Nisingesema: Wanaokumbuka Misri Tukiwakubalia ...

Nisingesema: Wanaokumbuka Misri Tukiwakubalia ...

KUGUSWA HAINA SHIDA, MAFISADI WAKUBWA NA MAPAPA NI KAMA AKINA LOWASSA NA HAWA AKINA KIKWETE, wanafuta kila aina ya uthibitisho na mahakamani unashindwa kesi mkuu

ebu acheni umaskini wa akili huo
kama mahakamani tunashindwa kesi na hawa mafisadi,kuna ulazimagani wakuwanazo mpaka sasa??mpaka ungwe hii hakuna alie silimishwa napata mashaka na hii safari,Mussa alifanya maajabu yakiungu hata kabla jua halija chomoza
 
Tumekubali kuondoka Misri lakini hatutaki kiongozi wa Msafara wetu atoke katika familia ya ki-Pharaoh. Ndiyo maana Musa hakuwa na uhusiano wowote na wana wa Misri.
ndugu Musa alilelewa katika familia ya farao kama watoto wa farao lakini alipoona ndugu zake waisrael wananyanyasika na asingeweza kuwasaidia kwani bado alikua mwanafamilia wa farao alichukua maamuzi magumu ya kukataa kuishi katika familia hiyo kwani hali ingechafuka wanafamilia hawakumtaka tena ndipo aloondoka nje ya familia hiyo
huu mfano ungemfaa sana Nd.Mhe.E N Lowassa sema tu bahati haikua upande wake
 
Unajua kuwa hata Waisraeli kabla tu hawajafika nchi ya ahadi walijikuta wanatamani kurudi Misri? Tena baada tu ya kuvuka Bahari ya Shamu? Japo walikuwa watumwa Misri lakini kule Misri walikuwa na uhakika wa maisha yao, walikula nyama na vyakula vyenye vitunguu saumu; na nina uhakika walikuwa comfortable in their misery (walistarehe katika shida zao!). Na hata wakati Musa anawatuma Joshua mwana wa Nuni na Kalebu mwana Yefune kwenda kupeleleza ile nchi (na wenzao wengine) ni hawa wawili tu walirudi na mtazamo tofauti kwani wengine wote waliona jinsi gani hali yao itakuwa mbaya huko waendako kwani maadui wao walikuwa ni watu wakutisha!

.......
Imeandikwa hivi: ... siku ya kumi na tano ya mwezi wa pilil baada ya kutoka kwao nchi ya Misri. Na mkutano mzima wa wana wa Israeli ukawangun'unikia Musa na Haruni, huko barani; wana wa Israeli wakawaambia, Laiti tungalikufa kwa mkono wa BWANA katika nchi ya Misri tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulipokula vyakula hata kushiba; kwani mmetutoa huko na kututia katika bara hii, ili kutuua, kwa jaa kusanyiko hili lote. Kut. 16:1-3

Umefanya kitu nzuri kuanza kazi ya kuhubiri.
Ulisoma seminari weye au madrasa?

Unaijua bei ya sukari ? Sio 1800.
 
Niambie mpaka leo hii ni fisadi gani ameguswa kati ya yale mafisadi yaliyofilisi hii nchi?

Mafisadi ya Escrow leo hayako uraini?

Baadhi ya watuhumiwa wa hii kashifa hawako kwenye cabinet yake?

Ya Lugumi,ya UDA,ya bilioni 9 za Ikulu(mazingira) n.k hayajui?
Mkuu umemsahau fisadi wa Richmond naye yupo uraiani.
 
