Nisome nini chuoni mwaka huu 2025?

Nisome nini chuoni mwaka huu 2025?

Nina 400k hapa Daslam. Njoo tuangalie tunafanyaje ili kuizalisha kiwango cha kuendesha maisha ya kila siku

Hata mimi huko University nilipita tena under artecture engineering, sasa hivi niko huku Kawe nafukunyua vifusi
 
Tuliza wenge subiri matokeo yatoke . Usije tu ukashangaa umelamba div 3 ya 14
Dah we jamaa 😂😂 mbona sijawahi kufikiria kuwa nitapata Division 3 😂😂
Najua nilichokiandika siwezi pata Division 3 wala 2
Tatizo usipojua cha kusoma sasahivi maana yake utahangaika kwenye ku apply chuo siku matokeo yakitoka. Yani inabidi dirisha linapofunguliwa hapohapo ni apply course fulani chuo fulani mapema bila kuchelewa
That's why najiandaa sahiz nataka siku matokeo yakitoka niwe na final saying tayari
 
Dah we jamaa 😂😂 mbona sijawahi kufikiria kuwa nitapata Division 3 😂😂
Najua nilichokiandika siwezi pata Division 3 wala 2
Tatizo usipojua cha kusoma sasahivi maana yake utahangaika kwenye ku apply chuo siku matokeo yakitoka. Yani inabidi dirisha linapofunguliwa hapohapo ni apply course fulani chuo fulani mapema bila kuchelewa
That's why najiandaa sahiz nataka siku matokeo yakitoka niwe na final saying tayari
Nyie ndio mnaojinyonga , mtihani unavyuona na marking scheme inavyotaka huenda ni tofauti mwisho wa siku unaangukia pua.

Hata hao ambao matokeo yao wame differentiate constant walikuwa na tumaini kama lako.

Hata TCU guide book sidhani kama imetoka , wenge la nini sasa?

Maana course husika inategemea capacity wanayoitaka na ufaulu wa mwaka husika kulinganisha na wa kwako.
 
Nyie ndio mnaojinyonga , mtihani unavyuona na marking scheme inavyotaka huenda ni tofauti mwisho wa siku unaangukia pua.

Hata hao ambao matokeo yao wame differentiate constant walikuwa na tumaini kama lako.

Hata TCU guide book sidhani kama imetoka , wenge la nini sasa?

Maana course husika inategemea capacity wanayoitaka na ufaulu wa mwaka husika kulinganisha na wa kwako.
Sawa
 
Wakuu mimi ni mkazi wa Lindi nimesoma PCM shule moja uboizini huko Mbeya na nimemaliza mtihani wa taifa siku chache tu zilizopita. Hapa bado nawaza niende JKT au nipumzike home hii miezi kadhaa

Kwa nilivyofanya mtihani najua nitapata Division 1 ya point 6 hadi 8.
Sasa kuna Jambo linanitatiza hususani kwenye hii era ambayo ajira hakuna. Naomba ushauri kwa JF Experts.
Vyuo ninavyotamani kusoma ni
  • University of Dodoma
  • Dar es Salaam Institute of Technology
  • National Institute of Transport
  • Dar es Salaam Maritime Institute
  • Mbeya University of Science and Technology
  • Muhimbili University of Health and Allied Sciences
UDSM na MUHAS napapenda ila nasikia cutting point zao ni kubwa Sana

Sasahivi walimu wetu wanatuambia kuwa Biomedical Engineering ina soko ila kama ukipata ufaulu chini ya Division 1 ya 5 hupati chance ya kusoma hiyo kozi

Kwa hiyo huwa nawaza sana nisome kozi ipi ambayo ina nafasi kubwa ya kupata ajira au kujiajiri at least ukilinganisha na kozi nyingine

Watu wengine wanasema Computer Engineering ina soko, hivi ni kweli wakuu au ndo tunaingizana cha kike?

