Nisamehe kama nakufuru, nahitaji kufahamishwa

Nisamehe kama nakufuru, nahitaji kufahamishwa

Mkuu na mimi nakujibu Hivi:
Mungu wetu ni Mungu wa Sifa anapenda kuabudiwa kupewa sifa na utukufu na hapendi tuabudu miungu mingine maana ni Mungu Baba mwenye wivu.

Sasa Misri hawakua wakimuabudu Mungu Baba wao waliabudu Miungu mingine toka enzi na enzi na lakini pia kwa wakati ule kusudi la Mungu lilikua ni kuwaokoa watu wake wa taifa teule yaan Israel pekee na ndio hata ukisoma Biblia agano la kale sana linawaongelea wana wa israel na si watu wa mataifa kwa sababu ndio waliochaguliwa na lengo la Mungu lilikua ni kuona wanamuabudu yeye Mungu pekee. Maana walikua chini ya torati na sheria na si neema kama sasa ( neema kwa wote ilikuja baada ya Bwana Yesu Kristo kuja)

Sasa Mungu alimpa pharaoh Moyo Mgumu kwa nini? Ni kwa sababu kwanza pharaoh na misri yote waliabudu Miungu mingine na si Mungu Baba.

Pili Mungu alitaka kudhihirisha kua yeye ni Mungu pekee mkuu juu ya miungu mingine waliyokua wakiitegemea.

Na pia lengo halikua kumuumiza Pharaoh ila ilikua ni kuurejesha moyo wake kutambua yupo Mungu Mmoja mkuu anayeishi na anayepaswa kuabudiwa na kupewa sifa kupitia mapigo yote waliyopata.

Hata leo Mungu anawarejesha watu wake kumjua yeye na kumtambua ukuu wake kupitia yale wanayopitia yawe mazuri kwa macho au mabaya kwa macho. Asante
Farao alikua ni mpinga Mungu na huyu ndio muumini wa imani ya hakuna Mungu ambayo siku hizi wanaiita Atheism yaani wakana Mungu.

Mungu anaefahamu mwanzo na mwisho wa kila mwanadamu alifahamu vyovyote vile atakavyofanya Farao hatobadilika. Na ndio sbbu ya kuufanya moyo wake kua Mgumu. Kwahiyo Mungu hakuingilia utashi huru wa Farao....


Naomba unijibu hili swala. Nini maana ya neema?
 
Mimi ni Mkristo Mkatoliki na napenda sana dini yangu. Ila zaidi napenda sana kujifunza hasa pale ambapo panakua na ugumu ama mkanganyiko.
Narudia tena, nitaomba mnisamehe kama nakosea ila nina swali nahitaji kufahamishwa.

Tunaambiwa kwenye Biblia kwamba Mungu alimtuna Musa(Moses) akawakomboe wana wa Israel kutoka mikono ya Farao(Pharaoh) na akampa maelekezo namna ya kufanya ili Farao aweze kumuelewa. Lakini Mungu pia akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu asikubaliane na ujumbe wa Musa. Sasa swali langu ni kwamba, Je? Mungu alikua anatafuta sababu ya kumuangamiza Farao? Maana pengine asingefanya moyo wa Farao kua mgumu, pengine Farao angekubali tu kwamba sawa enendeni maana Mungu wenu amewataka muende nchi ya ahadi.

Tunaambiwa Mungu wetu anaruhusu Free Will yaani Ruksa ya kufanya maamuzi mwenyewe, je mbona aliingia maamuzi ya Farao? Mbona aliufanya moyo wa farao kuwa mgumu?
Aisee...
 
Mungu wakati wote hafanyi mtu awe na moyo mgumu.

Mungu hafanyi makosa, kazi zake ni njema pasipo kasoro, makosa, majeraha, uchungu au uharibifu.

Kosa kubwa ambalo watu wengi, asilimia 95 wanafanya ni kuwa hawajui maana na elimu ya Mungu.

Biblia sio kitabu cha rekodi za matukio ya kila siku, ni historia ya dini-teolojia.

Ni makosa kuitazama biblia kama matukio yaliofanyika kila siku wakati huo.

