Nitakufa Mara Ya Pili

Nitakufa Mara Ya Pili

57--Swali langu lilimfanya Helena anyamaze kimya na kutazama chini, nililirudia swali langu la awali. “Helena mbona hunijibu, kwa hiyo umeacha uchawi?” “Shija nashindwa nikujibu nini ili unielewe,” Helena alinijibu kwa sauti ya upole akiwa bado ameangalia chini.

“Helena lolote utakalonieleza nitakuelewa.” “Nikikueleza kuwa nimeacha uchawi nitakudanganya ila kwa asilimia kubwa sitashiriki kwenye kazi za kichawi, muda wangu mwingi nitautumia kuhakikisha usalama wako japo kwa sasa najua huna tatizo lolote kutokana mzee Manoni kukusimamia.”

“Najua una kazi nzito ya kuibadili tabia uliyoizoea lakini kila kitu kina mwisho wake, uchukie uchawi mwisho Mungu atakutoa bila ya wewe kujielewa,” nilimpa moyo. “Shija nitajitahidi kufanya hivyo .”

Tuliongozana na Helena kurudi kijijini, njiani tulizungumza mengi yakiwemo yale tuliyoyafanya wakati tukiwa marafiki. Tulipofika kijijini tuliagana na kila mmoja alienda kwao. Nilipofika nyumbani nilijikuta nikijawa na mawazo mengi juu ya maneno ya Helena ya kuniomba msamaha.

Japo nilikuwa na wasiwasi kwa maneno yake na kuyaona kama kweli yalipandikizwa ili kuniteka kimawazo na kunifanyia kitu kibaya. Lakini moyo wangu ulijaa ujasiri kwa kuamini kile nilichomueleza Sabina amsamehe Helena, kuwa adui wa jana anaweza kuwa rafiki mwema wa leo.

Nilijikuta nikimuamini Helena kwa kauli yake kwamba kutaka kuniua kulitokana na shinikizo la kutolewa yeye kafara. Nilijikuta nikimuonea huruma, siku zote pamoja na ubaya aliotaka kunifanyia lakini bado niliyakumbuka mema aliyonifanyia pale alipojitolea kwa hali na mali kumtorosha marehemu kaka yangu.

Badala ya kujionea huruma mimi nilijikuta nikimuonea huruma Helena kwa masaibu yote aliyopata mpaka kuponea tundu la sindano kuuawa na Sabina. Kumbe hata angemuua angekufa na siri nzito moyoni ambayo ilionesha mimi ndiye mhusika mkuu.

Niliamua kusahau yote yaliyopita na kuganga yajayo , nikamchukulia Sabina kama rafiki yangu mwema aliyetaka kujiokoa kwa kuutoa uhai wangu. Siku zote niliamini mwenye uwezo wa kuuchukua uhai wa mwanadamu ni Mungu pekee na si nguvu za giza wala mashetani.

Siku zilikatika, niliendelea na masomo yangu vyema huku nikionekana zile nguvu nilizokuwa nazo shule ya msingi nimezihamishia sekondari, Nilikuwa mmoja ya wanafunzi tegemezi kutokana na uwezo wangu niliouonesha darasani ambao ulinifanya niwe maarufu shuleni.

Wakati wa likizo kubwa mama alinieleza kwamba mjomba ananiita mjini. Nilikwenda kwa mjomba ambako nilijua muda wangu nitautumia kusoma. Jioni ya siku niliyofika , mjomba aliniita pembeni na kutaka kujua niliyomueleza kuhusu kumleta marehemu kaka akiwa hai yaliishia wapi? “Anko mbona kimya, harakati zako za kumleta kaka yako ziliishia wapi?”

Swali lilikuwa zito, nilijikuta nimebakia kimya nikiwa sijui niseme nini. Sikuwa na cha kumueleza kwa kuamini kila nitakachomueleza atazidi kuniona muongo. “Shija si nakuuliza? Ulisema kaka yako hakufa yupo hai, si ndiyo?”
“Kuna mtu alinihakikishia lakini mwisho wa siku alisema alikuwa akinidanganya,” nilitengeneza uongo ili kuficha siri nzito ya kifo cha kaka nilichokishuhudia kwa macho yangu.

“Kwa hiyo hayupo hai?” “Ndiyo.” “Lakini si ulituhakikishia kuwa ulimuona akiwa hai?” “Niliwadanganya kwa vile kuna mtu alinihakikishia kamuoa akiwa hai na kuniahidi atamtoa nije kwako nimtafutie nafasi.”

