Nisingesema: Wanaokumbuka Misri Tukiwakubalia ...

Nisingesema: Wanaokumbuka Misri Tukiwakubalia ...

Mwanakijiji utaendelea kumkufuru Mungu hadi lini ? Amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu , sembuse mwanadamu mwenye makandokando !
 
Niambie mpaka leo hii ni fisadi gani ameguswa kati ya yale mafisadi yaliyofilisi hii nchi?

Mafisadi ya Escrow leo hayako uraini?

Baadhi ya watuhumiwa wa hii kashifa hawako kwenye cabinet yake?

Ya Lugumi,ya UDA,ya bilioni 9 za Ikulu(mazingira) n.k hayajui?

Haya yanaitwa Magoli; kwani hata wakuguswa utatafuta magoli mengine na kuyapanga!
 
Swali , je ni kweli tumeondoka misri ? Tumeondokaje wakati walewale wamisri ndio wanatuchagulia mkuu wa msafara ?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
uko sawa kabisa mkuu
 
ccm ni ile ile source ni hotuba ya raisi wako sijaona jipya pale la kumpeleka mfanyakazi kwenye nchi ya kanaani.... Musa aliwaambia wana wa Israel wazi wazi huko waendako.. na hata huko njiani kuna majipu yalitumbuliwa lakini bado walikula nyama na mikate ingawa ilikuwa jangwani... na hata Musa mwenyewe hakuingia kanaani lakini alitengeneza watu walioamini hata kumpita yeye..Joshua na kalebu... sasa leo hii hata bunge tu unalifanyia fitina lisionwe live..itakuwa hayo mengine? wacha watu wakumbuke misri maana hadi sasa sijaona nia ya dhati ya kumsaidia mwananchi wa chini... au unadhani 2% ndio suluhisho?..
Ccm ndio maana inaendelea kudumu kwa sababu hukubali kujikosoa pia hubadilika.usioona mabadiko basi wewe ni mbumbumbu
 
Hii hoja ni nzuri sana,inapima pia utimamu wa akili.Nasikitika kuona baadhi ya wachangiaji wao wamepanda milimani kufunga na kuomba kwa shetani tusipate maendeleo.
 
How

How? wakati ww mwenyewe uliyeimba mabadiliko kwa sasa unataka kurudi Misri!!


Yaani hadi inasikitisha; wengine walivyohubiri jinsi gani ufisadi ni mbaya sasa hivi wanataka tutamani kurudi kule; na huu ni mwezi wa sita tu! Siku kumi na tano tu toka watoke Misri Waisraeli walianza kutamani "masufuria ya nyama!"
 
sasa hivi nafikir sio uzee tu unaokusumbua, nafikiri una busha na tezi dume kwa pamoja
Sasa wewe una PhD ya nini?...labda ya upumbavu!...ujinga unatamalaki kwa "wanamabadiliko"..jikite kwenyee hoja na si kelele za matusi.
 
Tatizo Mzee huyu huwa anaeleweka kwa asilimia ndogo sana...nimekwepa kutaja namba kwani mada itabadilika na kuharibu kila kitu.
 
Unajua kuwa hata Waisraeli kabla tu hawajafika nchi ya ahadi walijikuta wanatamani kurudi Misri? Tena baada tu ya kuvuka Bahari ya Shamu? Japo walikuwa watumwa Misri lakini kule Misri walikuwa na uhakika wa maisha yao, walikula nyama na vyakula vyenye vitunguu saumu; na nina uhakika walikuwa comfortable in their misery (walistarehe katika shida zao!). Na hata wakati Musa anawatuma Joshua mwana wa Nuni na Kalebu mwana Yefune kwenda kupeleleza ile nchi (na wenzao wengine) ni hawa wawili tu walirudi na mtazamo tofauti kwani wengine wote waliona jinsi gani hali yao itakuwa mbaya huko waendako kwani maadui wao walikuwa ni watu wakutisha!

Siwalaumu wala siwadharau wanaotamani Misri...

Kwani kwa wengine walipokuwa kule Misri ile ya kale...

Waliweza kuishi maisha mazuri katika utumwa wa watu wao
Waliweza kujenga na kufanikiwa
Waliweza kusomesha watoto wao popote wanapotaka hata kwenye vyuo vya Kifarao (pharaonic schools)
Waliweza kula na kunywa na kusaza
Waliweza kuvaa na kuvalishana
Waliweza kuishi kama wasio watumwa
Waliweza kustarehe

Wanapoambiwa kuwa sasa ni wakati wa kutoka; bila ya shaka hii ni kutaka kuwaondoa katika ukanda wa starehe zao (comfort zone). Hili linasumbua. Hawajui lugha ya mabadiliko, hawajui hata kama walikuwa wanatkaa kuondoka kweli. Inawezekana walihubiri na kusimulia watoto wao juu ya ile "ahadi" ambayo waliambiwa. Lakini wakati ulipofika walisita, walikasirika na kwa wanaokumbuka hata Musa mwenyewe alifika mahali alijikuta anajuta kwani muda kigogo mlimani aliporudi watu walikuwa wamechoka sanamu ya ndama wa dhahabu!