Biblia ni mafundisho ya imani na maadili. "Imani" na "maadili" ni mambo yalio kwenye akili. Kuhusu ulimwengu chanzo chao ni kipi na hatima yao ni nini, kipi kinachotakiwa kufanywa na mtu, ni kazi za kiakili.

Akili ndio inafahamu na ndio inafanya kila kitu. Akili ndio chanzo na hatima ya vitu vyote.

Akili ndio huitwa Mungu.
 
Ni simple mkuu, tukio la yesu kuwa special ni kutokana na hizi hoja hapa

1.alikua mwanae mpendwa Mungu aliyependezwa nae
2.lakin bado akampitisha katika mateso katika hali ya kibanadamu kwa kubeba msalaba wa mwanadamu
3. Mungu alimuachia yesu Kristo ajaribiwe na shetani mara nyingi zaidi


Hizo hoja hapo juu ndiyo zilimfanya yesu Kristo kuwa special zaidi, je unadhani kwanini Mungu akampitisha Yesu Kristo kwenye njia ngumu, njia yenye miba
Utasemaje yesu alikuwa mwanae mpendwa kwa Mungu wakati yesu ndio Mungu mwenyewe?
 
Ni simple mkuu, tukio la yesu kuwa special ni kutokana na hizi hoja hapa

1.alikua mwanae mpendwa Mungu aliyependezwa nae
2.lakin bado akampitisha katika mateso katika hali ya kibanadamu kwa kubeba msalaba wa mwanadamu
3. Mungu alimuachia yesu Kristo ajaribiwe na shetani mara nyingi zaidi


Hizo hoja hapo juu ndiyo zilimfanya yesu Kristo kuwa special zaidi, je unadhani kwanini Mungu akampitisha Yesu Kristo kwenye njia ngumu, njia yenye miba
Unahakikishaje huyo Mungu yupo kweli na habari zake si hadithi za kutungwa na watu tu?
 
Vibltabu vya fini vina maswali mengi sana. but COSMOLOGY is the one way to go. it sound beautiful it will make you freely from several contratictions, Ultimate Matrixes,Time,space nad energy.

So unapokuwa unatafuta maarifaa usijifungeee mwenyewe soma uone na wengine wanasemaje uone ipi ina sound Ukingiza woga wa dhambi hutoboi
 
Mungu wakati wote hafanyi mtu awe na moyo mgumu.

Mungu hafanyi makosa, kazi zake ni njema pasipo kasoro, makosa, majeraha, uchungu au uharibifu.

Kosa kubwa ambalo watu wengi, asilimia 95 wanafanya ni kuwa hawajui maana na elimu ya Mungu.

Biblia sio kitabu cha rekodi za matukio ya kila siku, ni historia ya dini-teolojia.

Ni makosa kuitazama biblia kama matukio yaliofanyika kila siku wakati huo.

Biblia ni mafundisho ya imani na maadili. "Imani" na "maadili" ni mambo yalio kwenye akili. Kuhusu ulimwengu chanzo chao ni kipi na hatima yao ni nini, kipi kinachotakiwa kufanywa na mtu, ni kazi za kiakili.

Akili ndio inafahamu na ndio inafanya kila kitu. Akili ndio chanzo na hatima ya vitu vyote.

Akili ndio huitwa Mungu.
Haya uliyoyaandika ni mtazamo wako kwa namna ambavyo unamfikiria Mungu ama ni references kutoka kwenye bible ambapo una ushahidi wa kimaandiko?

Mdau katoa hoja kupitia reference ya biblia sasa unaposema Mungu hakufanya moyo wa farao kuwa mgumu unatuacha njia panda tuhisi kwamba unapinga hilo andiko kwamba limepotosha

Exodus 9:12 But the LORD hardened Pharaoh's heart and he would not listen to Moses and Aaron, just as the LORD had said to Moses.

Mimi nakubaliana na mtoa mada kwamba Mungu aliufanya moyo wa farao kuwa mgumu kwa reference hiyo hapo juu, wewe unapinga kua mungu hafanyi mioyo ya watu kuwa mgumu kwa reference ipi?
 
