Nisamehe kama nakufuru, nahitaji kufahamishwa

Nisamehe kama nakufuru, nahitaji kufahamishwa

Haya uliyoyaandika ni mtazamo wako kwa namna ambavyo unamfikiria Mungu ama ni references kutoka kwenye bible ambapo una ushahidi wa kimaandiko?

Mdau katoa hoja kupitia reference ya biblia sasa unaposema Mungu hakufanya moyo wa farao kuwa mgumu unatuacha njia panda tuhisi kwamba unapinga hilo andiko kwamba limepotosha

Exodus 9:12 But the LORD hardened Pharaoh's heart and he would not listen to Moses and Aaron, just as the LORD had said to Moses.

Mimi nakubaliana na mtoa mada kwamba Mungu aliufanya moyo wa farao kuwa mgumu kwa reference hiyo hapo juu, wewe unapinga kua mungu hafanyi mioyo ya watu kuwa mgumu kwa reference ipi?
Kosa lililopo hapa ni kuwa simulizi hili linasomwa kama historia.

Simulizi hilo sio historia. Kuna mambo ya kuangalia katika simulizi hilo.

Hayo ni mazingira au tamaduni za wakati huo, mwandishi wa hilo simulizi aliwaandikia kina nani, lengo la mwandishi lilikuwa ni nini. Simulizi hili lina ujumbe gani kwetu; sisi tunaoishi baada ya hao walioandikiwa?

Je, hayo umeyazingatia? Tunaposoma biblia tuache kufikiri kuwa ni matukio ya kila siku yaliyotokea.

Biblia ni neno la Mungu sio matukio ya kila siku ya watu; kazi za kiakili sio matukio ya kila siku ya watu.
 
Mwanangu dini zote ni nyenzo za kikoloni na kinyonyaji. Ni ukoloni wa kimila ambapo mila za kigeni zinapewa kipaumbele na kukamua utajiri toka kwetu. Hivyo, hujakufuru. Biblia na Koran ni hekaya za abwunasi zilizopewa jina la maneno ya Mungu. Ni utapeli mtupu mwanangu. Fumbo la Imani, Kristu Alikufa, Kristu Alifufuka Kristu atarudi tena LINI? Akili kichwani mwako. Fumbo la imani, Mtume alitokewa na malaika huko Jabar Hila. Nani alishuhudia? NANI? TUMIA AKILI YAKO.
 
Inshort Mungu aliufanya moyo Mgumu wa farao asikubali kuwa Kuna Mungu...Kama adhabu ya matendo Yake mabaya alowafanyia Wana waisrael.....

Watendao mabaya wakaiona kweli na wakaitaaa (Hii ni adhabu au laana kutoka kwa Mungu. kutokana na matendo yao wenyewe)...

Yoyote haya yaweza mfika...akiamua kukataa kuona kweli
 
Kiasili binadamu anaweza kutambua uwepo wa Mungu pasipo dini. Mazingira ya ulimwengu yanatoa picha kwamba kuna Mungu.

Mimi nasema Mungu wa "kweli" huwezi kumtambua bila kupitia dini ya kweli, nakubaliana kwamba mtu anaweza kutambua uwepo wa Mungu kupitia mazingira na hata fikra za mtu mwenyewe (placebo) lakini Mungu wa aina hiyo huwa ni Mungu wa mashaka na ndio maana nasema Mungu wa kweli ni yule anayejidhihirisha mwenyewe kwa watu wamtafutao kupitia dini na dini hiyo ndiyo inayoitwa dini ya kweli kwakuwa inakuwa imeletwa na huyo Mungu wa kweli kupitia mitume na manabii wake.

Lakini pia, mimi naamini hakuna dini ya kweli na haitakaa iwepo. Ila imani ya kweli juu ya Mungu ipo.

Dini ya kweli ipo dini za uongo zipo halikadhalika imani za ukweli na uongo zipo pia.

Imani za ukweli zinatoka kwa huyo Mungu wa kweli na hizo imani zimo katika dini ya kweli.

Swali ni dini ya kweli ni ipi???
 
Mimi nasema Mungu wa "kweli" huwezi kumtambua bila kupitia dini ya kweli, nakubaliana kwamba mtu anaweza kutambua uwepo wa Mungu kupitia mazingira na hata fikra za mtu mwenyewe (placebo) lakini Mungu wa aina hiyo huwa ni Mungu wa mashaka na ndio maana nasema Mungu wa kweli ni yule anayejidhihirisha mwenyewe kwa watu wamtafutao kupitia dini na dini hiyo ndiyo inayoitwa dini ya kweli kwakuwa inakuwa imeletwa na huyo Mungu wa kweli kupitia mitume na manabii wake.

Dini ya kweli ipo dini za uongo zipo halikadhalika imani za ukweli na uongo zipo pia.

Imani za ukweli zinatoka kwa huyo Mungu wa kweli na hizo imani zimo katika dini ya kweli.

Swali ni dini ya kweli ni ipi???
Kwa mujibu wa biblia
Yakobo 1 :27

"Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu."

Na urahisi ni kwamba Yesu alishatoa maswali tutakayoulizwa Mbinguni yako wazi kabisa.