“Yeye alinijuaje?” “Aliniuliza kama kuna mtu aliye mbali na kijiji ili akimtoa tumlete, nilimueleza upo wewe mjomba ndipo aliponieleza nije nikuambie kwa kunihakikishia kumtoa, hata nilipokuja hapa nilikuwa najiamini kutokana na kauli zake.” “Mmh! Tulijua huo ni uongo, tulikukubalia ili kukuridhisha lakini hakuna kitu kama hicho.

Kaka yako alikufa na tukamzika, hata wewe ulishuhudia.” Sikuwa na jibu zaidi ya kukubali kosa huku nikiendelea kuificha siri nzito moyoni mwangu. Niliamini kama ningemueleza ukweli kuwa kaka yangu hakufa ila ameliwa nyama wakati wa kumtorosha bado asingeniamini. Baada ya likizo nilirudi kijijini kujiandaa na msimu mpya wa kuingia kidato cha pili.

Kama kawaida nilikutana na Helena ambaye alionesha ushirikiano wa karibu sana, muda wote nilipokuwa nyumbani tulikuwa pamoja. Huwezi kuamini kila nilipotoka shuleni nilimkuta njiani akinisubiri na kurudi naye mpaka kijijini.

Siku zilikatika huku nikiendelea kufanya vizuri katika masomo yangu kiasi cha kila mmoja kunibashiria kufanya vizuri katika mtihani wa mwisho kwa kupata ‘division one’.

Nilipofika kidato cha nne katika mwezi wa saba, miezi mitatu kabla kufanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne nilitokewa na jambo jingine la kutisha.
Naikumbuka siku hiyo, wakati natoka shule nikiwa katikati ya mashamba sehemu iliyokuwa haina nyumba, wingu zito lilitanda kuonesha muda wowote ingeshuka mvua kubwa.

Nilijikuta njia panda kwani kurudi shuleni ilikuwa mbali na kwenda nyumbani ilikuwa mbali. Lakini kwa vile nilikuwa nakwenda nyumbani, nilikaza mwendo kuwahi kabla mvua haijateremka. Sikufika mbali mvua iliyoambatana na upepo mkali ikaanza kunyesha.

Nilianza kukimbia lakini upepo mkali ulioambatana na mvua ulinifanya nisione mbele. Niliangalia mti wa karibu ambao niliamini kabisa utanisaidia kupunguza kasi ya upepo japo kwa mvua ningeendelea kunyeshewa .

Nilisogea chini ya mti wa mwembe mkubwa na kujibanza na upepo mkali lakini mvua iliendelea kuninyeshea. Mfuko wa madaftari wote ulilowa pamoja na madaftali yote yaliyokuwemo . Kwa muda mfupi giza zito lilitanda
kama usiku wa manane.

Nilijikuta nikijiuliza kile ni kitu gani? Sikuamini muda wa saa tisa alasiri niliotoka shule mpaka kufika eneo mvua iliponikutia si muda mrefu kisasi cha kuwa na giza zito kama lile.

Nikiwa bado nipo chini ya mtu nikimuomba Mungu aniokoe na janga lile, nilishtushwa na sauti za watu waliokuwa wakicheka mfululizo. Nilitetemeka na woga ulinitawala na kukumbuka mambo niliyoyasahau ya kusumbuliwa na wachawi .


Inaendelea....
 
Muuza ubuyu vipi na wewe una kingozi nini cha kukulinda?ha ha ha
 
Hizi stori hebu muwe mnaziweka kwenye vitabu jamani...
Au Tanzania hamna publishers wa novels?
 
Nasubiri kujua namna gani mzee manoni nilishindwa kumrithisha mikoba yangu Shija, inaniuma kweli ndugu yangu Majigo!
Kwi kwi kwi kwi! JF bwana hadi raha!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Hahahahah
Muuza Ubuyu Banah...
Tuwe Pamoja!
 
Last edited by a moderator:
Muuza ubuyu vipi na wewe una kingozi nini cha kukulinda?ha ha ha

Tena nataka nimtafute Sabina make Majigo kasema kina dada weupe ndo ugonjwa wetu! Mie siogopi kugeuzwa LITUNGA (majigo wafafanulie hapa), ahahahahahaa!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Umeona eeh? Yaani nimejiuliza hivyo hivyo. Hii staili ya mwaka huu kiboko.

