Nishaurini, mwanamke anapokuwa chanzo cha umaskini

Nishaurini, mwanamke anapokuwa chanzo cha umaskini

Mkuu tayta nahisi nampenda na nisingependa kumpoteza...nilidhani naweza kumrekebisha katika hili.

Ni miezi mitatu niko nae...ndio maana nimeomba mnikosoe ,kama ni ujinga pia mniambie...kama kuna kitu naweza fanya kuendelea kuwa nae na akabadilika niambieni......

mzani bado haujakaa sawa...nimeona sifa zake mbaya ambazo ni mtia gharama zinazozuilika na mficha siri ya kazi yake...ili apimwe vyema ungetaja sifa nzuri alizo nazo zidi ya kusema ''nahisi nampenda''
 
Huyo sio mwanamke kwanza ni changudoa.Pili anania ya kukuchuna hana mpango na wewe.ushauri achana naye
 
mzani bado haujakaa sawa...nimeona sifa zake mbaya ambazo ni mtia gharama zinazozuilika na mficha siri ya kazi yake...ili apimwe vyema ungetaja sifa nzuri alizo nazo zidi ya kusema ''nahisi nampenda''

Hahahahaha,She is beautiful,Anakwepo wakati wote nikimhitaji,ananiskiliza katika mengine isipokua hizo kasoro,Amejitoa sana kwangu....ila tyta hili swali lako limenifumbua akili...haha
 
kaka jiulize mambo yafuatayo
kwanza muda wa kukufata fata anaupata wapi na project anafanya saa ngapi?
mkiagana asubuhi anaenda wapi na ulisha fika kwake au ofisini kwake?
Ulisha kutana na rafiki yake yeyote katika kipindi chote au kusikia mazungumzo yake na simu mkiwa wote ana pigiwa kuzungumza mambo gani?
kwanino alale kwako alafu aje bila nguo ya kuvaa kesho yake?na je nguo unazo mnunulia ni code gani i mean casual.au za ofisi?
Mwisho anaweza kuwa changudoa aliyetokea katika familia ya kifahari ila yeye binafsi hana mawe wala lolote.gari anachukua tu za ndugu.
 
laki 3 siku moja.......duh...

ni hivi mwanamke anaweza kukufanya kuwa na maendelea na pia anaweza kukufanya ukafilisika......sasa wew chagua unataka mwanamke wa aina gani.....

kama viatu vinakubana viache....using'ang'anize ukasema vitatanuka mbeleni...mana siyo vyote vinatanuka......jipime kama unaona hivyo viatu si.size yako.....achana navyo tafuta vinavyokutosha ili utembee kwa raha......
 
Mkuu tayta nahisi nampenda na nisingependa kumpoteza...nilidhani naweza kumrekebisha katika hili.

Ni miezi mitatu niko nae...ndio maana nimeomba mnikosoe ,kama ni ujinga pia mniambie...kama kuna kitu naweza fanya kuendelea kuwa nae na akabadilika niambieni......

Mkuu ilituupate uhalisia wa hiki unachokiongea,hebu toa invoice ya gharama alizokupa kwa hii miezi 3 uliyodumu nae?
 
Last edited by a moderator:
"Kila siku saa 4 asubuhi anakuja ofisini Kwako" - Ukiona mtu hana ishu kati ya saa 3 asubuhi Mpaka saa 7 mchana muogope sana.

Huyo ni mpigaji, hapo anakupanga tu ipo siku utakuta account yako nyeupe na vitu vyako vyote kwako vimekombwa
 
Hebu ngoja nichekeeeeeee....

Hv upo sawa upstairs had uendeshwe na mapenzi tena ambayo unaona hayana tija.!?

Cut off all ties na huyo demu, kama kiboksi manyoya tafta hata housegal mkali jiran punguza uchupa. Haf huyo wa matumiz akihoji vp mbona kimya mwambie ulikuwa waishi kwa hela za mkopo hivo akusapoti yy had uwe back on ur feet. Hapo ndii utajua je yy ni mtoaji na ana malengo nawe au ni mtumiaji kaja kuchuna mbuzi
 
huyo sio demu ni m-pesa
By MO11 wa JF
 
Last edited by a moderator:
kaka jiulize mambo yafuatayo
kwanza muda wa kukufata fata anaupata wapi na project anafanya saa ngapi?
mkiagana asubuhi anaenda wapi na ulisha fika kwake au ofisini kwake?
Ulisha kutana na rafiki yake yeyote katika kipindi chote au kusikia mazungumzo yake na simu mkiwa wote ana pigiwa kuzungumza mambo gani?
kwanino alale kwako alafu aje bila nguo ya kuvaa kesho yake?na je nguo unazo mnunulia ni code gani i mean casual.au za ofisi?
Mwisho anaweza kuwa changudoa aliyetokea katika familia ya kifahari ila yeye binafsi hana mawe wala lolote.gari anachukua tu za ndugu.

Nguo anazovaa ni dress code ya ofisini na zingine sio
Muda mwingi anapigiwa simu....she talks about kazi and the so...but kazi gani ambayo mtu hana hela...hua sipati jibu
Ofisini kwake sijafika
Nyumbani kwake nimefika...amepanga maeneo ya bahari b
Kisingizio kazi zake ni za kuzunguka sana.
Sasa hata kama ni uchangudoa anaufanya muda gani wakati muda mwingi yuko na mimi
 
Sasa hata kama ni uchangudoa anaufanya muda gani wakati muda mwingi yuko na mimi

Hiyo maana yake ni kwamba wewe ndio kazi yake. Yani anapokuwa na wewe ndio yupo ofisini hivyo kwahiyo jipange, wewe una clear bills za laki tatu kirahisi halafu unasema hana kazi!! Wewe ndio kazi yake
 
Mkuu ilituupate uhalisia wa hiki unachokiongea,hebu toa invoice ya gharama alizokupa kwa hii miezi 3 uliyodumu nae?

Hakuna invoice ...lakini roughly ni zinazidi milioni mbili na nusu...nimezitumia kutokana na kuwa na yeye
 
Back
Top Bottom