Nitagombea Urais - Kisandu Deogratius

Nitagombea Urais - Kisandu Deogratius

YEYOTE ANAYETEKENYWA NA KUSUMBULIWA SAAAANAA MOYONI MWAKE NA NDOTO ZA KUTAMANI KUWA MPANGAJI WA JUMBA LA TAIFA PALE MAGOGONI KWANZA AKAJIPEMBUE MWENYEWE KWA MISINGI HII

Kijana uko makini na unajua sana pia KUJENGA HOJA zenye mashiko na zenye kuweza kupenyeza katika akili za SERIOUS persons of this country.

Before I could objectively comment on your good aand constitutionally justified intents of providing leadership to our beloved nation, let me make a leap into any nearby forest (kuingia msituni) and do some basic overview of who you are and even seek to consult historical background so that the shades in there could tell me exactly you may have been standing for in life and get assurance whether if given an opportunity you can possibly remain steadfast without suddenly migrating into some people's pockets like we presently see of some 'politically fallen renowned soldiers' of our times around.

Mpaka sasa hivi labda tukupe benchi ukasubirie hapo sebuleni kwenye jumba hili la 'DEMOKRASIA YA USHINDANI WA KISIASA' huku tukijaribu kutafuta taarifa juu yako kama vile:

(1) Uwezo wa kufanya kazi na wenzio kama mwana-timu,

(2) Msimmo Usioyumba katika mambo ya msingi,

(3) Uwezo wa kujikinga na kimbunga cha UFISADI,

(4) Kwa namna gani umeweza kuwa SAUTI KAMILI kwa sehemu ya jamii yetu wasiokua na nafasi wala pa kusemea kero moyoni,

(5) Kutizama walau Ripoti ya vipindi vitatu mfululizo ambazo mtendaji mkuu wa chama chako (kwa hapa ni maoni ya Dr Slaa wa CHADEMA) juu ya UTENDAJI KAZI wako kwa jamii,

(6) Tutatafuta pia kuelewa kwamba wewe ni aina ya kiongozi unayefuata utaratibu wa USHIRIKISHWAJI WANANCHI katika shughuli zinazowahusu au ni yule mwenye kutoka na 'MAAMUZI YAKE BINAFSI CHUMBANI' na kisha kutafuta kutandaza usahihi wake kwa umma wapende wasipende,

(7) Mpango mahususi ulionao na uchambuzi wa wazi kabisa juu ya jinsi gani utakavyoweza kufanya ki-mkakati kuhakikisha ya kwamba hayo maono yako kweli unafanikiwa kuyageuza kuwa MATUNDA MARIDHAWA (na wala si matunda SUMU) kwa taifa letu.

(8) Jinsi gani unavyochukia UDINI na ubaguzi mwingine wowote ule na jinsi gani utakavyohakikisha kwamba kovu hilo linapona kimoja,

(9) Kusudio lako likoje katika KULINDA RAIA NA MALI ZAO, WATU WENYE MAWAZO HURU katika masuala mbalimbali kuhusu taifa letu kutokuchinjwa kila leo kama hivi sasa na jeshi lao wenyewe la polisi kwa maslahi ya wachache.

(10) .... na mengineo mengi tu.

NB: Mwisho, naomba nitoe angalizo kali hapa kwamba kwa uchaguzi kwa mara ya kwanza WaTanzania KAMWE HATUTOTAFUTA KUCHAGUA:

(i) Sura za watu,

(ii) hatutomchagua yeyote kwa misingi ya MWENZETU,

(iii) kamwe hatutomchagua mtu kwa UMAARUFU WA VYEO ALIVYOWAHI KUVISHIKA huko nyuma,

(iv) Kamwe HATUTODANGANYIKA KUCHAGUA mtu eti tu kwa misingi ya UKUBWA AU UCHANGA WA UMRI wake tu,


NITAGOMBEA URAIS

Watanzania wanahitaji MABADILIKO na MABADILIKO haya hayawezi kuja bila Watanzania KUAMUA. Na bila Mtanzania mmoja kujitoa kuongoza MABADILIKO haya, na mimi ni mmoja wao. Nimedhamiria, ninaweza kuwa raisi wa Tanzania leo, kesho au keshokutwa. Watanzania wanahitaji kujua KISANDU Deogratius ni nani?Anafanya nini na ana malengo gani kwa mustakabali wa Taifa la Tanzania.

