Nitagombea Urais - Kisandu Deogratius


Mwana siasa ni lazima awe na ngozi ngumu, sasa wewe jana tu leo umekurupuka kujitetea, ngoja kidogo. Hata hivyo si vibaya kujiridhisha, lakini kazi hiyo kama kwa bahati mbaya kweli utaipata hutaiweza. Furahisha baraza tu. Unafikiri Urais wa nchi ni ukatibu kata ama diwani? Ndugu yangu usipoteze nguvu nyingi katika hili wewe kajaribu ubunge, hata huo ubunge naona hutaupata pia.

Ushauri wa bure, wewe concentrate tu kwenye M4C, achana na mambo ya kugombea uongozi, muda bado mrefu sana. Sisi tutawatambua watu kwa matendo yao sio maneno.
 


Sasa kwa nini usisubiri kesho ndo ugombee.Sijakuelewa.TRASH
 
Naona anamwiga mtanga mwenzie Mr. Misosi. Nitoke vipi
 
Huyu mgombea wa urais kanistua kweli kweli! Dah! Yaani ana roho safi kama SARUJI!
 
Sisi tuko katika M4C, nyinyi wenzetu mko katika kugombea Uraisi, tuwaeleweje. Wagombea tuko wengi ila sasa tunatengeneza chama chetu ili mmoja wetu akiteuliwa ashinde. Hivi nyie mchango wenu katika chama ni nini. Mtueleze hata kabla ya huo uraisi.

Charity starts at home.
 
Kisandu hebu acha mambo yako ya utani utani bwana,tumeisha cheka inatosha,sasa nakupa ushauri kama kaka yako,CHADEMA kwa Kahama inapendwa sana lakini haijawahi kupata mgombea strong,huyu Lembeli ni Mwepesi sana sema hajapata mpinzani wa uhakika.Hebu jipange 2015 ukagombee ubunge Kahama,USIPOTEZE MUDA KUONGELEA KITU AMBACHO ROHONI UNAJUA NI NGUMU KAMA KUCHOTEA MAJI KWENYE PAKACHA,labda kama unataka uwekwe kwenye historia kama wakina DOVUTWA au MZIRAY kuwa uliwahi kugombea urasi basi.
 
Eti mkuu, akazane na M4C halafu tuone mchango wake. Tanga inamshinda, itakuwa Tanganyika?
 
Ni maumbile ya binadamu hatuwezi kuyakwepa kabisa! tuache maumbile ya kibinadamu yachukue asili yake!!! Kwani siku zote watu huvuja jasho,damu hata kupoteza maisha kutafuta mali, ukombozi, au mafanikio ya aina yeyote lakini mafanikio hayo yakishapatikana wanaokuja kufaidi ni wengine kabisa ambao hata ukiwauliza hicho wanachokifaidi sasa asili yake ni wapi hawajui.....!! Kwa maana hiyo hakuna haja ya kupoteza muda kuwakatisha tamaa wanaotaka kula mafanikio ya cdm waacheni kwani hayo ni maumbile ya mwanadamu.
 
Kikwete amafanya urais uwe rahisi kila mtu anatamani kwenda kutalii ulaya na kuvutwa na vitoroli kama jk,kweli hata mimi ninaweza kuwa amiri jeshi mkuu kha!
 
ILA SINA UHAKIKA NA HIYO ROHO YAKO MAANA UMESEMA NI NYEUPE KAMA SARUJI,SINA UHAKIKA HIYO SARUJI NI YA WAPI WAZO HILL AU TANGA CEMENT!!!! nadhani ulitaka kuandika Theluji!!! Au mmeku!!
 
Jamaa ameona akianza na kutaka kugombea URAIS atakuwa ameweka mazingira mazuri ya Ubunge. Jamaa kwanza ajiulize huko Tanga amefanya nini cha Maana cha kumpa ngumu za kuomba uraisi? Yaaani wanaume washinde Vijijini wakipiga M4C halafu wengine waje na matamko ya uraisi. Huu ni ujinga. Leo hii HECHE akisema anataka kugombea uraisi watu wengi sana watamwelewa,kwa sababu jamaa amehamishia makazi yake vijijini akifanya senstaization meeting. Sasa huyu MWEHU ashinde ofisini then aje na ngonjera za uraisi.
 
Mie Nasema kila siku kuwa Na shahada sio kuelimika watu wengine wanabisha Sasa oneni wenyewe..Na bado tutashuhudia mengi tu.. We ngojea muda uzidi kuyoyoma, urais, kila Mtu nataka kuwa rais . Aseeee mie nadhani katiba iruhusu kuwa Na marais Kama hamsini hivi at least kila angle rais.. Kabweka Wa kwamtogole anataka urais, mwatufileni wa mbambabey anautaka urais, Karoli wa magomeni naye anautaka, bado akina Bhasilisa, Budege, Punyetu, Mbano wote wanautaka huo urais, juzi hapa Yule mama Sofia wa Gongolamboto si kadai nae anauwania..

Hivi nani huyo anayegawia watu huo urais si awape tu, tunang'oana meno bure..Mtu akisema nataka kuwa rais Basi watu wanatetemeeeeeka Kumbe mwenzao anamaanishan rais wa shirikisho la vilabu vya pombe Za kienyeji, rais wa wabeba magunia sokoni, rais wa mchezo wa kujificha polipo, rais wa shoe-shine organizesheni, rais wa nanihii.. Soo many President.. Don't worry give them..

Lakini Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hatuwezi kuchagua Punguani Tena..!!
 
Utani na kazi. Hon.President and Commender in Chief Kisandu..Ku.

Ushauri wa Bure:
pamoja na kazi kubwa ya cdm kupitia M4c kuna haja ya kuwa na semina elekezi za safu za uongozi wa chama ngazi zote kutabainisha lengo la chama na mstabakali kwa ujumla towards 2015 !

Isije ikawa watu wanakaza misuli na M4C huku ndoto ni kupata vyeo na c ukombozi wa wanachi.

Tuyasikie tu kwa majirani kunakojengwa mitatandao. CDM needs internal politicisation much as required as mass mobilisation.

kujiunga na CDM tu haitoshi, ni kupewa pia elimu ya siasa ya chama na kuwa muumini.

chukua mfano mtu anapookoka, au kusilimu, haachwi bila mafundisho lukuki!

hii sio demokrasia kutangaza kila asubuhi kuwania uraisi kwa mtu aliyesrious na party cause!
 
Ningekuwa mimi ningetafuta kwanza wa "KUNIFUNDA"!

hovyoooooooooooooooooooooo!:A S embarassed:
 
Muacheni jamani aelezee anachokitaka. Hizo ndio ndoto zake! Time will tell.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…