Unapaswa kwanza kuelewa lengo la yaliyotokea zama hizo,
Kifupi hayo yote yalikuwa maandalizi ya ukombozi,kwa hiyo kila kilichotokea kilikuwa kinaandaa ujio wa Kristo,
Mimi ni Mkristo Mkatoliki na napenda sana dini yangu. Ila zaidi napenda sana kujifunza hasa pale ambapo panakua na ugumu ama mkanganyiko.
Narudia tena, nitaomba mnisamehe kama nakosea ila nina swali nahitaji kufahamishwa.

Tunaambiwa kwenye Biblia kwamba Mungu alimtuna Musa(Moses) akawakomboe wana wa Israel kutoka mikono ya Farao(Pharaoh) na akampa maelekezo namna ya kufanya ili Farao aweze kumuelewa. Lakini Mungu pia akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu asikubaliane na ujumbe wa Musa. Sasa swali langu ni kwamba, Je? Mungu alikua anatafuta sababu ya kumuangamiza Farao? Maana pengine asingefanya moyo wa Farao kua mgumu, pengine Farao angekubali tu kwamba sawa enendeni maana Mungu wenu amewataka muende nchi ya ahadi.

Tunaambiwa Mungu wetu anaruhusu Free Will yaani Ruksa ya kufanya maamuzi mwenyewe, je mbona aliingia maamuzi ya Farao? Mbona aliufanya moyo wa farao kuwa mgumu?
 
Mungu haufanyi moyo wa mtu mgumu...Bali mtu huufanya moyo wake mgumu kwa matendo Yake ukitenda dhambi sanaaaa moyo wako unakuwa mgumu...kiasi Kwamba hata Ukiona Haki na KWELIutaikataaa....


Farao alijiita Mungu kwanzia Musa hajazaliwa ...alifanya ukatili mkuubwa Sana ....kwa watu kiasi Kwamba moyo wake ukawa mgumu kutokana na matendo Yake....

Mwenyezi Mungu amekuonesha mema na mabaya..lakini wewe unachagua mabaya na unayateta na kuyoana Ni mema... Na mema unayatakaaa... Moyo wako unakuwa mgumu... Mungu anakuziba masikio...macho na Wala hutokaaa uione KWELI... Hiii kufanya moyo wako mgumu Ni laana kutoka kwa Mungu kutokana na matendo yako mwenyewe ...

Asante
 
Na huwezi kumpata Mungu wa kweli nje ya dini ya kweli.

Dini ya kweli ni ipi?? Hilo ndilo swali la kwanza.
Kiasili binadamu anaweza kutambua uwepo wa Mungu pasipo dini. Mazingira ya ulimwengu yanatoa picha kwamba kuna Mungu.

Lakini pia, mimi naamini hakuna dini ya kweli na haitakaa iwepo. Ila imani ya kweli juu ya Mungu ipo.
 
Mungu haufanyi moyo wa mtu mgumu...Bali mtu huufanya moyo wake mgumu kwa matendo Yake ukitenda dhambi sanaaaa moyo wako unakuwa mgumu...kiasi Kwamba hata Ukiona Haki na KWELIutaikataaa....


Farao alijiita Mungu kwanzia Musa hajazaliwa ...alifanya ukatili mkuubwa Sana ....kwa watu kiasi Kwamba moyo wake ukawa mgumu kutokana na matendo Yake....

Mwenyezi Mungu amekuonesha mema na mabaya..lakini wewe unachagua mabaya na unayateta na kuyoana Ni mema... Na mema unayatakaaa... Moyo wako unakuwa mgumu... Mungu anakuziba masikio...macho na Wala hutokaaa uione KWELI... Hiii kufanya moyo wako mgumu Ni laana kutoka kwa Mungu kutokana na matendo yako mwenyewe ...

Asante
Kwa hiyo biblia inavyosema Mungu alimfanya farao awe na moyo mgumu ilikuwa na maana gani.
 
Mungu humpa ufalme amtakae..Mungu humuongoza amatakae...Mungu Ni mwingi wa rehema....Farao bado Mungu alimpenda Sana akampa Ufalme na utajiri mkuubwa...