Mathayo 25:35-40

"kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi."

Tujitahidi kutenda mema mbwembwe za. Dini za kileo na madhehebu rutaziacha hapahapa.
 
Mimi ni Mkristo Mkatoliki na napenda sana dini yangu. Ila zaidi napenda sana kujifunza hasa pale ambapo panakua na ugumu ama mkanganyiko.
Narudia tena, nitaomba mnisamehe kama nakosea ila nina swali nahitaji kufahamishwa.

Tunaambiwa kwenye Biblia kwamba Mungu alimtuna Musa(Moses) akawakomboe wana wa Israel kutoka mikono ya Farao(Pharaoh) na akampa maelekezo namna ya kufanya ili Farao aweze kumuelewa. Lakini Mungu pia akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu asikubaliane na ujumbe wa Musa. Sasa swali langu ni kwamba, Je? Mungu alikua anatafuta sababu ya kumuangamiza Farao? Maana pengine asingefanya moyo wa Farao kua mgumu, pengine Farao angekubali tu kwamba sawa enendeni maana Mungu wenu amewataka muende nchi ya ahadi.

Tunaambiwa Mungu wetu anaruhusu Free Will yaani Ruksa ya kufanya maamuzi mwenyewe, je mbona aliingia maamuzi ya Farao? Mbona aliufanya moyo wa farao kuwa mgumu?
Farao alikua ni mpotevu na mkana Mungu Kutoka 5:1-3. Na Mungu aliona hatima ya Farao lazima apotee tu. Hivo kupitia kuufanya moyo wa Farao kua mgumu Mungu alikua amelenge kuwajenga kiiimani na kuwaweka tayari wana wa Israel ktk kukabiliana na tabu na kumtegemea yeye ambao kwa wakati huo walikua hawako tayari ata kuondoka Misri...

Tusome hii nukuu hapa chini inaweza kutusaidia

The Hebrews had expected to obtain their freedom without any special trial of their faith or any real suffering or hardship. But they were not yet prepared for deliverance. They had little faith in God, and were unwilling patiently to endure their afflictions until He should see fit to work for them. Many were content to remain in bondage rather than meet the difficulties attending removal to a strange land; and the habits of some had become so much like those of the Egyptians that they preferred to dwell in Egypt. Therefore the Lord did not deliver them by the first manifestation of His power before Pharaoh. He overruled events more fully to develop the tyrannical spirit of the Egyptian king and also to reveal Himself to His people. Beholding His justice, His power, and His love, they would choose to leave Egypt and give themselves to His service. The task of Moses would have been much less difficult had not many of the Israelites become so corrupted that they were unwilling to leave Egypt. {PP 260.2}
 
Mimi nasema Mungu wa "kweli" huwezi kumtambua bila kupitia dini ya kweli, nakubaliana kwamba mtu anaweza kutambua uwepo wa Mungu kupitia mazingira na hata fikra za mtu mwenyewe (placebo) lakini Mungu wa aina hiyo huwa ni Mungu wa mashaka na ndio maana nasema Mungu wa kweli ni yule anayejidhihirisha mwenyewe kwa watu wamtafutao kupitia dini na dini hiyo ndiyo inayoitwa dini ya kweli kwakuwa inakuwa imeletwa na huyo Mungu wa kweli kupitia mitume na manabii wake.

Dini ya kweli ipo dini za uongo zipo halikadhalika imani za ukweli na uongo zipo pia.

Imani za ukweli zinatoka kwa huyo Mungu wa kweli na hizo imani zimo katika dini ya kweli.

Swali ni dini ya kweli ni ipi???
Wakristo wanatunza siku ya saba yaani wasabato
 
Kwa mujibu wa biblia
Yakobo 1 :27

"Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu."

Na urahisi ni kwamba Yesu alishatoa maswali tutakayoulizwa Mbinguni yako wazi kabisa.

Mathayo 25:35-40

"kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi."

Tujitahidi kutenda mema mbwembwe za. Dini za kileo na madhehebu rutaziacha hapahapa.

Neno dini maana yake nini??
 
Utasemaje yesu alikuwa mwanae mpendwa kwa Mungu wakati yesu ndio Mungu mwenyewe?
Yes ni Mungu mwana au hujui hilo, aisehh we ndugu ni mbishi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jibu swali langu kwanza, mimi ndiye nimeanza kukuuliza.

Ukijibu, nitakujibu.

Hata ukijibu kwa kusema hujui jibu tu nalo ni jibu.
Uwepo wa Mungu hiyo ni mada pana sana mkuu tukianza hapa tutatoka nje mada na tukaweka mkanganyiko kwenye mtiririko wa wachangiaji, na pia ishajadiliwaga humu pia, ila we jua tu kua nina amini Mungu yupo na vielelezo vipo
 
Kwani mimi nimesema huamini?

Unaelewa hata swali nililouliza ni lipi?
 
Kama ukitaka kumwelewa Mungu vyema inakulazimu utoke kwenye mduara wa dini kwanza.
These are the million of reason for your question
Mungu na dini ni maji na mafuta
Toka utawani huko katafute maarifa hata china
 
Back
Top Bottom