Nitagombea Urais - Kisandu Deogratius

Nitagombea Urais - Kisandu Deogratius

[h=2]08 OCTOBER 2012[/h]Na Benedict Kaguo,Tanga

VITA ya kuwania urais mwaka 2015, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imezidi kushika kasi baada ya Katibu wa Baraza la Vijana (BAVICHA), mkoani Tanga, Bw. Deogratius Kisandu, kutangaza rasmi dhamira ya kuwania nafasi hiyo.

Uamuzi wa Bw. Kisandu kutaka kuwania nafasi hiyo, unaweza kuongeza mpasuko ndani ya CHADEMA, baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe, kutangaza kuwania nafasi hiyo hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga jana, Bw. Kisandu alisema Watanzania wanahitaji mabadiliko ambayo hayawezi kupatikana kama vijana makini hawatapewa nafasi.

“Nimefanya tathmini ya muda mrefu kabla sijatangaza uamuzi huu na kuiani kuwa, hakuna kiongozi mwenye dhamira na uwezo wa kuliongoza Taifa hili hasa wale wanaotoka katika nyadhifa mbalimbali za uongozi serikalini na bungeni.

“Mimi nimejitoa ili kuongoza mabadiliko haya na ninaweza kuwa Rais wa Tanzania, Watanzania wanahitaji kujua Kisandu ni nani, anafanya nini na malengo yake ni yapi kwa mustakabali wa nchi hii,” alisema Bw. Kisandu.

Alisema kwa muda mrefu wagombea urais wamekuwa wakitokea kwenye ubunge na Uwaziri lakini hicho si kigezo cha kupata viongozi hodari kwani wameonesha udhaifu mkubwa licha ya kupewa nafasi hizo.

“Ni wakati wa kuiga mfano ya Mwalimu Nyerere ambaye hakuwahi kuwa mbunge lakini aliweza kuongoza vyema Taifa letu, alipewa mamlaka makubwa ya kuongoza nchi akiwa hajawahi kushika madaraka makubwa serikalini lakini aliweza kuwaunganisha Watanzania na kupata uhuru wa kisiasa,” alisema.

Bw. Kisandu aliongeza kuwa, umefika wakati wa kufanya mageuzi ya kiuchumi ambapo kazi hiyo lazima iongozwe na Mtanzania mmoja na yeye yupo tayari kwani hajawahi kuwa mbunge wala Waziri zaidi ya uongozi ndani ya CHADEMA.

Alisema uwezo wa Mwalimu Nyerere kuongoza bila kupitia kada hizo ndicho kinachomfanya akumbukwe kwa ongozi wake ambao umetukuka hivyo wanasiasa wanaotokana na ubunge au Uwaziri hawastahili kupewa urais wa nchi.

“Nilidhani marais ambao wameliongoza Taifa letu wakiwa na uzoefu wa ubunge, Uwaziri kabla ya kupata Urais wangeweza kuiongoza nchi kwa ufanisi zaidi kushinda Mwalimu Nyerere.

“Badala yake wameonesha udhaifu mkubwa ambao unatupa tafsiri kwamba Taifa hili halihitaji kiongozi mwenye uzoefu mkubwa bali aliye na maono, uadilifu na hofu ya Mungu,” alisema Bw. Kisandu.

Alisema amejiandaa kisaikolojia kuwania nafasi hiyo na kuomba Watanzania wamuunge mkono ili kufanikisha dhamira ya kuleta ukombozi wa pili nchini baada ya ule aliofanya Mwalimu Nyerere kuwaondoa wakoloni na kupatikana uhuru.

Aliongeza kuwa, mwanasiasa yeyote mwenye kipaji na maono hawazi jana na leo bali anawaza jana, leo, kesho na kesho kutwa hivyo jambo la msingi ni kutazama ni jinsi gani tunaweza kupata ukombozi wa pili wa Taifa letu,” alisema.



 
Yaayi... I really don't know him... NO COMMENT !!!
 
KISANDU: SIJATUMWA NA CHAMA WALA NA ZITTO.

Baada ya tamko langu la kutaka kugombea urais la jana tarehe 8/10/2012 limeleta sura tofauti na mitazamo tofauti, wengine wakini chafua kwenye mitandao yakijamii na wengine hata kunipigia simu za kunipinga. Wapo wanaosema nimetumwa na CHADEMA ili kupunguza nguvu ya kaka ZITTO ili aonekane wa kawaida sana, wapo wanaosema nimetumwa na ZITTO ili kuendelea kumjengea mazingira, wapo walio sema mimi natoka kanda ya kaskazini na ni mkristu. Haya ni mitazamo ya watu isiyo fanyiwa utafiti kwa kile wanachokisema.