Wengine bado tunasubiri kutoka mikononi mwa Farao, bado tuko utumwani
Siyo wote waliosema wanachukia kuwa Misri walimaanisha hivyo
Siyo wote walioshangilia kuondoka Misri walimaanisha hivyo
Siyo wote walioanza safari walikuwa wanataka kweli kuondoka
Siyo wote waliokaa kwenye safari waliweza kustahamili magumu ya safari
Siyo wote watafika mwisho wa safari!
Wewe unaota tu, hujaondoka wala huna nia ya kuondoka...bado umepiga kambi katika jumba la Farao, Rameses II na mkewe Nefretiri. Siku ukiamka utajikuta humo humo na watu wale wale katika mfumo ule ule...kalaghabaho!
Uamuzi ni rahisi kwa wengine - turudi Misri au tuondoke Misri; tatizo ni kuwa wengine waliondoka kimwili (physically) lakini kifikra (mentaly) na kiakili (pyschologically) walikuwa bado Misri.. Misri kulikuwa na utamu wake bana,
Nadhani ni wewe ndiye hujitambui...kimwili bado uko Misri ingawa kifikra na kiakili unajidanganya umeaga. Katika ndoto yako unawashangaa waliokataa kudanganyika kama wewe. Umewasaliti nduguzo kwa tamaa ya vinono vya Misri.
 
Inasikitisha kuona UKAWA wanapinga kila juhudi ya rais kuleta mabadiliko.. Mpaka wengine tunashangaa mbona wanayolilia sasa ni kutaka turudi kule kule tulipotoka?

Ukawa ni matapeli wakubwa wa siasa wananchi tumewakataa.

Rais piga kazi tunakuunga mkono.
 
Mzee wa kubongoa naona umerudi tena baada ya upepo kutulia kidogo!
naona kiuno kimeacha kumuuma,sasa nadhani yuko tayari kuendelea na kubong'oa!dume zima lina wabong'olea madume wenzie!ptuuuu!
 
Unajua kuwa hata Waisraeli kabla tu hawajafika nchi ya ahadi walijikuta wanatamani kurudi Misri? Tena baada tu ya kuvuka Bahari ya Shamu? Japo walikuwa watumwa Misri lakini kule Misri walikuwa na uhakika wa maisha yao, walikula nyama na vyakula vyenye vitunguu saumu; na nina uhakika walikuwa comfortable in their misery (walistarehe katika shida zao!). Na hata wakati Musa anawatuma Joshua mwana wa Nuni na Kalebu mwana Yefune kwenda kupeleleza ile nchi (na wenzao wengine) ni hawa wawili tu walirudi na mtazamo tofauti kwani wengine wote waliona jinsi gani hali yao itakuwa mbaya huko waendako kwani maadui wao walikuwa ni watu wakutisha!

Siwalaumu wala siwadharau wanaotamani Misri...

Kwani kwa wengine walipokuwa kule Misri ile ya kale...

Waliweza kuishi maisha mazuri katika utumwa wa watu wao
Waliweza kujenga na kufanikiwa
Waliweza kusomesha watoto wao popote wanapotaka hata kwenye vyuo vya Kifarao (pharaonic schools)
Waliweza kula na kunywa na kusaza
Waliweza kuvaa na kuvalishana
Waliweza kuishi kama wasio watumwa
Waliweza kustarehe

Wanapoambiwa kuwa sasa ni wakati wa kutoka; bila ya shaka hii ni kutaka kuwaondoa katika ukanda wa starehe zao (comfort zone). Hili linasumbua. Hawajui lugha ya mabadiliko, hawajui hata kama walikuwa wanatkaa kuondoka kweli. Inawezekana walihubiri na kusimulia watoto wao juu ya ile "ahadi" ambayo waliambiwa. Lakini wakati ulipofika walisita, walikasirika na kwa wanaokumbuka hata Musa mwenyewe alifika mahali alijikuta anajuta kwani muda kigogo mlimani aliporudi watu walikuwa wamechoka sanamu ya ndama wa dhahabu!

Na wengine ambao walikuwa wanapinga kutoka kule Misri walikuwa ni watu wakaribu kabisa na Musa!

Matokeo yake... matokeo yake... kati ya walioondoka Misri... walioamua kweli kuondoka Misri... ni 2 tu walioingia nchi ya ahadi! Pana funzo hapa!

Siyo wote waliosema wanachukia kuwa Misri walimaanisha hivyo
Siyo wote walioshangilia kuondoka Misri walimaanisha hivyo
Siyo wote walioanza safari walikuwa wanataka kweli kuondoka
Siyo wote waliokaa kwenye safari waliweza kustahamili magumu ya safari
Siyo wote watafika mwisho wa safari!