Kozi nyingine ninazowaza ni
  • Mechanical Engineering
  • Automotive Engineering
  • Electrical Engineering
  • Chemical Engineering
  • Mechatronics Engineering
  • Telecommunications Engineering

Kweli napenda Engineering ila sijui hata ipi inahitajika kwa Bongo ipi haihitajiki. Nimesoma thread nyingine nyingi ila bado sijapata majibu. Kuna muda nawaza niachane na Engineering labda nisome Accounting and Finance au Agricultural Science pale SUA ila nahisi watu wa Accounting ni wengi sana. Ajira zitakuwa ngumu mbeleni (sijui ila ninahisi tu)

Au nisome "Mechanical Engineering" Halafu nikatafute kazi JWTZ maana walisema ni kozi adimu na inahitajika jeshini. Au sijui nisome Automotive Engineering kwenye magari au hata treni nione kama ina tija 🥲

Nikisikia na watu wa mtaani wanavyotutisha kuhusu maisha ya mtaani yalivyo magumu ndo nachanganyikiwa kabisa. Hizo habari zinafanya nakosea hadi raha. Au niende chuo nikasome kwa bidii sana nipate GPA kubwa nione kama naweza kuwa lecturer. Nawaza mengi ila bado Niko njia panda Sana.

Naombeni ushauri wakuu nikasome nini chuo. Kozi yoyote Ile nzuri yenye soko la ajira Tanzania hata kama ni ngumu fresh tu, kupiga msuli naweza maana nina hamu sana na ajira.
Naombeni mawazo yenu wakuu
Upepo wa Pesa

Wewe binafsi unapenda course ipi kati ya hizo ulizotaja ?
 
Soma Political Science and Public administration,PSPA ,ukimaliza tu unakuwa Mbunge,unaanza na Salary ya 18M kwa mwezi,unapewa posho kila kikao 400+,unapewa gari na dereva ,Lakini uwe mzalendo pigania nchi yako
 
Nilikuwa nawaza hivyo ila juzi niliona taarifa ya habari wanasema "VIJANA WALIOHITIMU JKT WAPEWA SOMO WAACHE KUTEGEMEA KUAJIRIWA JWTZ BADALA YAKE WAJITEGEMEE"
Hii habari ikanitisha kidogo kuwa huenda imekuwa kero huko JKT kila mtu anataka kubaki hadi JKT inaamua kuingilia kati kuwatoa matumaini hayo
JkT ingeangaliwa upya ikafumuliwa na kuweewa mazingira mazuri hata mtu asipobaki kule atoke na kitu

Tunapeleka vijana wengi sana JKT ila wanaobaki kupata ajira ni sehemu tu mbaya zaid ule mfumo wa ajira zetu za Majeshi yote kupitia JKT ndio umeharibu zaidi madogo wengi wanarud Nyumban baada ya miaka mi2 hadi mi3 yakukaa kule kambini

Kwangu mimi ningependekeza yafuatayo itungwe sheria Askari wote wa vyombo vya ulinzi na usalama kupitia JkT iwe lazima sio Ombi

Kule Jkt iwepo miezi 4 mafunzo ya kijeshi afu miaka miwili au mitatu mtu anajifunza Fani kama VeTA vile na kupewa Cheti kabisa ili akikosa ajira hata za majeshi ataajiriwa hata na Halmashauri, Taasisi mbalimbali hata idara mbalimbali au atajiajiri

Mtu kasoma hadi kidato cha 6 akaharibu matokeo yake yakaw sio mazuri anaenda JkT anakaa miaka mi2 hadi mia3 anatoboa mkataba unamrudisha Home hapo unakuta na elimu ya kidato cha 4/6 kashavuka miaka 25 akirud kutafuta ajira za vyombo vingine vya usalama haajiriki kwa kigezo tu kavuka 25 y_O hapohapo hana fani yoyote tuseme angeweza omba hata Idara ya msji huko
 
Nenda DIT pale utatoka fit sana kwenye kozi zao!!

Iwe electrical, computer au civil engineering utakua POA man!!

Acha kusomea kazi za kuchomekea na kupuliza unyunyu u ta be disappointed!!
 
Luca Paguro
Umekaza mzuri vizuri A level hongera kwa ufaulu mzuri.

Tanzania yetu haijawai kueleweka kwenye swala zima la ajira, hakuna kozi yenye matarajio mazuri ya ajira kwani kila kukicha watawala wetu wanabadilisha sera na mifumo ya elimu na ajira.

Nakushauri, Kipindi cha kupata mafunzo ya JKT usikose kuwepo humo, mafunzo yatakapoisha jitahidi ubaki hapo. Tengeneza ukaribu na hao wanajeshi mpaka wakuchukue engineering zako utasomea humo na ukiwa na ajira yako kam jwtz.
 
Back
Top Bottom