Nisome nini chuoni mwaka huu 2025?

Nisome nini chuoni mwaka huu 2025?

Nenda DIT, piga IT, au, electrical,
Mdogo wangu ilibidi ujue mapema haya Mambo, mi nilipanga kusomea, uhandisi, nikiwa darasa, LA saba!
Kozi, yoyote,inakutoa, kwa, maisha, ya, sasa, hata, kama, una degree ya kitu Fulani, ongeza hata ujuzi wa kupiga picha, music production, kupiga, rangi,kuchomelea, kitu chochote cha ufundi we jifunze tu
Asante kwa ushauri
 
Ukisoma kozi kwa sababu ina soko utakuja kupata nsobgo wa mawazo baadae. Hizo kozi unasema zina soko leo fikiria miaka 4 au mitano baada ya wewe kumaliza chuo. Je zitaendelea kuwa na soko? Bila shaka soko linakuwa limebadilika.

Nadhani swala la muhimu ni kuangalia passion yako na utayari wa wewe kuitumia hiyo kozi maishani. Suala la Ajira linabadilika sana. Kuna kipindi niko sekondari Telecom Ilikuwa kozi matata sana. Lakini namaliza form six ikawa Petroleum, ila tulipomaliza chuo waliosoma petroleum wakjikuta mtaani
Uzi ufungwee.
 
Wanangu wawili wamemaliza kozi hizo bado wapo mtaani wanahangaikia ajira mwaka wa tatu huu.

Siku hizi hakuna ajira iliyo wazi kwamba ukimaliza straight forward mzigoni.

Kozi yoyote unayosoma unasota kweli kweli halafu ukija mtaani unasota tena kupambania ajira.

Waulize madaktari kama kuna ajira za moja kwa moja siku hizi ndipo utapata majibu ugumu wa ajira ulivyo kwasasa.
Mmh.. Ni kweli Agricultural Engineering hakuna ajira nako
 
Ungekuwa na hela ungetafuta chuo duniani kinachotoa degree ya blockchain technology na issue za cryptocurrency maana ndipo uelekeo dunia ilipo.
kama hiyo option ya 1 ngumu kuwezekana ningekuwa wewe ningesoma computer science/engineering baadae ningesoma hizo field nilizomention hapo juu plus cyber security
Kuna chuo cha kinaitwa Parul University, kipo Vadodara, Gujarat (India) hiyo course wanayo ila Ada per semester ni 2100USD ambayo kwa mwaka moja (semester mbili) ni 4200USD sawa na milioni 11 kwa mwaka. Hostel zao bei ni 1200USD kupanda.
Sasa bora Parul vyuo vingine vya nje bei zake ni za moto. Kweli hivyo vyuo sitaviweza
 
Kama unataka usiangaike na ajira means hata ukitoka chuoni unaweza kupata sehemu ya kujishikiza kasome electrical engineering hii ukiwa nayo Mtaani huwezi lala njaa!! Lakini kama unataka kusubiri mpaka ajira soma mechanical engineering au Mechatronics engineer hizi kozi Zina soko japo Kuwa watu ni wengi sana so competition ni kubwa mno unaweza ukasota mno.

Kuhusu Biomedical engineering hii course naweza kusema ni course ambazo zimeletwa kisiasa kama zile sijui Petroleum engineer, Marine engineer Bsc. Of Biological nk ni course kwa Bongo hapa hazina access za ajira zimeletwa kwa Siasa za bongo tu lakini upatikanaji wake wa ajira ni mgumu sana hata upande wa masomo yake kwa vitu vingi hamfundishwi mnakula theory kwa sababu hamna vifaa vya kutosha.

Kwa Tanzania course ambayo Ina ajira ambayo ukimaliza unaenda Moja Kwa Moja kufanya kazi na unaajiriwa ni Aircraft Engineering hii inatolewa pale NIT ada yake ni 6M kama upo vizuri kasome hii kozi maana ajira zake ni uhakika Asilimia 100.

Point to note: unapo chagua course zingatia chuo mfano kwa upande wa Engineer DIT is the best lakini mazingira yake ya kuishi ni magumu mno. kwa DSM chuo ambacho mazingira yake ni mazuri kwa kuishi na Elimu yake ni nzuri ni NIT tu huko utapata vyumba vya kupanga misosi kwa 1000 tu unakula unashiba tofouti na vyuo vingine.

Kila la kheri.
DIT na NIT sio vyuo, ni taasisi.
 
Nilikuwa nawaza hivyo ila juzi niliona taarifa ya habari wanasema "VIJANA WALIOHITIMU JKT WAPEWA SOMO WAACHE KUTEGEMEA KUAJIRIWA JWTZ BADALA YAKE WAJITEGEMEE"
Hii habari ikanitisha kidogo kuwa huenda imekuwa kero huko JKT kila mtu anataka kubaki hadi JKT inaamua kuingilia kati kuwatoa matumaini hayo
Kwanza hii ya kusema wanabaki na kusomeshwa na jeshi, naona km haiko ktk ukubwa huo.
Kunae jamaa nilikua nae Coy 1, yeye alipata 1 ya 7 PCM alitaka kubaki pale, mbna alikataliwa, sio wote wanabaki na kukubaliwa.
 
Hii inaonesha jinsi Gani familia na watanzania tulivokuwa hatuna maono Wala mwelekeo wa maisha.

Hadi unaenda PCM ulikuwa hujui unataka kusoma kitu Gani au kuwa nani?. Sad!!

Kuna haja ya kuwa na carrier counselling mashuleni.

For me, Tele au Computer engineering inafaa (cyber security)

Kutokana na Dunia inakoenda.