Mwalimu Nyerere alipewa mamlaka makubwa ya kuongoza nchi yetu akiwa hajawahi kushika madaraka makubwa serikalini kama Uwaziri (kabla ya uhuru), na wala hajawahi kuwa Mbunge lakini aliweza kuwaunganisha watanzania na kupata uhuru wa kisiasa. Sasa ni wakati wa kufanya mageuzi ya kiuchumi. Kazi hii lazima iongozwe na Mtanzania Mmoja na mimi ni mmoja wao ambaye sijawahi kuwa Mbunge wala Waziri zaidi ya uongozi ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Tulidhani Marais ambao wameliongoza Taifa letu wakiwa na uzoefu wa Ubunge, Uwaziri n.k. kabla ya kupata nafasi ya Urais wangeweza kuliongoza Taifa hili kwa ufanisi zaidi kushinda Mwalimu Nyerere lakini badala yake wameonyesha udhaifu mkubwa ambao unatupa tafsiri kwamba taifa hili halihitaji kiongozi wenye uzoefu mkubwa bali kiongozi mwenye maono, umakini, uadilifu na hofu ya Mungu.

Mwanasiasa yoyote mwenye kipaji na maono hawazi jana na leo, anawaza jana, leo, kesho, keshokutwa na mtondogoo n.k. Jambo la msingi ni kutazama ni kwa jinsi gani tunaweza kupata UKOMBOZI WA PILI WA TAIFA LETU.

NIMEDHAMIRIA, NINAWEZA, Nitagombea Urais

Deogratius KISANDU
Katibu Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA)
Mkoa wa Tanga


3 Octoba 2012
 
hongera DEO! katika yote ninayoweza kukusifia ni kwamba walau umeweza kutikisa kurasa za magazeti na mitandao ya kijamii. hii ni hatua kubwa na yenye mafanikio makubwa kwako kwa mwaka huu. big up br! jipange tena vizuri zaidi mwaka ujao.
 
Raisi wangu kipenzi dr slaa wewe tulia tu.acha hawa vijana warusherushe mateke na kutafuta publicity.
Najua adolescence ndio inawasumbua.
Dr slaa your my hero....
 
... pindi ninapomsikia mtu mzima na msomi sana kama Prof Lipumba anapojinadi kuwania urais eti kwa njia ya KUHIMIZA SEHEMU YA WATANZANIA WAKAJIBAGUE KWA KOFI TU LA UISLAMU WAO (eti Wa-Islamu kapiganieni haki zenu mpaka kieleweke), hadi hapo wala sihitaji maoni ya waheshimiwa kama vile Joseph Sinde Warioba, Salim Ahmed Salim, Dr Hassy Kitine wala Mzee Edwin Mtei KUNITAANGAZIA KWAMBA PROF LIPUMBA tayari kafilisika kupindukia katika siasa za Tanzania.

Mbaguzi kama huyu Prof Lipumba kamwe HATUIFAI katika kiti cha uongozi wa nchi kama rais ila bado ni mtu wa muhimu sana kule katika korido zetu za kitaaluma kule mashuleni kama vile Mlimani.
 
Hivi hii dhana ya mtu akiongea anachofikiri, watu wanasema katumwa, inatokana na nini? kwani mtanzania hawezi kusema mpaka atumwe? Nasema tena NITAGOMBEA URAIS.
Umeshatoa maoni kwenye katiba mpya kwamba umri wa mgombea Urais uwe chini ya 40? Vinginevyo wewe na mwenzio aliyetangaza wote wahuni, mtakuwa mmekula dili na Tume ya Katiba nini?
 
Katika hizi Post zenu kuna hoja mmeijadili??
Mkuu, me huwa nawashangaa baadhi ya jamaa wa hapa jamvini, mtu humfahamu, hajawahi kumwona na pengine hawataonana wala kufahamiana hadi Yesu atakaporudi. Halafu wanarumbana, wanagombana, wanatukanana hata kupelekea kupigwa BAN. Haina maana kabisa, bora wangekuwa wanarumbana kwa hoja na siyo hii ya kuficha busara ya mtu binafsi!!!!
A%20S-confused1.gif
 
KISANDU: SIJATUMWA NA CHAMA WALA NA ZITTO.

Baada ya tamko langu la kutaka kugombea urais la jana tarehe 8/10/2012 limeleta sura tofauti na mitazamo tofauti, wengine wakini chafua kwenye mitandao yakijamii na wengine hata kunipigia simu za kunipinga. Wapo wanaosema nimetumwa na CHADEMA ili kupunguza nguvu ya kaka ZITTO ili aonekane wa kawaida sana, wapo wanaosema nimetumwa na ZITTO ili kuendelea kumjengea mazingira, wapo walio sema mimi natoka kanda ya kaskazini na ni mkristu. Haya ni mitazamo ya watu isiyo fanyiwa utafiti kwa kile wanachokisema.