Na wengine ambao walikuwa wanapinga kutoka kule Misri walikuwa ni watu wakaribu kabisa na Musa!

Matokeo yake... matokeo yake... kati ya walioondoka Misri... walioamua kweli kuondoka Misri... ni 2 tu walioingia nchi ya ahadi! Pana funzo hapa!

Siyo wote waliosema wanachukia kuwa Misri walimaanisha hivyo
Siyo wote walioshangilia kuondoka Misri walimaanisha hivyo
Siyo wote walioanza safari walikuwa wanataka kweli kuondoka
Siyo wote waliokaa kwenye safari waliweza kustahamili magumu ya safari
Siyo wote watafika mwisho wa safari!

Uamuzi ni rahisi kwa wengine - turudi Misri au tuondoke Misri; tatizo ni kuwa wengine waliondoka kimwili (physically) lakini kifikra (mentaly) na kiakili (pyschologically) walikuwa bado Misri.. Misri kulikuwa na utamu wake bana,

Imeandikwa hivi: ... siku ya kumi na tano ya mwezi wa pilil baada ya kutoka kwao nchi ya Misri. Na mkutano mzima wa wana wa Israeli ukawangun'unikia Musa na Haruni, huko barani; wana wa Israeli wakawaambia, Laiti tungalikufa kwa mkono wa BWANA katika nchi ya Misri tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulipokula vyakula hata kushiba; kwani mmetutoa huko na kututia katika bara hii, ili kutuua, kwa jaa kusanyiko hili lote. Kut. 16:1-3
Ningekuwa sijakutambua ningejitahidi kusoma andiko lako!
 
Safari ya taifa Letu haina Uhusiano Wowote na Safari ya wana wa Israel. Maana wao pamoja na kuwa na kiongozi shupavu Ugumu wa mioyo uliwafanya Safari ya siku 7 ichukue miaka 40.

Tanzania ilitoka Misri 1961/1964. zaidi ya 40 iliyopita siku moja na SINGAPOLE. Wenzetu walipitia Njia ya SIKU Saba angalau wanaona matunda na asali, Sisi hadi leo tuko jangwani tunatapatapa.

UPOFU (Usiri wa viongozi kwa wananchi) na UBABE (Hasa wa kutowasikiliza viongozi wa DIni) Kuliwafanya hata hao waliokwenda nchi ya ahadi iliririkayo maziwa na asali Kurudi Misri. Tena safari hii ilikuwa ni kwa LAZIMA sio Hiyari (Ukisoma Story ya kutoka Misri, Usisahau kupitia na Kitabu cha Yeremia Kutoka NCHI YA AHADI Kurudi tena Misri tena kwa UDIKTETA WA VIONGOZI(yeremia 43:2)).
 
warioba na kamati yake walizunguka nchi nzima wakatumia milioni 300 na zaidi halafu unataka niamini kipi kwenye nchi hii?haya maneno hayatasaidia kwa mla ugali na kibendu.
 
Ccm ndio maana inaendelea kudumu kwa sababu hukubali kujikosoa pia hubadilika.usioona mabadiko basi wewe ni mbumbumbu
wewe hujui chochote kuhusu nchi hii.. Leo hii nape kawa Waziri..makamba kawa Waziri...pole pole kawa Mkuu wa wilaya.. halafu unaniambia eti kuna mabadiliko! hakuna mabadiliko yatakayoletwa na ccm hata iweje ..ngoja kilo ya sukari ifike 5000 utajua ninachomaanisha
 
Mnatumia mpaka vitabu vya dini kuonyesha mnachokifanya sahihi hili la bunge tu limewashangaza wengi sasa hiyo nchi ya ahadi tutafikaje bila Uhuru Wa habari Na misri tumetokaje wakati tangu Uhuru anayeongoza ni huyu huyu kutoka misri kwa Tanzania ni siku nchi kuongozwa Na upinzani Wa chama chochote
 
Mussa wako wewe binafsi sio Mussa wa kila mtu

Mussa alifanya miujiza vyakula vikashuka....
huyu wako hana miujiza hiyo...hivyo watu wana haki ya kuhofia njaa mbele ya safari..
na hizi sio enzi za kuishi kwa miujiza na kwnda tu kwa kuamini...
 
Mussa wako wewe binafsi sio Mussa wa kila mtu

Mussa alifanya miujiza vyakula vikashuka....
huyu wako hana miujiza hiyo...hivyo watu wana haki ya kuhofia njaa mbele ya safari..
na hizi sio enzi za kuishi kwa miujiza na kwnda tu kwa kuamini...

Tatizo walituaminisha kuwa wanataka kwenda mbele na kwamba huko mbele kumejaa asali na maziwa, lakini ndani ya miezi sita wanasema bora kurudi kule kule tulikotoka. Mfano halisi, walisema posho, warsha viondolewe, lakini sasa wanataka posho na warsha virudishwe. Pili, rais ana safiri sana, sasa wanataka rais asafiri! The list is endless. confusaniiiii!
 
Back
Top Bottom