Narudia tena" kama Unaona haikufai
Ilie Nyuti,sio kuweweseka tu Hapa
Hiki ni kipengele kidogo sana cha JF
Ningekuwa nashare nawe bundle Sijui Ungenitulia Wapi?
Nakuvika haiba Ya "Mzee Mano...."
Mazima
 
Umeona eeh? Yaani nimejiuliza hivyo hivyo. Hii staili ya mwaka huu kiboko.

Wakuu Speed Tanker na Dina! Niwaulize Kitu? Mweshimiwa Majigo anakopata muda wa kutype ujinga anaupata kule kule mnakopata muda wa kusoma huo ujinga anaouandika!
Na kwa taarifa yenu, hizi kazi zinawafanya watu waishi mjini!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Dii !! Majigo bado tuu???

Ee bana ee..

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Wakuu huenda baada au kabla ya 58
Tutaonana saa moja jion
Chaji mzigoni haisomi!
Mazima
 
58--Sauti za vicheko kila dakika zilizidi kuongezeka na kufanya ziwe kero kwangu kutokana na kuwa kubwa na hivyo kuumiza ngoma za masikio yangu. Nilishindwa kuelewa sauti zile zilitokea wapi, pia giza zito ndilo lilinichanganya zaidi.

Nilijiuliza kile kilichonitokea ni nini, kama ni wachawi ina maana wamekaidi amri ya mzee Manoni? Sauti zilizidi kusogea karibu yangu na kufanya nione kama ngoma za masikio zikikaribia kupasuka. Wakati huo mvua ilianza kukatika lakini ubaridi ulikuwa mkali ambao ulifanya nianze kutetemeka na meno kugongana.

Kutokana na woga huo nilijikunyata kwenye mti bila kujua sauti zile zinatokea mbele au nyuma yangu. Mara zilianza kupungua huku zikisogea mbali na mimi, nilibaki nikiwa sijui nini hatima yangu. Baada ya muda sehemu ile ikawa kimya ikiacha sauti za vyura na bundi ambaye sauti yake niliifahamu kutokana na kuelezwa na baba.

Hiyo ilitokana na siku moja kuisikia juu ya nyumba yetu, nilifahamu karibia sauti zote za ndege kutokana na tabia yangu ya uwindaji. Sauti hiyo ya bundi ilinitisha kwa kujua ni ya uchuro ambayo wengi huamini haina habari njema.
Nikiwa bado nipo chini ya mti, kiza kimeendelea kutanda niliamua kuondoka sehemu kwa sababu macho yalishazoea giza na kuiona njia kwa urahisi.

Nilitamani kulia lakini niliamini si suluhisho la tatizo langu zaidi ya kupambamba nalo. Nilijipa moyo na kutembea kufuata njia ambayo niliamini ilikuwa ikielekea nyumbani. Baada ya mwendo mfupi nilisikia kitu kama ngoma mbele yangu ikija upande wangu, nilibadili njia na kuingia kwenye mashamba japo sikujua nikipata kule nitatokea wapi hasa kutokana na kiza kilichokuwa kimetanda. Ajabu ya Mungu, nilipoingia tu kwenye shamba milio ya ngoma ilizidi kunifuata, sikukubali kushikwa kirahisi, hivyo nilianza kutimua mbio. Kila nilivyokuwa nikikimbia ndivyo ngoma nazo zilivyokuwa zikisogea kwa karibu yangu. Nilizidi kuchanganyikiwa , niliendelea kukimbia. Kuna kipindi nilifanikiwa kuikimbia sauti ya ngoma ambayo niliisikia kwa mbali, kwa vile nilikuwa nimekimbia kwa muda mrefu bila kupumzika huku nikipiga miereka na kuchubuka baadhi ya sehemu ya mwili na kulitupa begi lililokuwa na vitabu ambalo nililiona kama mzigo. Nilisimama huku nikitweta, sehemu za mbavu zilichoma na kunifanya niiname, mikono ikishika magoti na kuhema kwa shida kutokana na kusikia maumivu makali kila nilipopumua. Nikiwa katika hali ya kukata tamaa nilishtushwa na vicheko ambavyo vilionesha havipo mbali nami. Niliamua kuondoka tena eneo lile huku hali yangu ikiwa mbaya kutokana na kuhisi kizunguzungu, maumivu makali ya mbavu na kifua. Niliandoka kwa kuchechemea angalau nipate sehemu nikajifiche kwa kuamini sitafika mbali kutokana na kupoteza nguvu. Hata hivyo , kutokana na macho kupoteza nguvu nilishindwa kutambua nilipo.