Uamuzi ni rahisi kwa wengine - turudi Misri au tuondoke Misri; tatizo ni kuwa wengine waliondoka kimwili (physically) lakini kifikra (mentaly) na kiakili (pyschologically) walikuwa bado Misri.. Misri kulikuwa na utamu wake bana,

Imeandikwa hivi: ... siku ya kumi na tano ya mwezi wa pilil baada ya kutoka kwao nchi ya Misri. Na mkutano mzima wa wana wa Israeli ukawangun'unikia Musa na Haruni, huko barani; wana wa Israeli wakawaambia, Laiti tungalikufa kwa mkono wa BWANA katika nchi ya Misri tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulipokula vyakula hata kushiba; kwani mmetutoa huko na kututia katika bara hii, ili kutuua, kwa jaa kusanyiko hili lote. Kut. 16:1-3
mkuu,hapo ulipo umebong'oa au umelala chali?
 
naona kiuno kimeacha kumuuma,sasa nadhani yuko tayari kuendelea na kubong'oa!dume zima lina wabong'olea madume wenzie!ptuuuu!
Wakuu.... kuna limit ya matusi aisee

Ni kweli MMM kabadilika sana, hata vile ambavyo alikua anavikandya just April 2015 kwa sasa ni kama vimekua lulu ya thamani lakini kwenye kubong'oa na kuinama naona kama tunaenda below the belt

Mwanakijiji: magu ana mazuri mengi sana, and his intention is clear, lakini anahitaji sana msaada kwa kumwongoza au kumshauri afikie malengo, ila kuanza kunfanya kwamba yeye ametakasika ni mapema mnoooo, usiturudishe kule kwa akina Ulimwengu na ile makala ya "tumaini lililorejea"

badala ya kukaa na kumchekesha mfalme kutwa kucha, ni vyema ungemuandikia waraka (tena na hivi unavyopenda sana dini - we anza waraka wa mwanakijiji kwa magufuli), na uwe na waraka tofauti hata kila mwezi na ziwe za kumsaidia bila kumkashifu wala kumdharau.... utawasaidia zaidi watanzania na kumsaidia zaidi yeye (kuliko ata utakavyowasaidia watanzania) kumfanya awe mwenye busara zaidi... KUMBUKA HATA MFALME SULEIMANI HAKUPATA BUSARA KWA KUSIFIWA TU

tafakari
 
Je, tayari tumesha anza safari ya kuondoka Misri?
Je, tulikua tayari kwa safari ya kuondoka Misri?
Ikiwa tumeondoka Misri, Je tulijiandaa kuondoka kimwili au kimawazo?
Je, hatuta juta kuanza kwa safari ya kuondoka Misri ikiwa bado hata atuja maliza kuvuka bahari ya shamu?
Kiukweli maswali bado ni mengi na hayaonekani kua na majibu.
Ebu ngoja nimalizie kupiga ugali mie
 
Mussa aliondoka nyumba ya Farao, huyu wa kwetu bado yumo au naye katoka?
 
Tumekubali kuondoka Misri lakini hatutaki kiongozi wa Msafara wetu atoke katika familia ya ki-Pharaoh. Ndiyo maana Musa hakuwa na uhusiano wowote na wana wa Misri.
Mbona mliyetaka atuongoze naye ametoka huko huko kwa mafarao?
 
KUGUSWA HAINA SHIDA, MAFISADI WAKUBWA NA MAPAPA NI KAMA AKINA LOWASSA NA HAWA AKINA KIKWETE, wanafuta kila aina ya uthibitisho na mahakamani unashindwa kesi mkuu

ebu acheni umaskini wa akili huo

Siku hizi Kikwete naye anajumuishwa kwenye class ya mafisadi kama Lowasa? Lakini JPM bado anamheshimu sana kama mwenyekiti wake wa chama na mhisani wake aliyecheza kete ya turufu iliyomwezesha kuingia Ikulu.
 
Daah mwanakijiji andiko lako limesheheni ukweli tuu,Kwa waliofaidika tawala zilizopita sasa wanaona shida.Maana mategemeo yao ni tofauti na utawala huu.Goo Magufuli usirudi nyuma nchii ililiwa sana na watu.
 
Back
Top Bottom