Nisome Diploma ipi Kati ya hizi

Nisome Diploma ipi Kati ya hizi

Joined
Jun 11, 2019
Posts
34
Reaction score
16
Ndugu zangu naombeni mawazo yenu, nisome diploma ipi Kati ya hizi. Nina vigezo vyote vya kujiunga na hizi kozi.

Mimi nataka kozi itakayo nipa fursa ya kujiajili na kuajiliwa

Diploma in pharmaceutical sciences

Diploma in electrical and biomedical engineering

Diploma in clinical medicine

Diploma in medical laboratory

Diploma in mechanical engineering

Diploma in electrical and electronic engineering

Diploma in Accounting and Finance

Diploma in Business Administration
 
Clinical Medicine kwa sasa haina ishu utatumbukia kwenye umaskini hasa kama utakosa chance ya kusoma Md....Sikushauri kwa sasa maana hata kujiajiri ni ngumu ukikosa kazi serikali utategemea vijiwe ulipwe buku 10-15 kwa shift...naendelea kuchambua

Pharmacy nzuri hasa kama una mtaji wa kujiajiri utatoboa boss

Medical lab nayo nzuri ila si sana kama pharmacy nayo inafaa kujiajiri ila vyema ushirikiane na mtu wa pharmacy....

Accountancy watu wanaidharau lakini kozi nzuri hasa ukiwa mjasiria mali pia kama ukapata sehemu ya kuajiriwa nzuri kama Mashirika umeula boss...

Naendelea
 
Bussiness administration nayo kama Accountacy tu kaka(post ya juu hapo nimechanganya kumbe ipo)

Kwahiyo mimi kwa ushauri wangu ni huu

Clinical Medicine soma ukiwa na lengo la kuwa Md hapo utafanikiwa japo utapoteza miaka 10..kama huna lengo hilo piga chini utakuwa kama mwalimu tu labda upate kazi serikalini na bado pia mshahara uko chini na utaenda vijijini kabisa kufanya kazi

Pharmacy kwangu hii ndo best kwa kozi za afya kama unahitaji kujiari

Medical lab nzuri ila inapendeza ukijiajiri uwe na pharmacy hapo utapiga hela.

Accountacy na Bussiness administration nimeshakushauri

Zilizobaki sina ujuzi nazo asubuhi njema
 
feyzal, Umemwambia kinadharia, watu wengi binafsi wanafungua zahanati na sana sana health centre, na wengi hawana uwezo wa kumwajiri MD hivyo CO huwa wana Soko sana kwasababu atleast cheap ukilinganisha na MD. Hata ajira za government utakuta CO 200 na MD 50 tu kwasababu ni rahisi kuwalipa.

Kwa mfano Health centre inatakiwa iwe na MD mmoja wakati CO 4, zahanati huko CO ndo wanatakiwa na CA, Kikubwa kinachompa CO ajira kirahisi na kama nilivyosema hapo juu, unafuu kwenye kuwalipa. So kama anataka ajira faster apige CO.

Ila kwa upande wangu ningemshauri apige diploma ya Lab, japo ajira zake sio nyingi kihivyo maana certificate wa hiyo kozi ndo wanachukuliwa wengi zaidi kwenye ajira. Faida yake ni moja, rahisi sana kupata chuo cha kufundisha, na pia kwasababu wengi wanafungua dispensary na health centre cheti cha mtaalamu wa maabara ni muhimu sana, so anaweza kupiga pesa.

Kuhusu pharmacy, labda uishi mjini, theoretically Inaonekana ni bonge la kozi ila practically sio rahisi hivyo kwenye ajira, ni kozi ambayo ili ikulipe unahitaji uwe na connection ya kutosha, maana ajira za kutangazwa kwa kozi hiyo sio nyingi sana na competition ni kubwa hasa kwa miaka ya hivi karibuni, but kama una connection utakula maisha.

Japo hujaitaja ila Nursing ni bonge la kozi ukitaka usisote mtaani piga hiyo kozi, iwe certificate au diploma, wew ni marketable, maana nurses ndo moyo wa hospital, na wanatakiwa sana, japo wanaume wengi hawaipendi hii kozi, ila mambo yamebadilika sana, Sio sawa na zamani. Watu wameelimika siku hizi.

Hizo zingine sizijui, so siwezi kuzizungumzia.

NB, ambacho nimekiandika ni from my experience sio blah blah za mitaani. Ni sehemu ambako nipo kwa miaka kadhaa sasa, so nilichoandika ndiyo hali halisi.

KARIBU....
 
Ya kwanza liko safi sana hiyo PHAMACETICALS poa sana
 
Japo hujaitaja ila Nursing ni bonge la kozi ukitaka usisote mtaani piga hiyo kozi, iwe certificate au diploma, wew ni marketable, maana nurses ndo moyo wa hospital, na wanatakiwa sana, japo wanaume wengi hawaipendi hii kozi, ila mambo yamebadilika sana, Sio sawa na zamani. Watu wameelimika siku hizi.
Ushauri kuntu, hata huko majuu ukiwa na cheti kizuri ni rahisi kupata kazi. Bahati mbaya kama ulivyosema bado vijana wengi halija waingia hilo.

Na sasa tuna degree pia na huko mbeleni kuna masomo ya specialisation ambayo watu wa nursing na medicine hawapishani kama Public Health na pia Epidemiology.
 
Ushauri kuntu, hata huko majuu ukiwa na cheti kizuri ni rahisi kupata kazi. Bahati mbaya kama ulivyosema bado vijana wengi halija waingia hilo.

Na sasa tuna degree pia na huko mbeleni kuna masomo ya specialisation ambayo watu wa nursing na medicine hawapishani kama Public Health na pia Epidemiology.
Ahsanteni sana wakuu kweli mko nondo sana
 
Back
Top Bottom