Hivi hii dhana ya mtu akiongea anachofikiri, watu wanasema katumwa, inatokana na nini? kwani mtanzania hawezi kusema mpaka atumwe? Nasema tena NITAGOMBEA URAIS na staacha mpaka kieleweke. Mimi sija tumwa na mtu nimetumwa na Mungu hivyo wamulaumu Mungu. Roho yangu ni kuonesha ukweli kuhusu upendo wangu kwa watanzania wenzangu. Roho ya Kisandu ni nyeupe kama saruji. Upendo wa Kisandu kwa watanzania ni kuwatumikia watanzania, nawashangaa wabunge vijana wanao sema eti vijana wasikurupuke. Wabunge wa aina hii hawawatakii mema watanzania maana hawapendi kuona rutuba ya vijana kama Kisandu tena mwenye uchungu na watanzania.
Mimi sitokei kanda ya kaskazini, nipo huko Tanga kikazi kwa nafasi yangu ya uongozi ndani ya chadema huko Tanga, ambako ndiko na elimu yangu ya chuo kikuu nilikoipatia kabla ya ile ya diploma ya elimu niliyo ipata pale chuo cha ualimu Tabora. Mimi nimzaliwa wa wilaya ya kahama, mkoani shinyanga, tena shule ya msingi mpaka sekondari nimesoma hukohuko. Labda kwasababu niligombea ubunge 2010 jimbo la lushoto(Tanga), wasome katiba vizuri wajue sifa za kugombea Ubunge.

Unajua kundi fulani linakereka sana kutaka kuwa mtumishi wa watanzania, usomi siyo kuvaa tai, suruali za vitambaa, suti au usharobaro bali ni kuhamasisha wananchi ili walete mabadiliko yenye maendeleo na sio kusifia ujinga unaosemwa na kila kiongozi unayemwamini.

Mimi na sikitika sana mtu anaponisema vibaya, ndio maana najiuliza maswali mawili, ni nani anayesema na kwanini anasema? Huenda nayeye si yeye na mimi naweza sema katumwa kuniharibia. Nasema tena hamuwezi kuzuia mipango ya Mungu isitimie, Urais nitagombea maana uhuru na maendeeo huhusiana kama kuku na yai lakini ukiweza kuwa na akili timamu, wakati kila mtu ameigizwa wazimu, wewe ni mtu maarufu. Wananchi watanzania wote wana akili timamu, uozo wa viongozi wao wanauona unaharufu mbaya sana na Plato aliwahi kusema “ uovu ni tokeo la kukosa maarifa” sasa viongozi wetu huenda wamekosa maarifa ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayodaiwa na wananchi silalamiki sana lakini nasema tu.

Ni fursa pekee sasa vijana kuikomboa Tanzania na kuepuka na ule upungufu usemao vijana ni taifa la kesho. Nasasa vijana ni Taifa la Leo.

Deogratius Kisandu
Katibu wa Baraza la Vijana wa chadema mkoa wa Tanga.
9 oktoba 2012

Mie sipingi wewe kuwa na nia ya kuwa Rais (I mean wa JMT). Ni jambo jema kabisa, Ila una uwezo wa kuwa Rais??? Koz hapo penye bluu ndo panaanza washa indicator jinsi ya umakini wako!!! Roho yako NYEUPE kama SARUJI..... Hahahaha, Vuta hand Brake shusha pumzi kisha keti!!!! Au Ulimaanisha THELUJI??? Go back home, Have shower, Re-arrange urself then come back as fresh as new may be Nitakuelewa.
 
Huyu mwandishi nadhani hajui vita! Namshauri aangalie video ya uvccm Mara!
 
Hivi kuna biashara gani ikulu hadi mtu upakimbilie? Kwa mtu mwaminifu na mwadilifu ikulu kwake ni mzigo, sio sehemu ya kupakimbilia. R.I.P Nyerere.
 
Ni haki yao ya kikatiba waacheni wajitokeze tena wawe wengi zaidi ili baadaye sisi wapiga kura tuje tukapembue vizuri mchele na pumba mbali mbali bila ajizi hata kidogo.

Yeyote anayesema eti kujitokeza kwa wagombea wengi ndani ya chama ni KUONGEZEKA KWA MIPASUKO huyo mtu hajui kitu katika siasa hivyo ni vema akaomba darasa rasmi toka kwa gwiji wa eneo hilo kote nchini; Prof Mwesiga Baregu ili akapate kuelimishwa zaidi.