Nilifuata kichaka kilichokuwa mbele yangu kama hatua hamsini toka niliposimama. Nilifikiria nikifika pale nitaingia kwenye kichaka kingine ambacho sikuhofia wanyama au wadudu wakali zaidi ya kuokoa uhai wangu ambao ulikuwa unanadiwa kwa bei rahisi.

Nilitembea kwa kuchechemea huku mkono mmoja ukiwa kifuani, sauti ambayo haikuwa ngeni masikioni mwangu iliniita: “Shija...Shija.” Kwanza nilisita kuitika kwa kuhofia kujulikana nilipo, lakini sauti ile iliendelea... “Shijaaa....Shija usiende huko.”

Sikutaka kumsikiliza, niliendelea kwenda huku sauti nazo zikizidi kusogea. Nilipotaka kutimua mbio nilihisi maumivu kwenye goti kutokana na jeraha nililolipata nilipojikwaa na kuangukia shimoni lakini nilinyanyuka na kuendelea kukimbia.

Sauti ile ilizidi kuniita: “Shija usiende huko mbele kuna makaburi, wachawi wanafukua maiti, watakuona.” Sauti ilikuwa ya Helena lakini sikujua alipo, nilijikuta nasimama ghafla na kuitafuta sauti ile inakotokea. “Shija rudi nyuma,” Helena alinielekeza kwa sauti.

Nilifanya kama nilivyoelekezwa kwa kurudi nyuma kuifuata njia niliyokujanayo huku nikiamini kabisa huenda Helena anataka kunifanyia kitu kibaya kutokana na kunirudisha sehemu iliyokuwa na vicheko. Lakini nilipiga moyo konde na kurudi hadi kwenye njia panda.

Helena alitokea kwenye kichaka kidogo ambacho nakikumbuka nilikipita kwa kukiona kama nikijificha naweza kuonekana, kumbe yeye alikuwa pale, alijitokeza akiwa katika mavazi yake ya kawaida.

Nilijiuliza ilikuwaje nimpite pale na kuniacha mpaka nilipokaribia kichaka kingine. Wakati Helena ananikaribia sauti zilizidi kutusogelea, nilitaka kukimbia lakini aliniwahi na kunishika mkono.


ITAENDELEA..SAA 1 jion
 
Narudia tena" kama Unaona haikufai
Ilie Nyuti,sio kuweweseka tu Hapa
Hiki ni kipengele kidogo sana cha JF
Ningekuwa nashare nawe bundle Sijui Ungenitulia Wapi?
Nakuvika haiba Ya "Mzee Mano...."
Mazima

No offense broda, was just wondering muda unakopatikana, wala usinitafutie haiba za kunivika......POLE KWA KUKWAZIKA.
 
Majigo, mzizimkavu na chaichungu yanii raha kwelikweli mkuu nakusubilia
 
59--“Shija unataka kwenda wapi?” Helena aliniuliza kwa ukali kidogo. “Helena watatukamata,” nilisema huku nikijitahidi kujitoa mikononi mwake ili nikimbilie kule aliponikataza. Lakini Helena alikuwa na nguvu za ajabu zilizonifanya niwe mpole.

“Shija, unataka kwenda wapi?” “Helena, husikii wanatusogelea.” “Kina nani?” “Kelele huzisikii?” “Unajua zinatoka wapi?” “Si huku unakotaka kunipeleka.” “Shija, ulipotaka kukimbilia ndiko ulipokuwa unajipeleka, kelele hizi ni mtego wa kukusogeza walipo wachawi .”

“Helena, mbona imekuwa hivi hawamuheshimu tena mzee Manoni?” “Shija, kwani mzee Manoni umeacha kumuona kwa muda gani?” “Mmh! Muda mrefu kidogo.” “Basi kwa taarifa yako kuna kombora alipigwa katika kazi yetu ya uchawi na kumfanya alale kitandani kwa muda mrefu. Na jana amefariki dunia.”

“Ha!” Nilishtuka kumsikia mlinzi wangu amekufa. “Shija mzee Manoni kafariki jana usiku, kijijini, tayari taarifa zimezagaa kila kona ila wewe uliyetoka asubuhi kwenda shule, hukuwa na taarifa ile. Baada ya kifo cha mzee Manoni kulikuwa na sherehe kubwa huku mama yangu akiwakumbushia kukutia adabu baada ya kufa mtu aliyekukingia kifua.”

“Mungu wangu nimekwisha,” nilisema nikishika mikono kichwani kwa kukata tamaa. “Shija nimeapa kukusaidia, jana usiku walipanga wakushughulikie wakati ukitoka shule. Baada ya kupata taarifa hizo nilikuwahi shuleni kwenu, lakini tulichengana kutokana na kupita njia za mkato ili nikuwahi.

