mmmmmmh....jamani hii chai kama imezidi kapilipili manga kwa mbaaali! Hicho chombo cha usafiri mlikokutana bila shaka ni ndege maana kwa magari aliyo nayo haiwezi kuwa mlikutana kwenye daladala au bajaji za jero jero. Kama hii sio chai mpe heko huyo mwanamke mwenzangu na wewe nakupa pole kijana mwenzangu. Hizo brevis na murano sijui rava 4 ulishawahi tek trabo ya kuhakiki umiliki japo kwa kuchungulia kadi zake? Kama ni tapeli huwezi kuta document yeyote kwenye gari, sijui wanafichaga wapi. Au ukopi namba za magari yake yote ukafanye ujasusi wako huko wanakosajili magari. Na huko nyumbani kwake BAHARI BICHI kwi kwi kwi......ushaenda mara ngapi? Kama anaweza kuazima magari hashindwi kubebwa. peleleza utajua nyumba ni ya nani. Jina je ushahakikisha ni lake halisi? Umewahi kuona ID yake yeyote katika hiyo miezi mitatu? rafiki je? hata akuonyeshe kwenye picha zilizoko simuni.
Huko kukufata kazini asubuhi na jioni usifikiri ni mahaba bali mbinu za kukudhibiti usipate muda wa kufikiri hiki unachofikiri hapa au kumchunguza.
Halafuuu, kama anakufata kazini saa 4 na kuja kukuchukua baada ya kazi ina maana huna gari - asubuhi unapanda lifti au daladala, jioni honey anakuja kukupik. Kama ndivyo, si rahisi kutembea na wallet iliyotuna kwa sababu za kiusalama. Sasa em tuambie ile siku uliyokuta bili ya laki 3 serena ulilipaje lipaje? au ulienda ukiwa umejihami? Na hayo matumizi ya laki 3 kwa mtu mmoja hebu tupe mchanganuo wake isije ikawa walikuwa watatu kabla hujafika. Najua mtasema kuna vinywaji vya mpaka laki 5 kwa tot lakini hii haiji.
Kwamba binti anaingia ikulu kama nakumat nayo sijui kama ni hoja ya maana sana maana ni miaka kama miwili imepita tangu nione itv mtu akikamatwa baada ya kugundulika kujifanya afisa usalama wa taifa kwa muda mrefu na alishatapeli wengi, na ikulu alikuwa akionekana sana. Yaani mtu hana kazi nyigine we ndo kazi yake???? Bora hata akutie umaskini utatafuta hela nyingine, mi nina wasiwasi zaidi ya huo.