Kwanza, . Farao alikuwa dikteta wa kikatili akitekeleza matumizi mabaya ya kutisha na mateso ya Israeli, ambao wawezekana kuwa na idadi ya zaidi ya watu milioni 1.5 wakati huo. Mafarao wa Misri walikuwa wamewaweka Waisraeli utumwani kwa miaka 400. aliamuru kwamba watoto wa kiume waisraeli wauwawe wakati wa kuzaliwa (Kutoka 1:16). Farao ambaye Mungu aliufanya moyo wake mgumu alikuwa mtu mbaya, na taifa lenye alitawala lilikubaliana naye, au angalau halikupinga, matendo yake maovu.
Farao na Misri, walikuwa wamejiletea hukumu hii juu yao wenyewe kwa miaka 400 ya utumwa na mauaji ya halaiki. Tangu mwanzo mshahara wa dhambi ni mauti (Warumi 6:23), Farao na Misri, walikuwa wametenda dhambi za kuogofya dhidi ya Mungu, ingekuwa haki tu kwa Mungu ku ameangamiza Misri kabisa. Kwa hivyo, Mungu kuufanya moyo wa Farao mgumu iliikuwa ni haki, na kuleta mapigo mengine ya ziada dhidi ya Misri ilikuwa si kudhuluma.
Mwisho warumi 9 14-24
14 Tusemeje basi? Kwamba Mungu ana upendeleo? La, sivyo. 15 Kwa maana Mungu alimwambia Musa, “Nitamrehemu nipendaye kumrehemu; na nitamhurumia nipendaye kumhurumia.” 16 Kwa hiyo haitegemei mapenzi ya mtu au jitihada ya mtu, bali hutegemea huruma ya Mungu. 17 Kwa maana katika Maandiko Farao anaambiwa, “Nilikuinua kwa makusudi ya kudhihirisha nguvu zangu kwako na jina langu lipate kutangazwa duniani pote.” 18 Kwa hiyo basi, Mungu humhurumia mtu ye yote apendaye kumhurumia na huufanya mgumu moyo wa mtu ye yote atakaye.
19 Bila shaka mtaniuliza, “Kama ni hivyo, kwa nini Mungu anatulaumu? Kwa maana ni nani awezaye kushindana na mapenzi yake? 20 Lakini wewe mwanadamu, una haki gani ya kumhoji Mungu? Je, kilichotengenezwa kinaweza kumwuliza aliyekitengeneza, “Kwa nini umenitengeneza hivi?” 21 Je, mfinyanzi hana haki ya kufa nya apendavyo na udongo wake? Je, si anaweza kabisa kutumia sehemu ya udongo huo kutengeneza chombo kimoja kitumikacho kwa kupamba na kutoka katika udongo huo huo akatengeneza kingine kwa matumizi ya kawaida?