officialBossmtoto
JF-Expert Member
- Jul 1, 2019
- 369
- 1,178
Mimi ni Mkristo Mkatoliki na napenda sana dini yangu. Ila zaidi napenda sana kujifunza hasa pale ambapo panakua na ugumu ama mkanganyiko.
Narudia tena, nitaomba mnisamehe kama nakosea ila nina swali nahitaji kufahamishwa.
Tunaambiwa kwenye Biblia kwamba Mungu alimtuna Musa(Moses) akawakomboe wana wa Israel kutoka mikono ya Farao(Pharaoh) na akampa maelekezo namna ya kufanya ili Farao aweze kumuelewa. Lakini Mungu pia akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu asikubaliane na ujumbe wa Musa. Sasa swali langu ni kwamba, Je? Mungu alikua anatafuta sababu ya kumuangamiza Farao? Maana pengine asingefanya moyo wa Farao kua mgumu, pengine Farao angekubali tu kwamba sawa enendeni maana Mungu wenu amewataka muende nchi ya ahadi.
Tunaambiwa Mungu wetu anaruhusu Free Will yaani Ruksa ya kufanya maamuzi mwenyewe, je mbona aliingia maamuzi ya Farao? Mbona aliufanya moyo wa farao kuwa mgumu?