Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,741
- 40,868
Unajua kuwa hata Waisraeli kabla tu hawajafika nchi ya ahadi walijikuta wanatamani kurudi Misri? Tena baada tu ya kuvuka Bahari ya Shamu? Japo walikuwa watumwa Misri lakini kule Misri walikuwa na uhakika wa maisha yao, walikula nyama na vyakula vyenye vitunguu saumu; na nina uhakika walikuwa comfortable in their misery (walistarehe katika shida zao!). Na hata wakati Musa anawatuma Joshua mwana wa Nuni na Kalebu mwana Yefune kwenda kupeleleza ile nchi (na wenzao wengine) ni hawa wawili tu walirudi na mtazamo tofauti kwani wengine wote waliona jinsi gani hali yao itakuwa mbaya huko waendako kwani maadui wao walikuwa ni watu wakutisha!
Siwalaumu wala siwadharau wanaotamani Misri...
Kwani kwa wengine walipokuwa kule Misri ile ya kale...
Waliweza kuishi maisha mazuri katika utumwa wa watu wao
Waliweza kujenga na kufanikiwa
Waliweza kusomesha watoto wao popote wanapotaka hata kwenye vyuo vya Kifarao (pharaonic schools)
Waliweza kula na kunywa na kusaza
Waliweza kuvaa na kuvalishana
Waliweza kuishi kama wasio watumwa
Waliweza kustarehe
Wanapoambiwa kuwa sasa ni wakati wa kutoka; bila ya shaka hii ni kutaka kuwaondoa katika ukanda wa starehe zao (comfort zone). Hili linasumbua. Hawajui lugha ya mabadiliko, hawajui hata kama walikuwa wanatkaa kuondoka kweli. Inawezekana walihubiri na kusimulia watoto wao juu ya ile "ahadi" ambayo waliambiwa. Lakini wakati ulipofika walisita, walikasirika na kwa wanaokumbuka hata Musa mwenyewe alifika mahali alijikuta anajuta kwani muda kigogo mlimani aliporudi watu walikuwa wamechoka sanamu ya ndama wa dhahabu!
Na wengine ambao walikuwa wanapinga kutoka kule Misri walikuwa ni watu wakaribu kabisa na Musa!
Matokeo yake... matokeo yake... kati ya walioondoka Misri... walioamua kweli kuondoka Misri... ni 2 tu walioingia nchi ya ahadi! Pana funzo hapa!
Siyo wote waliosema wanachukia kuwa Misri walimaanisha hivyo
Siyo wote walioshangilia kuondoka Misri walimaanisha hivyo
Siyo wote walioanza safari walikuwa wanataka kweli kuondoka
Siyo wote waliokaa kwenye safari waliweza kustahamili magumu ya safari
Siyo wote watafika mwisho wa safari!
Uamuzi ni rahisi kwa wengine - turudi Misri au tuondoke Misri; tatizo ni kuwa wengine waliondoka kimwili (physically) lakini kifikra (mentaly) na kiakili (pyschologically) walikuwa bado Misri.. Misri kulikuwa na utamu wake bana,
Imeandikwa hivi: ... siku ya kumi na tano ya mwezi wa pilil baada ya kutoka kwao nchi ya Misri. Na mkutano mzima wa wana wa Israeli ukawangun'unikia Musa na Haruni, huko barani; wana wa Israeli wakawaambia, Laiti tungalikufa kwa mkono wa BWANA katika nchi ya Misri tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulipokula vyakula hata kushiba; kwani mmetutoa huko na kututia katika bara hii, ili kutuua, kwa jaa kusanyiko hili lote. Kut. 16:1-3