Nishaurini, mwanamke anapokuwa chanzo cha umaskini

Nishaurini, mwanamke anapokuwa chanzo cha umaskini

mkuu inaonekana pesa unapata kirahisi sana ndio maana sioni kama unamanisha kwenye malalamiko yako vinginevyo ungeshatoka nduki siku nyingi sana
 
hilo la ikulu hujalisema ila nilitaka kukuonyesha kuwa wapo watu wanafanya makubwa zaidi ya kuongea na wanasiasa kwenye simu na ni matapeli wakubwa. Imagine mtu anaingia na kushinda ikulu miaka 7 na hashtukiwi!! Ulivyokosa hata kopi za kadi za magari uliwahi kujiuliza swali lolote? Una hakika na majina yake anayotumia/aliyojitambulisha kwako? Amesoma wapi na kamaliza mwaka gani? Akikwambia alikosoma sekondari na chuo ni kazi rahisi kufatilia kama ni kweli. Ni usumbufu lakini inakusaidia kumfahamu mtu anayeficha mambo yake. Hiyo miradi yake ni miradi inayohusu nini ambayo we ni mbumbumbu huwezi kuelewa? Navyoandika hapa nacheka maana nishakutana na kituko kinachofanana na hiki. Jamaa kila siku anaongelea projects, mara amechelewa ofisini alikuwa ana-sign cheque za ku-execute project halafu baada ya mwezi akaniomba nimuazime milion kadhaa kuna project alishachukua dola 25,000 akatumia kwa project binafsi bla bla.....bahati mbaya jamaa alikosea mahesabu. Mi uwezo hata wa kumpa laki 2 sina. Wasiwasi wangu usikute huyo bibie ana connections na watu wa hatari akakutia matatani maana akikulewesha penzi kakaangu utakuja kulia. Kuna principle moja "in doubt, never act". Kama umeweza kuwaza waza haya unayowaza ni alama ya onyo, usishupaze shingo kakaangu. Hapo ulipofika panatosha. Hawa watu wanavutia sana kuwa nao maana wanaonekana kuwa na akili na hawaboi kukaa nao, na kwa vile haeleweki eleweki unatamani uendelee kuwa naye maana nawe unajikuta una-enjoy mchezo wa kumtafuta ili uje umbane kwenye kona.

Na unakubalije gari yake ikae kwako wakati ushasema hata kadi hujawahi kuona? Hala hala bro. Mahaba upofuuu

huko serena kweli sijawahi enda. Niliishiaga tu calabash enzi hizo na hela kubwa niliyowahi lipa ni 20,000. Tehe

sina cha kuongeza wala kupunguza asipofuata haya ulompa
baaas
 
Gracious
1. chombo cha usafiri (Ndege, ma3...)?
2. Ndani ya Muda mfupi anabadilisha magari (So what/why? umedadisi?)
3. anafika kwako (umefika kwake/kwao?? bado? why?)
4. kununua nguo kila siku (mfano nakaa Mbezi mwisho, akija naenda posta kununua nguo ndo tutoke? unafanya/anafanya kazi saa ngapi)
5. CM ya mkulu muda wowote (Hapa naona yale ya "Baba na Mwana" kutoka na Seya yanakunyemelea)?
6. ana manage project (hapa wewe ni moja ya project hizo-so usiogope)

NB: Lakini hii ingefaa uwaone Bongo movie ungepata pesa nzuri!
 
Last edited by a moderator:
Wanawake wooooote umekosa ndo umeona huyo, haya mitaa yote, vyuo vyote hapa mjini, ofisi zote hapa mjini ndo umeona huyo. Pole
 
Ndugu zangu,Miezi mitatu iliyopita nilikutana na binti mmoja mrembo sana kwenye chombo cha usafiriIlikua ni usiku,baada ya kukaa sehemu moja nikawa nime anzisha conversation ambayo mwanzoni haikupokelewa vizuri lakini baada ya kuonekana kusisitiza basi maongezi yakanoga.

Huyu binti ndani ya muda mfupi alinieleza mambo yake mengi mwishoni tukabadilishana namba za simuBaada ya kuagana kesho yake nikaomba appointment ambayo haikukataliwa tukaonanaIkawa kila siku nikitoka kazini ananitafutanikiwa kazini ananifuata ananisubiri jioni twende nyumbani Ilichukua wiki moja tu tangu kufahamiana nikawa nimejuana nae.

Ikawa ni kila siku asubuhi saa nne anakuja kazini kwangu jioni ananisubiri anipeleke home.Anabadili magari ndani ya wiki moja anakuwa na zaidi ya magari mawili tofauti.Tangu nimefahamiana nae amekuwa akiendesha Rav 4,Mark X,Brevis,Murrano na Benz, haya ndiyo amekua akibadili zaidi.

Huyu binti ana connection kubwa sana na wanasiasa kuanzia mkulu hadi wengineo wakubwa wote sio chama tawala.sio upinzani Kwake kupiga kwa mkulu ni kawaida.Tatizo langu kubwa nikimuhoji kinagaubaga kazi yake ni nini ananijibu anamanage projects mbalimbali kitu ambacho sijawahi kukielewa kabisa it doesnt click na ukimuhoji sana ili kujua specifics mnagombana.

Mimi kazi yangu siyo ya kipato kikubwa kihivyooo.Lakini binti anaamua tu kwenda sehemu ambazo ni za gharama kwangu bila kunitaarifu alafu nikifika ananiambia ni settle bill.Kwa mfano one day akawa ananisubiri mjini kumuuliza uko wapi.

Akaniambia niko serena njoo kufika ameshaspend laki 3 mimi kwangu hio ni kubwa sana hasa kama sikupanga then ananipa mimi ni settle hajanitaarifu before kwamba tunaenda pale.

Kubadili nywele mara mbili kwa wiki nikimwambia hiyo siwezi sina pesa ugomvi naambiwa mimi bahili.Katika movement zote of course ni mimi nimekuwa nikizigharamikia.Akija kwangu kuna nguo zake ameachahataki kuzivaa tena kila akija anataka nimnunulie nguo nyingine ya kuvaa kesho yake.Kwa hio kwa wiki anataka mnunue nguo saba.

Kumpenda nampenda lakini naona kama ananirudisha nyuma.Nimemkalisha kumweleza aelewe hali halisi.Mgumu kunielewa,tunagombana then.Tatizo langu lingine hapa hata kama una pesa vipi mipangilio ni muhimu huyu binti wangu haelewi na hapo mnagombana.

Jamani nikosoeni nishaurini kama kuna kitu nakosea.

Huyu co mwanamke wa kujenga halaf mbona amekuonesha tabia yk mapema na jibu unalo nikupe hongera kwa moyo wakutoa mwanaume cku hiz wamekuwa wagumu mno angalau umenijibu swali langu lililokuwa linanosumbua kumbe bd wapo wenye roho za kuhonga ovyo
 
Mkuu kwa hizo sifa zote ulizozitoa, huyo mdada atakuwa ni mjane-aliachika yupo frustrated kwa hiyo kwako anajaribu ku kujiliwaza. Pia kuna uwezekano mkubwa akawa ni tapeli.
 
Back
Top Bottom