Baba Clara
Member
- May 10, 2011
- 94
- 27
NITAGOMBEA URAIS
Watanzania wanahitaji MABADILIKO na MABADILIKO haya hayawezi kuja bila Watanzania KUAMUA. Na bila Mtanzania mmoja kujitoa kuongoza MABADILIKO haya, na mimi ni mmoja wao. Nimedhamiria, ninaweza kuwa raisi wa Tanzania leo, kesho au keshokutwa. Watanzania wanahitaji kujua KISANDU Deogratius ni nani?Anafanya nini na ana malengo gani kwa mustakabali wa Taifa la Tanzania.
Mwalimu Nyerere alipewa mamlaka makubwa ya kuongoza nchi yetu akiwa hajawahi kushika madaraka makubwa serikalini kama Uwaziri (kabla ya uhuru), na wala hajawahi kuwa Mbunge lakini aliweza kuwaunganisha watanzania na kupata uhuru wa kisiasa. Sasa ni wakati wa kufanya mageuzi ya kiuchumi. Kazi hii lazima iongozwe na Mtanzania Mmoja na mimi ni mmoja wao ambaye sijawahi kuwa Mbunge wala Waziri zaidi ya uongozi ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Tulidhani Marais ambao wameliongoza Taifa letu wakiwa na uzoefu wa Ubunge, Uwaziri n.k. kabla ya kupata nafasi ya Urais wangeweza kuliongoza Taifa hili kwa ufanisi zaidi kushinda Mwalimu Nyerere lakini badala yake wameonyesha udhaifu mkubwa ambao unatupa tafsiri kwamba taifa hili halihitaji kiongozi wenye uzoefu mkubwa bali kiongozi mwenye maono, umakini, uadilifu na hofu ya Mungu.
Mwanasiasa yoyote mwenye kipaji na maono hawazi jana na leo, anawaza jana, leo, kesho, keshokutwa na mtondogoo n.k. Jambo la msingi ni kutazama ni kwa jinsi gani tunaweza kupata UKOMBOZI WA PILI WA TAIFA LETU.
NIMEDHAMIRIA, NINAWEZA, Nitagombea Urais
Deogratius KISANDU
Katibu Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA)
Mkoa wa Tanga
3 Octoba 2012Deogratius KISANDU
Katibu Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA)
Mkoa wa Tanga