All in all, there must be an inner voice that talks to you about a certain course, please listen to it and go for it, because that is where your destiny will shine. Huku kwingine na maushairi utapoteana Bure mdogo wangu.
Mkuu sisi tangu tupo la kwanza tunafundishwa tu mambo ya darasani sio ya nje mpaka tunafika form 4 hivyo hivyo. Muda wa kukaa mtaani ni kipindi cha likizo tu tunashindwa kujua mitaani mambo yakoje.
Unachosema ni kweli. Inabidi kuwa na darasani la ajira mashuleni la sivyo wengi tutaangamia

Tena wazazi wangu walinikaririsha niwe daktari since nipo mdogo hadi namaliza form 4 nikapata Division 1 ya 8 wakawa wananishinikiza niende PCB, binafsi nikawakubalia kinafika ila nilipoenda shule nikubali na PCM niliyokuwa nataka

Originally nilikuwa napenda "Mining Engineering" ndio maana nimeenda PCM ila baada ya kushika watu wengi wanasema kwa Bongo hiyo kozi ni kupoteza muda maana madini wananufaika watu wa nje tu mi nikaikatia tamaa ndo nipo natafuta alternative
 
Kama unataka usiangaike na ajira means hata ukitoka chuoni unaweza kupata sehemu ya kujishikiza kasome electrical engineering hii ukiwa nayo Mtaani huwezi lala njaa!! Lakini kama unataka kusubiri mpaka ajira soma mechanical engineering au Mechatronics engineer hizi kozi Zina soko japo Kuwa watu ni wengi sana so competition ni kubwa mno unaweza ukasota mno.

Kuhusu Biomedical engineering hii course naweza kusema ni course ambazo zimeletwa kisiasa kama zile sijui Petroleum engineer, Marine engineer Bsc. Of Biological nk ni course kwa Bongo hapa hazina access za ajira zimeletwa kwa Siasa za bongo tu lakini upatikanaji wake wa ajira ni mgumu sana hata upande wa masomo yake kwa vitu vingi hamfundishwi mnakula theory kwa sababu hamna vifaa vya kutosha.

Kwa Tanzania course ambayo Ina ajira ambayo ukimaliza unaenda Moja Kwa Moja kufanya kazi na unaajiriwa ni Aircraft Engineering hii inatolewa pale NIT ada yake ni 6M kama upo vizuri kasome hii kozi maana ajira zake ni uhakika Asilimia 100.

Point to note: unapo chagua course zingatia chuo mfano kwa upande wa Engineer DIT is the best lakini mazingira yake ya kuishi ni magumu mno. kwa DSM chuo ambacho mazingira yake ni mazuri kwa kuishi na Elimu yake ni nzuri ni NIT tu huko utapata vyumba vya kupanga misosi kwa 1000 tu unakula unashiba tofouti na vyuo vingine.

Kila la kheri.
Hiyo Aircraft & Maintenance Engineering nimeingia page ya NIT sasahivi kweli Ada ni milioni 6. Ni hela kubwa kwa familia yetu ila kama nikipata mkopo wa 50% hiyo milioni 3 wazazi wangu wanaweza kuimudu
Ngoja nianze kufuatilia hiyo kozi mkuu. Ahsante
 
Kwanza hii ya kusema wanabaki na kusomeshwa na jeshi, naona km haiko ktk ukubwa huo.
Kunae jamaa nilikua nae Coy 1, yeye alipata 1 ya 7 PCM alitaka kubaki pale, mbna alikataliwa, sio wote wanabaki na kukubaliwa.
Duh ila kweli hata Mimi nawaza hivyo sidhani kama kubaki ni rahisi hivyo
 
Hongera kufanikiwa kuhitimu Kidato cha Sita.

Nafahamu haikuwa safari nyepesi hasa Kwa Shule uliyosoma na matokeo unayotarajia kuyapata.

Nami pia nilipita hiyo Shule unayosema, japo ni miaka mingi iliyopita.

Naomba nikushauri tofauti kama ikikupendeza.

Tafuta passport kabla ya Mwezi July uwe umepata, then anza kuomba Vyuo vya Nje iwapo utakuwa na ufauru mzuri

Nenda kasome fani za Uhandisi iwe ni Civil engineering, ama Uhandisi wa Vifaa tiba.

Na iwapo utapenda kusoma IT, nenda kasome Ulinzi wa Taarifa na udukuzi kwenye vyuo vya Ulaya na Marekani

Umeona juzi baadhi ya Taasisi za Serikali zilivyodukuliwa

Unaweza kukuta IT wao wengi wamesomea hapa hapa Bongo ambapo teknolojia waliyotumia kujifunza unakuta ni zile Free Download

Ukifanikiwa kuhitimu huko Nje, ni rahisi kuajiriwa Huko huko ama Nchi zozote Africa kutokana na Ubora wa Elimu
 
Achana na shule mdogo wangu.. njoo dar uanze kupiga Winga, baadae utakuwa kama Fredy vunja bei.. shule unaenda kupoteza muda na unaweza ukaferi..

Anza kutafuta pesa mapema kwenye business, kuajiriwa ni utumwa wa kulipwa.

Business is hard but is really way to achieve what you want .
 
Umesema Accounting and Finance? Hiyo nzuri Ila wewe unataka nn ndani yako ?
Hata hiyo naweza kusoma. Ila mkuu sio kwamba ina watu wengi sana? Au ni hofu yangu tu. Mimi nikaenda kusoma hiyo accounting najiamini naweza pata GPA ya 4 or above kwa sababu chuo Ndio karibu na maisha
Kama ni nzuri sana naweza kusoma mkuu
 
Back
Top Bottom