Nilipofika nilikuta tayari umeondoka. “Nilijitahidi kuja kwa kasi kukuwahi lakini njiani nilikutana na wingu zito lililonifanya nijue huwezi kufika mbali, lazima utakuwa kwenye hatari ya wachawi , ndipo nilipoanza kukutafuta ili usijiingize kwenye mtego wa wachawi.
Kutokana na muda wa kuwanga ulikuwa haujafika, nilijua watakufanyia vitimbi vya kukuchanganya ili usiku uingie na kukutia katika mikono yao.” “Mungu wangu kama mzee yule amekufa utaweza nini Helena?” Nilizungumza kwa kukata tamaa baada ya kuhisi moyo umekufa ganzi.

“Shija najua upo katika kipindi kigumu hasa muda uliobakia kufanya mtihani, bora mzee huyu angekufa baada ya kufanya mtihani ningekueleza ukimbilie mjini. Lakini kwa udogo wangu, nipo tayari kufa ili kuhakikisha nayaokoa maisha yako.”

“Kwa hiyo huku tunakokwenda ni salama?” “Ni salama kwa vile sauti ile ipo nyuma wala si mbele yetu.” “Kama wasiponipata muda huu, usiku si watanifuata?” “Kazi hiyo niachie mimi, ngoja kwanza nikufikishe kwenu, mambo mengine baadaye.”

Helena alinishika mkono na kuniongoza. Kutokana na kuchanganyikiwa , sikujua pale ni wapi kwa sababu ya giza. Ajabu hatukutembea sana, Helena alinieleza.

“Shija tumefika.” Nilishtuka na kujiuliza mambo yote yale yalikuwa yakifanyika wapi.” “Helena mbona hatukuchelewa kufika?” “Shija ulichanganyikiwa , matukio yote yalikuwa nyuma ya makaburi.” “Haya miembeni?” “Eeh, lile shamba ulimokuwa ni la mzee Masanja.” “Ha!” Nilishtuka kusikia vile.

“Sasa tuachane na hayo, kama kungekuwa na uwezekano kulitakiwa kupatikane maji ya moto nikukande ili kesho uamke mzima bila hivyo utakuwa katika hali mbaya sana.”

“Helena na usiku utakuwaje?” “Nitakuletea ngozi yangu, kwa hilo usihofu.” “Nitashukuru Helena.” “Shija kama nilivyokueleza , nitahakikisha usalama wako muda wote.” “Wewe leo hutoki?” “Sitoki kwa ajili yako, kesho nitajua tutafanye nini.”

“Sasa maji ya moto hakuna, tutafanyaje maana kila dakika maumivu yanazidi?” “Hakijaharibika kitu, twende kisimani.” Tuliongozana na Helena huku akinisaidia kutembea kutokana na kila dakika maumivu kuongezeka.
Tulipofika kisimani, Helena aliniomba msamaha. “Samahani Shija, nakuja ila usiogope.” “Sawa.” Helena aliondoka na kutokomea kizani akiniacha nimejiegemeza kwenye mti wa mchongoma uliokuwa pembeni kidogo ya kisima.

Muda ule maeneo yale yalikuwa yakitisha sana. Milio ya wadudu na ndege wa usiku ndiyo iliyotawala . Lakini nilikaza moyo kumsubiri Helena bila kuelewa amekwenda wapi. Kutokana na uchovu na kibaridi cha usiku, nilijikuta nikipitiwa usingizi pale kwenye mti.
Sauti ya Helena kuniamsha ndiyo iliyoniondoa kwenye usingizi wa mang’amung’amu.” “He! Shija umelala?” “Helena wee acha tu, nipo hoi,” nilisema huku nikijitoa kwenye mti. “Shija tusipoteze muda, vua nguo zote na ulale hapo pembeni ya kisima.”

Nilifanya hivyo kwa kuvua nguo zote na kulala pembeni ya kisima. Helena aliingia kisimani na kuchota maji kwenye kindoo kidogo na kukiweka majani mabichi, sikujua ya mti gani. Aliyaingiza ndani ya maji ya baridi na kuanza kunikanda mwili mzima huku nikizidi kutetemeka kwa baridi ya maji.


Eeeeheiyaaaa.... picha Linaanzia Hapa....Mzee Manoni hayuko hai tena.
Nini hatima ya Shija?
INAENDELEA.....
 
Back
Top Bottom