Hivi hii dhana ya mtu akiongea anachofikiri, watu wanasema katumwa, inatokana na nini? kwani mtanzania hawezi kusema mpaka atumwe? Nasema tena NITAGOMBEA URAIS na staacha mpaka kieleweke. Mimi sija tumwa na mtu nimetumwa na Mungu hivyo wamulaumu Mungu. Roho yangu ni kuonesha ukweli kuhusu upendo wangu kwa watanzania wenzangu. Roho ya Kisandu ni nyeupe kama saruji. Upendo wa Kisandu kwa watanzania ni kuwatumikia watanzania, nawashangaa wabunge vijana wanao sema eti vijana wasikurupuke. Wabunge wa aina hii hawawatakii mema watanzania maana hawapendi kuona rutuba ya vijana kama Kisandu tena mwenye uchungu na watanzania.
Mimi sitokei kanda ya kaskazini, nipo huko Tanga kikazi kwa nafasi yangu ya uongozi ndani ya chadema huko Tanga, ambako ndiko na elimu yangu ya chuo kikuu nilikoipatia kabla ya ile ya diploma ya elimu niliyo ipata pale chuo cha ualimu Tabora. Mimi nimzaliwa wa wilaya ya kahama, mkoani shinyanga, tena shule ya msingi mpaka sekondari nimesoma hukohuko. Labda kwasababu niligombea ubunge 2010 jimbo la lushoto(Tanga), wasome katiba vizuri wajue sifa za kugombea Ubunge.

Unajua kundi fulani linakereka sana kutaka kuwa mtumishi wa watanzania, usomi siyo kuvaa tai, suruali za vitambaa, suti au usharobaro bali ni kuhamasisha wananchi ili walete mabadiliko yenye maendeleo na sio kusifia ujinga unaosemwa na kila kiongozi unayemwamini.

Mimi na sikitika sana mtu anaponisema vibaya, ndio maana najiuliza maswali mawili, ni nani anayesema na kwanini anasema? Huenda nayeye si yeye na mimi naweza sema katumwa kuniharibia. Nasema tena hamuwezi kuzuia mipango ya Mungu isitimie, Urais nitagombea maana uhuru na maendeeo huhusiana kama kuku na yai lakini ukiweza kuwa na akili timamu, wakati kila mtu ameigizwa wazimu, wewe ni mtu maarufu. Wananchi watanzania wote wana akili timamu, uozo wa viongozi wao wanauona unaharufu mbaya sana na Plato aliwahi kusema “ uovu ni tokeo la kukosa maarifa” sasa viongozi wetu huenda wamekosa maarifa ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayodaiwa na wananchi silalamiki sana lakini nasema tu.

Ni fursa pekee sasa vijana kuikomboa Tanzania na kuepuka na ule upungufu usemao vijana ni taifa la kesho. Nasasa vijana ni Taifa la Leo.

Deogratius Kisandu
Katibu wa Baraza la Vijana wa chadema mkoa wa Tanga.
9 oktoba 2012
 
haya sasa, kumekucha cdm.
Wapi mzee mtei na wapambe wake kina malemo waje kumtetea mbowe?
Hiyo ndio demokrasia, uhuru wa maoni sio kila mwenye mtazamo tofauti anakuwa adui.
 
Mungu ni mkubwa na uwezo wake haufananishwi na kitu chochote.
Natumaini kweli umetumwa na Mungu kwa kuwa mipango yake hudhihirika pasipo vificho.
 
Ubunge tu wenyewe inaonekana ulishindwa utaweza kupata kura za urais??
 
ni haki yako japo sijajua unagombea urais wa nini TFF? chuo? Au club
 
sio kila kitu utumwe na mtu,yaweza kuwa ulitumwa na pepo.maana hata ubunge tu umekushinda unataka urais.si bora tumchague lowasa,tamko lako lenyewe haliko strait kona kibao,sasa unataka tukupe nchi wewe,au una unataka urais wa tff???
 
anatafuta sifa tu huyu...jk ameifanya hii taasisi kuwa bure kabisa,.kila mtu sasa anatangaza kuutaka urais
 
Katika demokrasia kila mtu ana uhuru wa kusema chochote ili mradi havunji sheria hivyo sioni ubaya wa kijana kusema anachoamini.
 
... mkuu inatoshaaaa!!!!!!!

Kugombea urais sasa ndio imekua wimbo wa kila leo kuanzishia thread kumi kumi kila siku mtandaoni. Ulianza vizuri lakini sasa wajipunguzia ladha mwenyewe.

Tumeshasikia kwamba bKisandu anawiwa moyoni kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo anatarajia kuja kutuomba sisi wapiga kura kumfikiria katika mchepuo huo katika maisha.

Na sisi huku tunasema tunawahitaji Kisandu wengi zaidi wajitokeze ili nafasi yetu ya kikatiba kuchagua iwe mpana zaidi na zaidi bila kugeuzwa nongwa na wimbo wa kila leo mtandaoni.

Lulu ya taifa na nuru mpya ilibahatika kuzaliwa katikati yetu katika karne hizi Ndugu Kisandu, RUKSA KWAKO KAGOMBEE kitu chochote kile mkuu; hebu kawasalimie waheshimiwa wapiga kura wako watarajiwa tuliojaa tele hapa nje.
 
Back
Top Bottom