataka nikutoe lakini unawaogopa watu?” “Helena siwaogopi bali nilikuwa najiuliza jamii itanipokeaje?” ”Kama utakuwa Mwanza hakuna wa kukuuliza kwa vile hawakujui lakini ukirudi kijijini kila mmoja atataka kujua ilikuwa vipi ufufuke kama Masia.”


“Na Mjomba atanielewa vipi?” “Mweleze ukweli?” “Nikutaje?” “Usinitaje, tafuta cha kusema lakini mimi usinitaje wala kuwaeleza ulikuwa wapi.” “Helena nina siri nyingi toka siku ya kwanza kukutana na mauzauza yaliyopelekea kufungwa mdomo na mzee Manoni mpaka leo. Si wewe wala Sabina anayeijua siri iliyo moyoni mwangu.” “Kweli Shija, unaweza kuitunza siri naamini hata hii utaitunza.” “Ondoa shaka kuhusu hilo.”

********

Ajabu wiki ilikatika bila dalili zozote za kutolewa kwenye kifungo cha kuzimu huku kila siku nikipewa matumaini kuwa nisiwe na wasiwasi nivumilie kidogo, wiki ya pili nayo ilielekea ukingoni. Niliamini maneno ya Helena yalikuwa ya kunitia moyo lakini hakukuwa na uwezekano wa kurudishwa duniani.



Siku moja Helena alinieleza kuwa nipumzike nisifuatane naye shambani, nilikubaliana naye na kuendelea kuuchapa usingizi. Katikati ya usiku nikiwa nimejilaza kwenye mkeka wangu baada ya misukule kwenda kulima, nilishtushwa na sauti ya Helena. “Shija.” “Naam.” “Nifuate.” “Wapi?” “Sitaki maswali, fuata sauti.”


Nilinyanyuka kwenye mkeka wangu na kuifuata sauti iliyokuwa kwenye kiza kinene, ilikuwa tofauti na siku nyingine ambazo Helena huja na taa. Ndani ya jumba lile bila taa mnatisha kama ndani ya kaburi. “Upo wapi?” “Fuata sauti yangu,” Helena alisema kwa wasiwasi kidogo.


Nilitii amri na kuifuata sauti ya Helena kwa kupapasa kutokana na kiza kizito cha mle ndani. Nilijawa na maswali mengi yasiyo na majibu kuhusu ujio wa Helena muda ule kwani ulikuwa tofauti na siku nyingine zote za nyuma.


Nilipoikaribia sauti yake aliniita: “Shija.” “Naam, upo wapi?” “Nipo hapa, nipe mkono.” Nilipapasa mkono hewani na kufanikiwa kulishika bega, Helena aliushika mkono wangu na kuanza kuondoka. Kwa vile ilikuwa giza sikujua ananipeleka wapi.


INAENDELEA....
 
Back
Top Bottom