Mti kutoa maua mengi kwenye kila tawi maani yake ni kwamba mti wenyewe tayari umemea katika ardhi yenye rutuba nyingi sana na maridhawa sana.

Cha msingi hapa tu ni juu yetu sisi wakulima wa mti huu ndio tulio na jukumu la kuamua tena kwa busara wa hali ya juu kwamba ni tawi lipi halina faida hivyo tukalikate na kunawirisha zaidi yale mengine stahiki ili kuja kuwa na mavuno mema zaidi na wala si matunda sumu.
 
Wewe Kisandu nawe mbona unapita mulemule ambapo tumepakataa kwa kaka Zitto? Hebu jenga kwanza chama alafu mda ukifika utajitokeza kugombea kwan haupo peke yako kwani hata prof.Safari na Prof.Baregu nao pia wanautaka urais sema kwa hekima yao wametulia kwanza.
 
.. anajipa tuu promo na kutafuta recognition kisiasa! bado mbaali sana
 
Kisandu hujakua kisiasa kwanza usijitangaze wewe kama ww manake kila mtu mwenye uongozi chadema akisema nitagomea itakuaje?
 
Poor kisandu, unatafuta umaarufu au? Tamaa ilimpoza fisi. 2nahtaj kujenga chama kwanza ndipo muanze kuropoka ***** wenu. I knw hm ver wel hawez k2.
 
Kutokana na CCM kudai mara kwa mara kuwa kijana huyu kisha maliza chuo aondoke Tanga na kuonekana bado yupo imekuwa ni kidonda kwa CCM. Lilipo ibuka zengwe la Dokta .Slaa kuwa na kadi mbili na yeye kuomba uchaguzi urudiwe, sasa CCM wakamtumia mwenyekiti wa mkoa wa CDM ili kumtoa Kisandu mkoani humo kupitia mzozo wa chama. Kwa taarifa mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Tanga akishirikiana na mwenyekiti wa chama wamepewa fungu na Majimarefu mbunge wa korogwe vijijini ili wahakikishe anatoka mkoani humo. Natayari mkutano wa kuwaita wenyeviti baadhi wa majimbo na posho zao umeshaandaliwa na utafanyika mapema mwanzoni mwa mwaka 2013. Kisandu unalo!!!!!
 
Mimi hata sielewi, maana umeanza vizuri mwishoni tena unasema, M/kiti wa Bavicha Mkoani Tanga akishirikiana na M/kiti wa chama amepewa fungu na Kisandu maana yake nini hapo?
 
ipo haja ya kuondoa viongozi wasaliti ndani ya chama chetu haraka kulinda maslah ya chama
 
Kutokana na CCM kudai mara kwa mara kuwa kijana huyu kisha maliza chuo aondoke Tanga na kuonekana bado yupo imekuwa ni kidonda kwa CCM. Lilipo ibuka zengwe la Dokta .Slaa kuwa na kadi mbili na yeye kuomba uchaguzi urudiwe, sasa CCM wakamtumia mwenyekiti wa mkoa wa CDM ili kumtoa Kisandu mkoani humo kupitia mzozo wa chama. Kwa taarifa mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Tanga akishirikiana na mwenyekiti wa chama wamepewa fungu na Majimarefu mbunge wa korogwe vijijini ili wahakikishe anatoka mkoani humo. Natayari mkutano wa kuwaita wenyeviti baadhi wa majimbo na posho zao umeshaandaliwa na utafanyika mapema mwanzoni mwa mwaka 2013. Kisandu unalo!!!!!
Who is Kisandu?

Kafukuzwa lini, na nani, na kwaninini huko CHADEMA?

Je Yeye naye alikuwa kundi la ''Misukule ya Zitto'' linalofugwa na CCM linalokesha kuimba wimbo wa Nape wa Kadi ya CCM isiyorudishwa?
 
Mimi binafsi simuamini Kisandu kwani kadri ninvyomsoma kwenye mitandao ya kijamii anavyoandika na ku comment dhidi ya uongozi wa Chadema taifa sitegemei kwamba anaweza kuwa tishio kwa ccm bali yeye ni kipenzi chao, ni gamba lililo ndani ya gwanda.

Labda mleta mada unataka kuhadaa watu kwakuwa mahali alikofikia Kisandu, akifukuzwa ndani ya chama ama kuvuliwa ukatibu wa Bavicha mkoa wa Tanga itakuwa ndio afya kwa ustawi wa chama mkoani Tanga.
 
Back
Top Bottom