Lakini kutokuona Neema ya Mungu juu yetu... Watu huchagua njia za kuwaangamiza wenyewe....wanajua mbaya lakini waafanya Tena na Tena na Tena.... Hivyo Mungu anaweka pazia kwenye macho yao..na masikio..hutosikia muadhana Wala mnadi swala... Na mwisho utaangamia... Lakini chanzo Ni matendo yetu na machaguo yetu wenyewe..
 
Kwa hiyo biblia inavyosema Mungu alimfanya farao awe na moyo mgumu ilikuwa na maana gani.
Kuwa Mwenyezi Mungu hufanya mioyo Migumu ya wale watenda zambi....na Mungu alijua ufahari wa farao na kujiona Mungu ...kamwe asingeweza kubali kuwa Kuna Mungu zaidi Yake....

Na farao alitenda dhambi za kuchupa mipaka..... Moyo wake ukawa mgumu ..kutokana na matendo Yake..
Na laana ya Mungu juu Yake Ni kuangamia kwa kufanya moyo wake mgumu asipokeee mafundisho ya Musa ...

Ili Mungu atuoneshe Mwisho wa tenda dhambi....




Mungu
 
Haya uliyoyaandika ni mtazamo wako kwa namna ambavyo unamfikiria Mungu ama ni references kutoka kwenye bible ambapo una ushahidi wa kimaandiko?

Mdau katoa hoja kupitia reference ya biblia sasa unaposema Mungu hakufanya moyo wa farao kuwa mgumu unatuacha njia panda tuhisi kwamba unapinga hilo andiko kwamba limepotosha

Exodus 9:12 But the LORD hardened Pharaoh's heart and he would not listen to Moses and Aaron, just as the LORD had said to Moses.

Mimi nakubaliana na mtoa mada kwamba Mungu aliufanya moyo wa farao kuwa mgumu kwa reference hiyo hapo juu, wewe unapinga kua mungu hafanyi mioyo ya watu kuwa mgumu kwa reference ipi?
Mungu aliona tangu awali kua Farao ni mpotofu na anayajua maisha ya kila mwanadamu tangu mwanzo hadi mwisho.


Farao alikua ni mkana Mungu na mpinga Mungu na maandiko haya hapa chini yanadhihirisha hivo.



Kutoka 5 1
Hata baadaye, Musa na Haruni wakaenda wakamwambia Farao, wakasema, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Wape watu wangu ruhusa waende, ili kunifanyia sikukuu jangwani.

Kutoka 5 2
Farao akasema, BWANA ni nani, hata niisikilize sauti yake, na kuwapa Israeli ruhusa waende zao? Mimi simjui BWANA, wala sitawapa Israeli ruhusa waende zao.

Kutoka 5 3
Wakasema, Mungu wa Waebrania amekutana nasi; twakuomba, tupe ruhusa twende safari ya siku tatu jangwani, tumtolee dhabihu BWANA, Mungu wetu; asije akatupiga kwa tauni, au kwa upanga.


Fungu la pili ktk hii Kutoka linaonyesha ukana Mungu wa Farao. Linaonyesha upinga Mungu wa Farao...kwahiyo Mungu alitambua mwanzo hatima ya Farao na ndio sbbu akafanya kua na moyo mgumu ili ashuhudie ukuu wa Mungu na awaruhusu watu wa Mungu



The Hebrews had expected to obtain their freedom without any special trial of their faith or any real suffering or hardship. But they were not yet prepared for deliverance. They had little faith in God, and were unwilling patiently to endure their afflictions until He should see fit to work for them. Many were content to remain in bondage rather than meet the difficulties attending removal to a strange land; and the habits of some had become so much like those of the Egyptians that they preferred to dwell in Egypt. Therefore the Lord did not deliver them by the first manifestation of His power before Pharaoh. He overruled events more fully to develop the tyrannical spirit of the Egyptian king and also to reveal Himself to His people. Beholding His justice, His power, and His love, they would choose to leave Egypt and give themselves to His service. The task of Moses would have been much less difficult had not many of the Israelites become so corrupted that they were unwilling to leave Egypt. {PP 260.2}
 
Back
Top Bottom